Kula tunda kimasihara: Jinsi Mungu alivyoniepusha

Carnivora

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
3,651
5,997
Aisee mambo vipi. Habari za weekend.

Hiki kisa kilinitokea mwaka 2016.

Ilikua safari ya Mwanza-Dar. Nyegezi nilipanda bus na dada mmoja alikuwa wa kawaida tu hakuwa na uzuri wa kutisha sema tu alijaaliwa wowowo la kutosha. Njia nzima alikua kimya hana story nami. Nami baada ya kuona yuko kimya nikapiga kimya busy na simu yangu. Jaribu kuongea na yule mrembo wapi, naona ananipotezea kiaina. Nikasema basi yaishe mi mwenyewe nna stress za safari ile maana haikuwa njema kwangu. Nilikua naenda kwenye disciplinary hearing ya kazi makao makuu ya kampuni yetu. Stress zilizidi baada ya kunyimwa tiketi ya ndege na nikaambiwa nipande bus.

Picha linaanza tumefika Ubungo mishale mibaya ya saa 7 usiku. Dada akawahi kushuka. Mi sikua na haraka, nikasubiri ile foleni ya kushuka kwenye bus ipungue nikashuka. Nikamkuta chini anachukua begi lake toka kwenye boot. Nilipokuwa nataka kumpita akaniita. "Kaka samahani naomba simu yako nimpigie rafiki yangu naenda kwake, yangu imezimika". Sikuwa na hiyana, nikampa, akapiga isipokelewe.

Tukawa tunatembea kutokea nje anajaribu kupiga bila mafanikio ya kumpata. Tukafika nje pale kwenye vibajaji....dada hana la kufanya. Ikabidi nimhoji mawili matatu. Akasema rafiki yake anafanya kazi casino....nikamhoji ni casino gani? Hajui? Punde akapiga yule rafiki akasema yuko kazini anaongea kwa kujificha na ufunguo wa geto lake kajisahau kaondoka nao...casino ni wapi? Akasema ni Mtaa wa Ohio. Dada akakata na tukipiga hapokei tena. Kwa kuwa mi naijua vizuri Dar, bichwa likaclick fasta hapo ni Princess casino, Garden Avenue/Ohio. Nikamwambia kule ni mbali usiku ule. Ana nauli ya kwenda? Dada ana buku 7 mkononi....wakati nimesimama tunajadili haya, kuna boda boda akajisogeza akitafuta abiria.

Nikaaza kuona huyu bidada ananizingua mi nataka kuondoka zangu Jet Lumo kwa mchizi wangu ambaye nilishampanga niko njiani. Home kwetu ni Boko niliona mbali sana kwenda. Unajua tena mipango....pesa ya kulala niliyopewa na ofisi nifanyie mambo mengine. Huruma inanijia, Kumuuliza bajaj mpaka town sh ngapi ampeleke akasema elfu 10. Nikawaza akifika kule anampataje mwenyeji wake naye yuko ndani ya casino? Na anarudi vipi?

Dada yuko frustrated kaniganda. Yaani nikisogeza mguu tu ananifata. Nikawaza nikalale naye? Niende naye kwa mchizi? Nikamuambia basi twende wote...dada akasema sawa. Nikikumbuka next morning nina kikao cha kesi yangu akili inakataa. Akili inaniambia asije akakutia gundu ukajibu utumbo ukafukuzwa kazi bure. Tendo la ngono linabeba bahati, mikosi, hata laana za watu unaolala nao. Imani yangu inaniambia hivyo. Nikamwita bajaji, kabla hajafika nikamwambia dada basi tutafute loji ya jirani tulale wote maana mi nnakoenda pia ni mbali kma vipi tupumzike tu wote pamoja. Dada akatii, nikaogopa, mbona haleti kipingamizi? Nikamstopisha bajaji. Hapo tumekaa inakaribia nusu saa au dk 40 nawaza nimfanyeje?

