kuku kuzunguka na kukimbia kimbia hovyo na kukosa balance

TUPAMBANE

Member
Jan 25, 2021
62
88
Habari wadau wa ufugaji,

Nina kuku wangu ninayempenda sana amepatwa na kaugionjwa bado sijakaelewa. Ugonjwa wenyewe ni kukimbia kimbia na kuzungua na kukosa balance na kuanguka akisimama.

Hapo ni kukimbia tena yaani kuna saa unaibuka na kuna saa anakuwa kama anataka kuwa sawa ila tatizo hawi stable kabisa yaa namwonea huruma asubuhi namlisha kama mtoto mdogo nikirudi kazini nimlishe tena kama mtoto mdogo.

Ukimwekea chakula kwenye chombo au chini kama maindi kumi mfano ili aokote indi moja inamchukua dakika zaidi ya 3 maana anakosa timing kabisa mpaka anakula udongo yaani anashindwa kuokota punje ya muindi.

Hivyo nimeamua tuu asubuhi nimpe chakula na maji na jioni tena nimpe tena sasa naulizia mtu mwenye kujua aina ya dawa anitajie jina maana humu jamii forum kuna wataalam wa kila aina nitakushukuru sana wewe ambaye utakuwa sambamba na mimi kumwokoa huyu kiumbe weka mbali ushauri wa kuchinja
 
sorry kichwa cha habari Ni kuku kuzubaa na kuzunguka zunguka na kukimbia hovyo nimeshindwa ku edit
 
Pole ufugaji una tashwishwi sana ila Wanashauri msimu kama huu u natakiwa uwape chanjo ya kideri kama hawana dalili ila kama wamesha kuwa affected tafuta antibiotic ya kideri uwape kwa maji kwa 5 days then Ndio uwape chanjo...
_______________________
Nenda duka la dawa za mifugo kwa ushauri zaidi.
 
Mkuuu Tupambane pole na changamoto za Ufugaji. Kama bado hujasaidika tusaidie taarifa zaidi za hyo kuku.

Vp kuhusu Umri wake? Ni aina gani ya kuku: wakienyeji au wa kisasa? Na amepatiwa chanjo zipi mpaka sasa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom