Kukulupuka ama ukanjanja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukulupuka ama ukanjanja?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mfumwa, Feb 3, 2009.

 1. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu mwandishi anazungumzia kesi ya Zombe na wenzake kufanyika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu. Wakati kesi hii iko Mahakama Kuu na ilikuwa ikiendeshwa na Jaji Masati, manake kesi za mauaji hufanyika Mahakama Kuu, bali kwa kutajwa huanzia mahakama za chini. Hivi na wahariri wa habari nao hawana muda wa kupitia habari kabla ya kuchapishwa?. Soma habari:-

  Zombe na wenzake kuanza kujitetea leo
  Na James Magai

  KESI ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva teksi wa Manzese, Dar es Salaam inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Dar es Salama, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe na askari wenzake 12, inaendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

  Kesi hiyo leo inaingia katika hatua ya pili, ambayo sasa itakuwa ni zamu ya watuhumiwa hao kuanza kujitetea dhidi ya tuhuma zinazowakabili.

  Hatua hii ya pili ni muhimu na ngumu kwa washtakiwa kwa kuwa, watakuwa na kibarua cha kupangua hoja mbalimbali zilizotolewa dhidi yao na mashahidi wakati wakitoa ushahidi wao.

  Lakini pia ni ndiyo hatua itakayotoa mwelekeo halisi wa kesi hiyo, iwapo wote ama baadhi yao watatiwa hatiani.

  Pengine huu utakuwa uwanja mpana kwa Zombe, kuonyesha umahiri wake katika sheria, maana wakati wa ushahidi mara kwa mara alikuwa akiwaandikia mawakili wake ujumbe kwenye karatasi ama akiwaelekeza au kuwakumbushia maswali ya kuwauliza mashahidi au vifungu vya sheria

  Kubwa zaidi katika hatua hii ni uwezekano wa washtakiwa kusalitiana au kuwakana wenzao. Hatua hii ni hatua ambayo kila mmoja anatakiwa kujiokoa mwenyewe.

  Kutokana na hali hiyo, inaaminika kuwa huenda baadhi ya washtakiwa kusalitiana kunatokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, kutokana na baadhi ya mashahidi kuieleza mahakama kwamba, baadhi ya watuhumiwa walieleza ukweli jinsi mauaji hayo yalivyofanyika.

  Miongoni mwa mashahidi hao ni pamoja na shahidi wa 36, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Sigine Mkumbi aliyekuwa kiongozi wa timu ya Jeshi la Polisi ya upelelezi wa mauaji hayo na shahidi wa 30, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emson Mmari, aliyekuwa mjumbe katika timu hiyo.

  Mashahidi hao kwa nyakati tofauti waliieleza mahakama kuwa wakati wakifanya upelelezi juu ya tukio hilo, mshitakiwa wa 11, Rashid Lema na wa 12, Rajabu Bakari waliwaeleza wafanyabiashara hao kuwa waliawa katika Msitu wa Pande, ulioko Mbezi Luis nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

  Mmari ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa akifanya kazi makao Makuu ya Jeshi la Polisi, aliieleza mahakama kuwa washtakiwa hao waliwaeleza kuwa wafanyabiashara hao walikuwa wakishushwa mmoja mmoja kwenye gari na kulazwa chini kifudifudi na kupigwa risasi.

  Alisema wakati wa upelelezi alimhoji mshtakiwa wa 11, Koplo, Rashid Lema ambaye aliwaeleza ukweli wa jinsi na mahali maujai hayo yalikofanyika na kwamba, Machi 7 aliwapeleka eneo hilo ambapo walikuta damu ilikauka na kugandamana na udongo ambao waliupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kuthibitishwa kuwa ni ya binadamu.

  Pia Mmari alisema Koplo Lema aliwaeleza aliyefanya mauaji hayo kuwa ni Koplo Saad Alawi ambaye hadi sasa hajakamatwa na kwamba, baadaye walipotakiwa kwenda kujieleza kwenye Tume ya Rais, Zombe aliwashinikiza waseme uongo na kuwaandikia maelezo kwenye vikaratasi jinsi ya kueleza.

  Mbali na ushahidi huo wa Mmari na mashahidi wengine waliotoa uligusa watu wengi kutokana na kusisimua kiasi cha ndugu wa marehemu kutoa machozi, lakini shahidi aliyeacha gumzo ni shahidi namba 25, Shaban Said Manyanya.

  Shahidi huyo aliwashangaza wasikilizaji baada ya kudai kuwa yeye ndiye aliyestahili kuuawa kwa sababu ndiye aliyepora pesa za Bidco ambazo watuhumiwa walidai ziliporwa na wafanyabiashara waliouawa.

  Manyanya aliiambia mahakama kuwa aliumia sana aliposikia Zombe akitangaza kwenye luninga kwamba, wamewaua majambazi wanne Sinza kutokana na kupora fedha za Bidco kwa sababu hawakuwa na hatia hivyo walionewa kwani yeye na wenzake ndio waliopora pesa hizo.

  Alidai kutokana na maumivu aliyoyapata ya kuuwa watu wasio na hatia aliamua kwenda kutoa maelezo yake katika Tume ya Rais ya kuchunguza mauaji hayo iliyoongozwa na Jaji Mussa Kipenka.

  Hatua ya kwanza ya kesi hiyo ilianza kusikiliwa rasmi Mei 26, 2008 kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ilianza Mei 26 hadi Juni 12 na jumla ya mashahidi 29 walitoa ushahidi wao mahakamani hapo.

  Awamu ya pili ilianza Septemba 2 hadi Septemba 6 mwaha huo huo na mashahidi watatu tu ndio walitoa ushahidi na kufanya idadi ya mashahidi kufikia 32.

  Awamu ya tatu na ya mwisho katika kesi hiyo ilianza Septemba 22 hadi Septemba 26, upande wa mashtaka ulifunga ushahidi na jumla ya mashahidi 37, walikuwa wametoa ushahidi wao.

  Katika kesi hiyo Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Wilaya ya Mahenge mkoani Morogoro ambao ni Sabinus Sabinus Chigumbi maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe Juma Ndugu, dereva teksi aliyelkuwa akifanya kazi katika kituo cha Manzese jijini Dar es Salaam.

  Mbali na Zombe washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni SP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, F.5912 PC Noel Leonard, WP 4593 PC Jane Andrew, D6440, CP Moris Nyangelela, CPL Emmanuel Mabula, E6712 CPL Felix Cedrick, D8289 PC Michael Sonza, D 2300CPL Ebeneth Saro, D.9312D/C Rashid Lema, D4656 C/CPL Rajab Bakari na D.1367 D/CPL Festus Gwabisabi.

  Source: Mwananchi Read News
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mfumwa, heshima mbele.
  Ukiondoa kuchanganya mahakama ambalo ni kosa la kibinaadamu, mwandishi ni makini na hakuna dalili yoyote ya kukurupuka (sio kukulupuka) na wala hakuna Ukanjanja wowote.

  Wewe ndio umekurupuka kumshambulia mwandishi ambaye amefanya good analysis yake. Kumwita mwandishi wa aina hii amekurupuka au kanjanja ni dharau kwa fani uandishi wa habari na heshima ya mtu.

  Pamoja na uwezo wa waandishi wetu wengi ni duni na fani ya uandishi wa habari kuvamiwa na waandishi wasio na uwezo, wanaokurupuka na makanjanja kibao, mwandishi huyo si mmoja wa yoyote kwenye kundi hilo.
  Mwandishi anakurupuka pale tuu anapoandika habari nunu nusu huku hajui aandikacho, na kama angetulia na kufuatilia kwa makini, angeandika habari hiyo vizuri.
  Kanjanja ni mwandishi ambaye hana mahali popote pa kupeleka habari ama mtu anayejifanya mwandishi kuhudhuria matukio ili akunje mshiko huku kiukweli hana lolote aandikalo.

  Baada ya uteuzi wa Philemon Luhanjo, kama Katibu Mkuu Kiongozi, mwandishi mmoja mwandamizi tena mkongwe aliandika habari na picha ya Luhanjo, huku akiandika, Katibu Mkuu Kiongozi, Marten Lumbanga. Habari hiyo ikapita kwa Sub Editor, ikapita kwa Editor na ikatoka hivyo hivyo front page ya chombo cha habari chenye heshima kubwa nchini na nje ya nchi. Je utasema huyu mwandishi alikurupuka au ni kanjanja?.
  'We are only Human, born to make mistakes no mater how silly they are'.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Wenzetu huandika masahihisho siku ya pili kama wakikosea herufi ya kwanza ya jina la kati la mtu (middle initial) , kama unaitwa Daudi S Mushi, wakikuandika Daudi E Mushi kesho wataomba radhi na kusahihisha.Lakini kwanza mpaka mtu awaandikie na kuwasahihisha.