Nikampa elfu 20 na kumwambia nakuitia boda akupeleke ukalale. Akasuhukuru, akasema namba zako? Ila si zipo kwa Edna (rafiki yake) basi ntakutafuta. Nikasema sawa. Kwa kweli siku ile sikuwa na mzuka kabisa kulala naye japo ilishakuwa green light. Nikaita boda walivyofika nikamuuliza yule boda mmoja anaifahamu guest house ya bei nafuu karibu maeneo ya Riverside? Wakajibu wote ipo bro, twenzetu...mchukue huyu dada umpeleke tangulia mi nakuja nyuma na huyu mwenzio.

Safari ikaanza, tulivyofika darajani nikamwambia boda wangu simama. Nikamlipa na kumwambia we rudi. Acha yule amfikishe inatosha.

Dada yule hakuwahi kunitafuta kamwe. Sijawahi kujua hata jina lake. Na wala sikumtafuta yule rafiki yake. Leo tu nimeukumbuka uzi wa kulana kimasihara nikaona nitoe kisa hiki.
 
au labda inawezekana sura na umbo havijakuvutia

kama alikuwa si kiwango hapo sawa

ila kama ni kisu kimahesabu umekula hasara ya kukikosesha kichwa cha chini haki yake ya kimsingi
Dah mkuu...I was out of mood kabisa. Nikamuacha njiwa aruke.
 
Ile kesi ya ofisini iliendaje? Ulichomoka au wakatia kitanzi
Ile kesi iliisha kwa beef kali. Kati ya bosi wangu mkuu wa idara na bosi wa tawi la Mwanza. Baada ya kuwagaragaza wakanichukia sana.

Kuna mdau alinipenyezea kuwa siku ile ya kesi kuna mdosi mmoja mkuu wa idara nyingine alimuwakilisha MD alivutiwa sana na mimi nilivyojieleza na akasema mbona anaonekana kujiamini na hana wasiwasi sidhani kama ana kosa yule.

A few days later akaja Mwanza, alikua anaongea na Meneja msaidizi, nikakatiza akaniita. Akamwambia meneja huyu I want this guy to my dept....we want people like him. Full of confidence, determination and facts. Maana siku ya kesi nilikwenda na nondo zangu wakati wao (HR na mkuu wa idara yangu) hawakujiandaa.

Akaniambia andika email ya kuomba kuhama dept kisha nimCc bosi wangu. Simple nikahama dept....na kazi yenyewe nilikuja kuacha kwao two years later.
 
Aina ya watu kama mkurugenzi wako wa idara ndio wanafanya maisha haya yanasonga na kutupatia challenge maishani mwetu
 
Ile kesi iliisha kwa beef kali. Kati ya bosi wangu mkuu wa idara na bosi wa tawi la Mwanza. Baada ya kuwagaragaza wakanichukia sana.

Kuna mdau alinipenyezea kuwa siku ile ya kesi kuna mdosi mmoja mkuu wa idara nyingine alimuwakilisha MD alivutiwa sana na mimi nilivyojieleza na akasema mbona anaonekana kujiamini na hana wasiwasi sidhani kama ana kosa yule.

A few days later akaja Mwanza, alikua anaongea na Meneja msaidizi, nikakatiza akaniita. Akamwambia meneja huyu I want this guy to my dept....we want people like him. Full of confidence, determination and facts. Maana siku ya kesi nilikwenda na nondo zangu wakati wao (HR na mkuu wa idara yangu) hawakujiandaa.

Akaniambia andika email ya kuomba kuhama dept kisha nimCc bosi wangu. Simple nikahama dept....na kazi yenyewe nilikuja kuacha kwao two years later.
Safi sana, hizi kazi huwa zina challenge sana.
 
Basi kuipotezea ile pussy siku moja kabla ya hearing ulifanya jambo jema sana. Ila kama ungevuruga nahisi hata wewe mwenyewe ungejilaumu mnoo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom