Kuku wa kisasa wanakuzwa kwa ARVs | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuku wa kisasa wanakuzwa kwa ARVs

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Judith Francis, Mar 17, 2010.

 1. J

  Judith Francis Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna rafiki yangu amenitumia email hii ambayo imenishtua kiasi fulani. Wanajamii forum hebu tuichunguze na kuijadili kuona kama ina ukweli wowote.

  "Habari ndio hiyo, uamuzi ni wako

  Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa kitabibu, baadhi ya kuku wa kufugwa
  wanaoingia sokoni wamekuzwa kwa kutumia ‘utundu’ wenye hatari wa baadhi ya
  wafugaji wasio waaminifu kwa kulisha mifugo hiyo dawa za ARV ambazo
  huwafanya kuku hao kuonekana wakubwa na wanene kwa muda mfupi.

  Uchunguzi huo unakwenda mbele zaidi na kubainisha kwamba, tabia za dawa
  hizo ambazo ni kujenga mwili na kuimarisha kinga ya magonjwa kwa
  mwathirika wa Virusi vya Ukimwi, ndiyo inayompata mlaji wa kuku hao.

  Inadaiwa kuwa, kuku hao wanapokula chakula kilichochanganywa na dawa hizo,
  huweza kutumia siku kumi na mbili hadi kumi na nne kutoka kuwa vifaranga
  hadi utayari wa kuingizwa kwenye soko la walaji.

  Ili kukamilisha uchunguzi huo, Amani lilituma makachero wake maeneo ya
  Kibamba, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo ndipo kwenye viwanda vya
  kuzalisha kuku wa ‘sampuli’ hiyo.

  Kwa mujibu wa kijana mmoja ‘profesheno’ wa kutunza kuku katika moja ya
  nyumba maarufu kwa uzalishaji maeneo hayo, ambaye hakutaka jina lake
  lichorwe kwenye ‘pepa’ hii, alikiri kuwepo kwa ishu hiyo, lakini
  alibainisha kuwa hajui bosi wake anapochukulia vidonge hivyo vya ARV’S.

  MADHARA:
  Kwa mujibu wa Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbi ambaye aliomba
  hifadhi ya jina lake, mtu anayependa kula kuku waliokuzwa kwa kutumia ARV
  na yeye huanza kunenepa kupita kawaida, lakini uzito unaweza kuwa tofauti
  na unene ‘boya’.

  Mtabibu huyo aliongeza kuwa, watoto wengi wanaozaliwa siku hizo ambao
  wazazi wao wamekuwa watumiaji wazuri wa kuku, hukua haraka kiasi kwamba,
  mtoto wa miaka 18 huonekana kama ana miaka 27.

  Aidha, alidai kuwa, wengi ambao kuku hao wamekuwa chakula chao kikuu,
  hufika mahali wanakuwa ‘legelege’ katika utendaji wa kazi wa kila siku
  tofauti na zamani huku sehemu kubwa ya chakula hicho ikiangamiza ‘pati’ ya
  subira na uvumilivu na mlaji kuwa na hasira.

  Dalili nyingine ni mtu kuhisi muda wake wa kuchoka unakuwa mfupi
  akilinganisha na zamani na wakati mwingine hali ya kuhisi kusinzia
  humtawala hata kama anafanya kazi"


  Department of Agricultural Engineering,
  P.O. Box 3003,
  Morogoro
  TANZANIA
   
 2. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mimi sikuiami the first day nilipoiona.  Hii kali siku 12 unakula kuku?
   
 3. senator

  senator JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ilikwisha kujadiliwa kwa kirefu hii mada
   
 4. M

  Mchili JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii niliisikia huko mbeya
   
 5. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  dada Judy naona umejilipua mzima mzima na jina lako! teh teh teh eh!

   
 6. m

  matambo JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hii ni mbaya,kwani waweza jiweka katika risk ya kuleta resistance ya arvs
   
Loading...