Kuleni vyote, acheni kubagua bagua vyakula alivyoumba Mungu!

Kuleni vyote, acheni kubagua bagua vyakula alivyoumba Mungu!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Naamini umeishakutana na watu wasemao: “Mimi sipendi ndizi, sipendi dagaa, mimi sipendi parachichi, sitaki mboga fulani, sitaki kula chakula hiki wala kile, chakula changu ni chips mayai na soda.” Tabia hii ya kubagua bagua vyakula inapingana na hekima ya Mungu aliyeumba vyakula. Mungu sio mjinga; kila alichokiumba kina maana na faida katika mwili wa mwanadamu.

Maandiko yanasema:
“Kwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema, wala hakuna kitu chochote cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani, kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba..” (1 Timotheo 4:4-5)

Hii inatufundisha kwamba chakula chochote kilichoumbwa na Mungu kina faida. Waulize nutritionists, watakuthibitishia ukweli huo, kwamba kila aina ya chakula hubeba virutubisho maalum. Hakuna chakula kimoja peke yake kinachoweza kukupa virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini. Ndiyo maana Mungu aliumba aina nyingi za vyakula. Hivyo ukikataa baadhi ya vyakula, unakataa baraka na hekima ya Mungu aliyeumba vyakula vinavyotufaa.

Mara nyingi wanaosema: "Mimi sili mihogo, sili mchicha, sili chakula hiki au kile, utakuta wana upungufu wa virutubisho (nutrient deficiency) na hatimaye huathirika kiafya kwa kupatwa na magonjwa yatokanayo na kutokula vyakula fulani.

Ukibagua bagua vyakula, siku ukiugua na kukimbilia hospitali, usishangae daktari akikuambia utafute vyakula vile vile ulivyovikataa awali. Hata hivyo, watu wengi huambiwa hivyo wakati afya zao tayari zimeishaharibika!
 
Mwanzo 1:1-30:
Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia...akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe.. mwanaume na mwanamke aliwaumba...kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote, na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa chakula chenu. Nao wanyama wote wa nchi, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.

Umeyaelewa Maandiko hayo? Mungu hajasema tule vyakula fulani tu, anapenda tule aina zote za matunda, mboga na wanyama. Hivyo ndugu yangu, usidharau wala usibague chakula chochote ambacho Mungu alikiumba. Kila aina ya chakula ni muhimu katika kuimarisha afya zetu. Hivyo, kataa tabia ya kusema: “Mimi sipendi hiki, sipendi kile.” Badala yake, mshukuru Mungu kwa vyote.
 
3 Yohana 1:2
Mpendwa, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo.
 
Nikabugie mududu Leo jioni mbona hujasema kuhusu pombe, pombe tamu sana
 
Nikabugie mududu Leo jioni mbona hujasema kuhusu pombe, pombe tamu sana
Mungu hakuumba pombe. Achana na mipombe hiyo inayoharibu akili zako na kukuingizia sumu mwilini. Kunywa vitu natural.
 
Mkuu mbona hujagusia kwenye mdudu? Unachenga chenga tu
 
Ukipata diabetes au hypertension akili itakaa sawa.
By the way Mungu akulinde mtumishi na akuweke mbali na maradhi my sister.
 
Back
Top Bottom