  Halafu hapa tukianza kuwasahihisha wengine wanasema ni kosa la kibinadamu? Gazeti kama sehemu ya kupata rekodi linaweza kuchuza watu kibao kwenda mahakama ya Kisutu ilhali mambo yote yapo Mahakama Kuu.

  Moja ya mambo yanayotukosesha maendeleo ni kutotaka kuwa na viwango vya juu, kuanzia kwenye uongozi wetu, elimu yetu mpaka waandishi wetu.Tunakubali kubali vitu vyenye viwango vya chini kirahisi rahisi.
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Please mheshimiwa Pasco, magazeti yetu yana makosa kibao.Makosa ambayao yanatilia mashaka fani nzima ya uandishi wa habari.Habari nyingi hazina editing na si mara moja nimewapigia simu ma-editor kuwa onyesha makosa ambayo ni dhahiri.
  Pitia makala ya Profesa Kironde kwenye gazeti moja maarufu nchini na utaona makosa hayo KILA WIKI.
  Kicheko ni pale waandishi wakiona kifaa cha kutengeneza barabara, kwenye picha watakiita "katapila". Msemo ambao ni wa waswahili wasiojua kifaa kinaitwaje.
  Si uongo kuwa reporting na substance yake katika habari hiyo,ndani ya magazeti yetu ni ya chini mno.Linganisha na magazeti ya jirani zetu kama "East African",
  habari ile ile lakini imeandikwa kwa ufundi na umakini mkubwa.
  Usiwatetee mkuu Pasco.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  Siwatetei waandishi wetu ndio maana nimesema
  1.Uandishi wetu wa habari ni duni.
  2.Baadhi ya waandishi wetu wengi hawana uwezo
  3.Fani ya uandishi habari na utangazaji zimevamiwa
  4.kuna idadi kubwa ya makanjanja kwenye game.

  Nikasisitiza, pamoja na yote hayo mwandishi aliyeandika story ile hajakurupuka bali amefanya analysis yake. Nikamfafanulia maana ya kukurupuka katika fani ya uandishi wa habari
  Pia nikamfafanulia kanjanja ni nani. Kitendo cha kuripoti story na ikatokaa popote, hata kama hujaajiriwa sio ukanjanja.

  Pamoja na madhaifu yote ya fani ya uandishi wa habari Tanzania, naomba tuwaonee huruma waandishi wetu, wanafanya kazi katika mazingira magumu sana. Waandishi wengi wakike hujikuta wanalazimika 'kuachia'
  Wakati hawa wa kiume ni 'bahasha' mbele.

  Kenya na Uganda shahada ya Journalism ilianza miaka mingi zaidi ya 20. UDSM imetoa wahitimu wa kwanza mwaka juzi. Angalau Tumaini na Sauti walitangulia kidogo lakini mpaka sasa ninapoandika, hatuna masters labda vipost graduate diploma.

  Wenzetu waandishi wanaspcialize. Mwandishi wa Afya ni daktari. Mwandishi wa sheria ni mwanasheria. Wakina Prof. Mwakyembe, Prof. Palamagamba Kabudi na Dr. Sengodo Mvungi, wote walikuwa waandishi wakasoma sheria na walipohitimu, wakaukimbie waandishi wasije lala njaa. Hiyo specialization itoke wapi.

  Kwa msio ujua uandishi waandishi ni 'mchumia juani mazao yaliyonyauka na kulia juani' wakati fani nyingine mchumia juani hulia kivulini.
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana nawewe mkuu ,kwenye makala nyingine subject matter ni hafifu sana katika waandishi wasiona ujuzi katika fani wanayoiandikia.
  Mwakyembe ,Kabudi na Mvungi nawafahamu siku nyingi na si tu wanajua uandishi lakini vile vile walipitia fasihi za lugha na kuzielewa vizuri na ndio maana wanaweza kukuweka ujumbe kwa mbwembwe za kuijua si lugha tu lakini katika uandishi bora.
  Tunaomba waandishi wetu wajaribu kujiboresha katika hili.
   
Loading...