Kuleni hela za wagombea, kura msiwape...na T-shirt vaaaeni.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuleni hela za wagombea, kura msiwape...na T-shirt vaaaeni....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtu66, Oct 4, 2010.

 1. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Askofu Mokiwa: Kuleni hela za wagombea, kura msiwape
  Monday, 04 October 2010 07:56 0

  [​IMG]Askofu Mkuu wa kanisa la Anglican Tanzania,Valentino Mokiwa,akizungumza Dar es salaam jana,wakati wa uzinduzi wa huduma ya Bina ya afya ya imani,kwa watu wenye kipato cha chini,Bima iliyoanzishwa na mtandao wa afya wa kanisa hilo.

  Michael Jamson
  ASKOFU mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Valentino Mokiwa amewakumbusha na kuwataka waumini wa kanisa hilo kupokea na kula pesa zote zinazotolewa na wagombea wa nafasi mbalimbali katika kampeni zinazoendelea nchi nzima akisema "fedha za namna hiyo si dhambi, haramu wala rushwa".

  Lakini Askofu Mokiwa akawakumbusha waumini kuwa fedha hizo zisiwafanye wawapigie kura wagombea wa namna hiyo kwa kuwa wanaotoa rushwa hiyo ni "wajinga na kula fedha ya mjinga bila ya kumtekelezea azma yake si kosa".Kiongozi huyo wa kidini alisema hayo wakati wa kuzindua mpango wa "Bima ya Afya ya Imani kwa Watu Wenye Kipato cha Chini".
  "Mnawajua wagombea wenye sifa na uwezo wa kuongoza, lakini hao wanaokuja kwa kuahidi vitu vingi na kutoa pesa hawafai hata kidogo kuchaguliwa,’’ alisema.

  "Pokeeni; kuleni lakini katu msimchague kwa maana kiongozi anayetanguliza hela hatufai; mtu wa namna hiyo mimi ninamuita mjinga na kula hela ya mjinga si haramu; si dhambi na wala si rushwa, ila tu usimtekelezee lile alilotaka kwa kutokumchagua," alisema.

  Kwa mujibui wa mpango wa bima hiyo, iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana eneo la Buguruni Malapa, mwanafamilia anatakiwa kulipia Sh60,000 kwa mwaka kama gharama za vipimo na matibabu ili atibiwa magonjwa matatu ambayo ni maralia, kifua na huduma za wanawake wajawazito.

  Alisema magonjwa aliyoyataja ndiyo yanayowasumbua watu wa kipato cha chini mara kwa mmara kutokana na hali na mazingira wanamoishi.
  Alisema katika maeneo mengi kumeibuka maduka ya dawa ambayo yako kibiashara zaidi kiasi cha kudiriki kuuza dawa bila hata kuona cheti kutoka kwa daktari.

  Alisema nao wananchi kutokana na kukwepa gharama za kumuona daktari, kupima na kununua dawa zinazozidi Sh10,000, huamua kwenda kwenye maduka hayo wanapojisikia dhaifu na kununua dawa.  Naye mwakilishi wa Mtandao wa Afya wa Anglikani, Japhet Makau alisema kwa bara la Afrika, Tanzania ni nchi ya kwanza kunufaika na huduma hiyo na kwamba itakuwa mkombozi mkubwa kwa watu wa kipato cha kawaida maana kanisa limelenga kuwaondolea adha zilizokuwa zikiwakabiri kwa muda mrefu.


  Kuleni hela za wagombea, T-shirt vaaaeni....Malori pandeni na chakula kuleni ....kura msiwape kwa sababu ni WAJINGA
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  tehteh CCM msumari mwingine huo.hahaaaaa
   
 3. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Namsubiri Tendwa Abwabwaje tena kwa huyu
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kura ni siri yako bwana so iyo mijihera ipokee bse ndo izo zilizo kwapuliwa kwa mgongo wa stimulus package,rich monduli,meremeta,radar.
  Infact ni kuwa wanazirudisha kwa walengwa inofficially
   
 5. u

  urasa JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tendwa amemjibu askofu Mokiwa kwa kusema askofu huyo kwa kauli yake ya kuwaeleza wananchi kuwa wale pesa za wagombea na kura wampe kiongozi anayefaa inamfanya askofu huyo kuwa sehemu ya rushwa.

  My take here:

  Askofu Mokiwa ana kosa gani kutoa elimu ya uraia hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu?

  Nani anakiuka sheria hiyo ya gharama ya uchaguzi anayoisema Tendwa?

  Hao wanaotoa rushwa ndio walisababisha maisha magumu kwa watu, wahujumu uchumi wakubwa, walikusanya hizo pesa na sasa wanazitumia kuwarubuni watu, tuzipokee hizo pesa, ni zetu na tuwanyime kura zetu!
   
 6. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sasa, atamjibu slaa, we subiri 2, utasikia mwezi hauishi
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  ccm-tendwa
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  anajua hii kauli itawaumiza CCM kwani ndio wahongaji wakubwa.......
   
 9. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tendwa inamuuma kusikia mwaka huu pesa za mafisadi ZITALIWA bila KURA...:A S 13:
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,937
  Trophy Points: 280
  Tendwa ni bogus kweli.

  Nimetoka kumsikiliza Askofu Kakobe mahubiri yake Star TV yale ambayo yalimtoa huko aliko Tendwa na kusema Kakobe na Yahaya wanakosea na nikajiuliza hivi Tendwa kweli kamsikiliza Kakobe kweli au wapambe kama Tambwe na Makamba ndio walimpa agizo la kusema hayo aliyosema?

  Kakobe alitoa darasa hasa la uraia bila ya upendeleo ila uwazi na ukweli kabisa. Na kwa vile walidhani baada ya tishio lile mahubiri yale hayatarushwa hewani basi wamejiingiza mkenge kwani kila mtu baada ya kuona Kakobe anazungumzia uchaguzi mkuu na ni kile alichokemewa, wakawa na hamu ya kusikia.

  Ukweli ni kuwa Kakobe kapiga rungu la kichwa na Tendwa atakuwa kaaibika sana kwani somo alilotoa Kakobe ni elimu ya uraia ambayo wananchi wa kawaida walipaswa kupewa na vyombo halali vya serikali.

  Hata yeye Kakobe alilisema hilo la kuwa ukipewa hongo kula tuu ila mchague yule atakaye kutoa katika lindi la umasikini. Kura inapigwa kwa siri na watu wasidanganywe kuwa watajulikana na hao wahongaji kuwa hawakuwapa kura. Hiyo ni elimu tosha kwa mwananchi wa kawaida hasa yule aliyeona asiachie kilo mbili za sukari na kanga kutokana na shida zake.

  Maneno ya Kakobe na Shk Yahaya kuyalinganisha ni matusi makubwa. Tendwa amuombe radhi Kakobe, na wengine wamuige Kakobe kufundisha uraia bila woga
   
 11. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  ccm hawaelewi kabisa kwa nini imekuwa hivi mwaka huu, walishadhani kwamba WaTz hawataamka .... na sasa wameamka lakini wao wanaona kama bado wako ndotoni na wakiamka watakuta mambo ni kama walivyozoea !! KWA MSEMO WA SIKU HIZI .. ... ITAKULA KWAO!!
   
 12. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  yeye kama kiongozi wa DINI hakufaa kutamka hayo maneno kwenye nyekundu
   
 13. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Hivi alichokuwa akikifanya Kakobe ndio elimu ya uraia mnayoipigia kelele...........no wonder wale wajasariamali wa NGOs huishia kuingiza mifukoni fedha za wahisani wanazopewa kufanya shughuli hiyo.

  Du, ama kweli demokrasia ni gharama.
   
 14. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wengi katika JF wamechoka kufikiri.

  Sasa aliyetoa rushwa na aliyepokea wote wana makosa. lakini umaskini mkubwa walio nao wananchi ni vigumu kupokea hiyo 4000 wanayopewa na CCM.

  Hebu fikiria, A amempa X sh 4000 (kama allowance kwa kumkatizia X kazi zake, siyo rushwa)na akampakiza kwenye roli hadi kwenye mkutano wa kampeni kisha na kumrudisha pale alipomtoa. Sasa askofu anasema amekupa sawa, umepokea, sawa lakini usimpe kura (kwa maana mgombea anayetoa rushwa, hafai kuwa kiongozi).

  Sasa hapo wa kulaumiwa ni askofu au A aliyetoa hiyo "alawansi"?? Tafakari kwa makini
   
 15. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Sitashangaa kumsikia Tendwa siku ya mwisho ya campaign akiwaagiza watanzania kumpigia kura Jk. Sasa ameanza kudhihirisha rangi zake kwamba ni kada wa chama cha mapinduzi. Hata hivyo ameishapoteza uhalali wa kuwa mlezi wa vyama vyote ila kwa sababu li-nchi letu ni la mabavu na la watu wanaolazimisha kutawala hakuna hatua zinazochukuliwa.
   
 16. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kiongozi wa dini angesema msipokee hongo au kuwataja wanatoa hongo mgesema ameanza siasa. huyo kaamua kutumia tu njia ya mkato kwani wenye kusimamia sheria ndo wanao toa hongo, kiongozi afanyeje?

  Kwani Tendwa hajui wanotoa hongo? mbona anacheka nao? Mikutano ya CCM unakutana na suala la watu kusafirishwa kwa magari, hiyo utaita ukarimu (sijui takrima).
   
 17. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #17
  Oct 4, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  KULA CCM, KURA Dk SLAA.
   
 18. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  "WATU WANAOKUBALI KUDANGANYWA, HAWANA MAONO JUU YA MAISHA YAO WENYEWE," Askofu Mokiwa, kwenye sherehe ya kumweka wakfu Askofu mpya wa Ruaha na Kumuaga Akofu Mkuu Mtetemela
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,937
  Trophy Points: 280
  Ukiacha ushabiki au fikra za kidini, alichokisema ndicho wanachopaswa kusema walio wafuasi wa demokrasia ya kweli na sio siasa za maji taka.
   
 20. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ninavyoelewa ukipokea kula ya mgombea halafu ukamnyima kura yako, hii haiwezi kudaiwa kuwa umepokea hongo kwani lengo la hongo halikutimizwa. Je, hii haiwezi kuwa kama msaada tu ? Naomba wataalamu wanijuze hapa.
   
Loading...