Kukwepa kutumia miwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukwepa kutumia miwani

Discussion in 'JF Doctor' started by Simplelady, Oct 30, 2009.

 1. S

  Simplelady Member

  #1
  Oct 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani kuna dawa ya kusafisha macho yaweze kuona vizuri hasa mbali bila kutumia miwani.
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  na mimi nisaidiwe katika hilo.
   
 3. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kunywa juice ya karoti na ya mchicha wa kienyeji.
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hii inasaidia zaid katika kuzuia tatizo au nakosea?
  Macho yakishaharibika na kufikia kiwango cha kuhitaji msaada WA MIWANI huna jinsi.Ukitaka kukwepa kuvaa miwani basi unahitaji kufanyiwa laser surgery.... ila hii operation ni delicate na ni recent development haina hata miaka 15 toka ianze kufanyika na hivyo haijulikani madhara yake kwa zaid.
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ni kweli hii ni kwa prevention tu, ila ukitumia inaweza kuzuia macho kuharibika zaidi ya stage yalioko.
   
 6. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Nami pia nina tatizo hilo. Nimeshajaribu karoti na mchicha, sikuona mafanikio yoyote. Ni kama anavyosema Mkuu Vera, hii inasaidia kuzuia tatizo, sio kutibu.
  Hivi jamani nimeshamsikia Dr. Ndodi, yule wa Magomeni, akisema anaweza kutibu shida ya macho na usitumie miwani tena. Ni kweli? Wenye taarifa zaidi watupashe.
   
 7. S

  Simplelady Member

  #7
  Oct 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wenye idea ya huyo Dr. tuambizane jamani , maana sipendi kweli kuvaa miwani.
   
 8. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ee bwana mie nilikimbiakimbia kuvaa miwani weee. Mpaka ikafkia sasa ili mkono uingie kinywan nilitakiwa nivae miwani. Nachukia! Yaan nkiwa sipo kazin navua. Street miwan kapuni. But wa2 wanasema hii vaa na vua inaharibu zaidi. Ni kweli hii wakuu?
  Nashaur jiandae 2 kuvaa. Ma-operation c mazuri kwa macho.
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,160
  Trophy Points: 280
  ntapata wapi mchicha wa kienyeji?
   
 10. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  You can have lasik surgery if it is available in your area.
   
 11. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  hapo hakuna kukwepa ndugu, kama daktari amekushauri utumie miwani naomba ufuate ushauri wake, maana ukikaidi ndio ugonjwa unazidi. Hata mimi nilipoambiwa kuvaa miwani nilona kama nitashindwa kuishi, lakini sasa nimeizoea kiasi kwamba hata sitaki kuikosa, na nimechukualia kama part and parcel ya maisha yangu. part of my body. Vaa tu ndugu ndio maisha hayo kuliko kuwa kipofu kabisa hebu fikiria kuwa kipofi na kuvaa miwani utachagua nini?
   
 12. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Pengine ujaribu contact lense kama huna tatizo la kupekua jicho kuweka au kutoa hizo contact.
   
 13. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Watu wengine wanasema unatakiwa upunguze vitu vinavyokufanya utumie miwani sanaaa mfano: kusoma, kutumia computer, etc..(sasa sijui maisha yatakuwaje if that your common way of earning..maana yake uangalie kazi za outdoor ..ambazo si lazima sana kutumia miwani..huku ukiendelea kutumia vyakula vinavysaidia kuona..
   
 14. s

  shabanimzungu Senior Member

  #14
  Nov 1, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  miwani ni muhimu........mimi nikipata shida sana ya kutoona ...na nilishauriwa na wengi kwamba nisiwae miwani.
  Badaye nika enda kumwona daktari wa macho -shoppers plaza- kani shauri vizuri madhara na akanieleza LAZER haita saidia macho yangu.
  Pia nil elmishwa jinzi macho yangu ilivyo.........na sasa nin hakika kwamba macho ni muhimu...kama inatakiwa kuwaa miwani ..ni lazma hatuwezi kukwepa na pia hakuna dawa wala biti shamba!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...