Hebu niambie katika Dunia ya social network, utaenda meza ya magazeti ili ufanye nini?
Yaani ukae kusikiliza dj leo atapiga nyimbo gani redioni wakati una app kama youtube?
Taarifa ya habari uisubiri mpaka saa mbili usiku, tena utangaziwe habari iliyochujwa kwa manufaa ya watu fulani wakati habari hiyo unaweza kuipata kwenye social network muda ule ule inapotokea tena bila kuchujwa.
Ndugu, dunia ilipofikia, TV, redio na magazeti hayana maana
Hata kipindi zinaingia TV flat, wenye machogo walikua wabishi, lakini leo hii ukiwa na chogo watu wanakushangaa.