Kulikoni Dkt. Magufuli kutohudhuria karamu ya Mabalozi Ikulu?

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Nimeshangazwa kidogo kwa kitendo cha Rais Dkt Magufuli kuwaandalia karamu ya kuukaribisha mwaka mpya, mabalozi na Maafisa wa kimataifa waliopo nchini na kisha yeye mwenyewe kumtuma waziri wake wa mambo ya nje kumwakilisha.

Kwa maoni yangu naamini hili ni kosa la kiufundi hasa ikizingatiwa kuwa Magufuli ndio ameanza tenure yake kama Rais na hivyo angepaswa kutumia fursa hiyo kikamilifu ili kujenga taswira yake vema kimataifa kupitia kile anachokiamini na kusimamia.

Taarifa iliyorushwa na vyombo vya habari haikusema ni dharura gani aliyokuwa Mhe Rais ilihali yupo nchini.
1454998189265.jpg
1454998175539.jpg
1454998161575.jpg
 
Nimeliona na kujiuliza . Nadhan suala la Zanzibar ni mtihani mgumu sana. So lazima ausome vizuri na kujipanga
 
Nimesoma sehemu humu kwamba Waziri alikuwa na kikao nao kujadili mambo kadhaa likiwemo suala la kuwashauri hao "marafiki" wa Maalim Seif Hamad wamshawishi ashiriki uchaguzi sikuwa nafahamu kama ni sherehe/karamu
 
Nimeshangazwa kidogo kwa kitendo cha Rais Dkt Magufuli kuwaandalia karamu ya kuukaribisha mwaka mpya, mabalozi na Maafisa wa kimataifa waliopo nchini na kisha yeye mwenyewe kumtuma waziri wake wa mambo ya nje kumwakilisha.

Kwa maoni yangu naamini hili ni kosa la kiufundi hasa ikizingatiwa kuwa Magufuli ndio ameanza tenure yake kama Raisi na hivyo angepaswa kutumia fursa hiyo kikamilifu ili kujenga taswira yake vema kimataifa kupitia kile anachokiamini na kusimamia.

Taarifa iliyorushwa na vyombo vya habari haikusema ni dharura gani aliyokuwa Mhe Rais ilihali yupo nchini.
Kwani mkalimani hakuwepo?
 
Kwenye kikao palikua na wazungu??? Lugha gani ilikua inatumika??
 
Sasa naanza kuamini lugha ya kiingereza ni tatizo kubwa kwa mkuu wa kaya. Na kwa vile sasa hivi yeye kusifiwa ni fashion anajua litakuwa gumzo la nchi. Anajua ni jinsi gani atawaangusha wale wote wanaomsifia tu.Hapo ndio siri ya urembo ua kutokusafiri ama kukutana na wanaotumia lugha ya malkia.
 
Sijui atakimbia hivi hadi lini? Ni bora akafungua darasa la kiingereza pale Magogoni. Mbona walimu wazuri wa kiingereza hata humu JF wamo?
 
Hata mimi nimeona kwenye habari nikashangaa sana, Mheshimiwa huyu kwa kweli hasomeki kabisa...!!
 
Back
Top Bottom