La shaka ALLAH ni Mwingi wa msamaha,
PIA JUA MAANA YA KUFURU NA SHIRKI KISHA UJE UPINGE KWA HOJA NA DALILI
Lakin nasaha zangu kwako, ISOME DINI YAKO.
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Na wenye kukufuru na kuzikanusha ishara zetu, hao ndio watakao kuwa watu wa Motoni, humo watadumu.
Al Baqara 39
Nyingine hii
👇👇👇👇
قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ سَتُغۡلَبُونَ وَتُحۡشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ
Waambie walio kufuru: Karibuni mtashindwa na mtakusanywa, mtiwe kwenye Jahannam; nako huko ni makao mabaya kabisa.
Al Imran, aya 12.
Nyingine
👇👇👇👇
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ
Na wale walio kufuru na wakakanusha Ishara zetu, hao ndio watu wa Motoni.
Al-Ma'idah 10.
Ziada
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمۡ شَرُّ ٱلۡبَرِيَّةِ
Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.
Al-Bayyinah, Ayah 6
Sasa ndg yangu je baada ya hizi dalili je waweza kutupa faida nasisi juu ya dalili ya ALLAH kuwasamehe MAKAFIRI NA WASHIRIKINA?
Baarakallah feeyka
Mkuu mimi ninakubaliana kabisa na hizo aya za Qur'an, ila mimi sikubaliani na maneno yako yanayopinga baadhi ya aya za Qur'an pale uliposema:-
"Allah hasamehi yoyote atakayekufuru ila tu kama atafikwa na mauti akiwa katika ukafiri"
Neno "YOYOTE" uliloandika ndilo linaloleta mushkeli, kwani ukisoma katika 18:58, inasema:- "Na Mola wako ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa huruma, kama angaliwashika kwa yale waliyochuma basi angaliharakisha adhabu kwao, lakini wanao muda maalumu ambamo hawatakimbia."
Hapo katika hiyo aya Mungu anajaribu kwanza kuonyesha msamaha na huruma yake kwa wakosefu kabla ya kuwaadhibu, na kuna aya kadhaa zinataja kwamba Allah ni mwingi wa huruma 6:147, 18:58 nk.
Kwakuwa kusamehe na huruma ni sifa za Allah basi wapo makafiri atakaowasamehe na wapo atakao waadhibu kwa sababu kuadhibu ni moja ya sifa yake pia na ndiyo maana napinga matumizi ya neno kafiri "YOYOTE".
Ukisoma katika 5:118, Nabii Isa (as) anasema/atasema siku ya kiyama juu ya watu wake waliokufuru kwamba:- "In tua'dhibtum fainnahum i'baaduka wa in faghfirlahum fainnaka anta al aziizul hakiim"
Yaani; kama utawaadhibu wao ni watumishi wako na kama utawasamehe Wewe ni mwenye nguvu mwenye hekima"
Ukiangalia tafsiri yako ya ukafiri uliyoitoa mwanzoni mwa uzi wako (ambayo ninaikubali), hapo hao wafuasi wa Nabii Isa (as) nao ni makafiri na Nabii Isa (as) anataja sifa ya kusamehe ya Allah ili kama akipenda aitekeleze juu ya wafuasi wake siku ya kiyama, hivyo pia katika siku ya hukumu (kiama) Allah atawasamehe baadhi ya makafiri atakapopenda na siyo kafiri YOYOTE ataadhibiwa, kwahiyo nafasi ya watu (makafiri) kusamehewa na ALLAH ipo.