IKULU: Rais Magufuli anapokea Hati za Utambulisho kwa Mabalozi wapya wa Marekani na Vietnam 🇻🇳

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Agosti, 2020 atapokea Hati za Utambulisho za Mabalozi Wateule wa Marekani na Vietnam hapa nchini. Tukio hili litarushwa mubashara na vyombo vya habari kuanzia saa 9:00 alasiri kutoka Ikulu, Dar es Salaam.

Kumekucha karibu balozi wa watu wa Marekani.

Amefika wakati muafaka kabisa kuwakilisha maslahi mapana ya watu, serikali na nchi ya Marekani hapa Tanzania.

Marekani kama kaka mkubwa na pia mjomba wa nchi nyonge ambaye hasiti kutetea demokrasia, uhuru wa kupashana habari na utu wa mtu hatasita kufanya ushawishi hali hiyo itamalaki nchini Tanzania.
Tamko Kuelezea Masikitiko Yetu Kuhusu Uhuru wa Kujieleza na Ushiriki Jumuishi wa Kisiasa
Ubalozi wa Marekani umesikitishwa na hatua za hivi karibuni za Serikali ya Tanzania za kuminya demokrasia, ikiwa ni pamoja na kuwakamata viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wakiwa katika vikao vyao vya ndani na kufuta leseni ya gazeti la chama cha siasa cha upinzani. Hatua hizi ni mwendelezo wa mlolongo wa matukio ya kusikitisha ya vitisho kwa wanachama wa vyama vya upinzani, asasi za kiraia na vyombo vya habari. Haki ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza ni mambo yaliyojumuishwa na yanayolindwa na Katiba ya Tanzania na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu. Ubalozi wa Marekani unafahari kusaidia na kuunga mkono uhuru wa kujieleza na ushiriki jumuishi wa kisiasa kwa namna zote.
Source:
Tamko Kuelezea Masikitiko Yetu Kuhusu Uhuru wa Kujieleza na Ushiriki Jumuishi wa Kisiasa | Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
By U.S. Embassy Dar es Salaam | 25 Juni
 
Mmarekani kaingia na barakoa, kufika ndani kwa Mzee Baba kaivua ye pamoja na wenzake wawili
Watampelejea taarifa Trump kuwa Tanzania Corona hamna tumeingia na barakoa Ikulu wakawa wanatushangaa sababu hamna mwenye barakoa

Na Bila Shaka wameona mitaani kote walikopita wananchi hawana barakoa

Watatusaidia kukanusha uongo wa balozi aliyeendoka ambaye kutwa Alikuwa akipeleka taarifa za uongo Washington

Lisu naye alikuja na ushamba na kibarakoa chake akijiona anajuaaaaaa!!! Kufika airport akijiona super hero kashangaa wanaompokea hakuna aliyevaa barakoa .Kwa aibu akalivua huku wengine wakimshangaa na kumzomea yeye na mkewe kwa kuvaa barakoa .Wakiwaona Ni washamba Fulani hivi
 
Kumekucha karibu balozi wa watu wa Marekani.

Amefika wakati muafaka kabisa kuwakilisha maslahi mapana ya watu, serikali na nchi ya Marekani hapa Tanzania.

Marekani kama kaka mkubwa na pia mjomba wa nchi nyonge ambaye hasiti kutetea demokrasia, uhuru wa kupashana habari na utu wa mtu hatasita kufanya ushawishi hali hiyo itamalaki nchini Tanzania.
Hawa ni wenzetu tunatengeneza ndege kwao kwa fedha taslim
 
Hawa jamaa hawaamin Kama cc hatuna korona ee!
IMG_20200802_160624_0.jpg

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Sina hakika Balozi wa TZ akipokelewa USA, taarifa yake itakuwa ktk hardnews magazeti siku ya pili.Sisi huku eti mubashara!?

Lazima serikali ya CCM Mpya ijipendekeze kwa kaka mkubwa na mjomba wa nchi masikini kama yetu inayopokea misaada kibao toka kwa Hisani ya Watu wa Marekani.
 
JPM ni bingwa wa diplomasia ya kiuchumi Tanzania bado inahitaji huduma yake kwenye nafasi ya urais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Agosti, 2020 atapokea Hati za Utambulisho za Mabalozi Wateule wa Marekani na Vietnam hapa nchini. Tukio hili litarushwa mubashara na vyombo vya habari kuanzia saa 9:00 alasiri kutoka Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Agosti, 2020 atapokea Hati za Utambulisho za Mabalozi Wateule wa Marekani na Vietnam hapa nchini. Tukio hili litarushwa mubashara na vyombo vya habari kuanzia saa 9:00 alasiri kutoka Ikulu, Dar es Salaam.

Tatizo kesho tu tatawaita mabeberu wakati wametoa $600M kusaidia, Afya, Kilimo na Lishe.
 
Back
Top Bottom