Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 989
Kwa miaka kadhaa tumekuwa tukiona wanandoa wanakosana na hatimaye wanatengana, yaani ndoa inavunjika. Kwa sababu ni mazoea ya enzi na enzi, hakuna anayeshangaa kuona watu wliopendana wanafikia hatua ya kutengana na hawatakai hata kuonana kw amaisha yao yote.
Hata kutengana urafiki si jambo geni. Na hata ndugu kukogombana na mkachukiana hata kutozikana, nako si jambo geni kwa waliokwisha kuona hilo.
Lakini kuna jambo ambalo nimeliona nalo sasa si jipya lakini tunalifumbia macho wakati linaangamiza karibu kila kona. Nalo ni la kuvunjika uhusiano kati ya mzazi na mtoto.
Wote tunaelewa kwamba mtoto hulelewa na baba na mama hadi utu uzima yaani miaka 18. Kwa Tanzania huwa tunaenda hadi hata miaka 25 unakuta mtu bado yuko kwa wazazi wake na ndipo huanza kujitegemea.
Ukishajitegemea basi mzazi anakuwa mwananchi wa kawaida kama mwingine.
Sasa taabu imekuwa kwamba wazazi wengi hujikuta wanapitiliza na kutaka kum-ctrol kijana ambaye tayari anajitegemea. VIjana wengi wa kike na kiume hujikuta wanaathirika kwa kuogopa kugombana maana hawataeleweka kwenye jamii. Tena kuna kauli tele zenye kuonya zikisema "mzazi ni mzazi". Hivyo, kijana anaathirika na hata maendeleo anazidiwa kwa sabau mzazi aliendelea kum-control.
Lakini wapo vijna ambao wametokea kuwa majasiri na kukabili waziwazi wao. Wamefanya hivyo kwa kuwaambia "mama, ninajitegemea na mimi nimeanzisha mji wangu kama wewe ulivyoanzisha mji wako, tuheshimiane kwa mambo yangu, heshimu mipaka yako na mimi yangu"
Binafsi nimeshuhudia wazazi wengi wakiwa wabishi wakiambiwa hivi au kuzuiwa na watoto wao, tena watoto wakiwa na haki kabisa.
Wazazi wa aina ile huamua sasa kutangaza ugomvi na watoto wakitegemea jamii itawaunga mkono na magomvi kama asilimia 90, wazazi hupata uungwaji mkono. Hadi jamii itambue kwamba mzazi ndiye alikuwa mkorofi inaweza kuchukua hata miaka 15 baadaye wakati huo kijana alishachukiwa na asilimia kubwa ya ndugu na hata marafiki na ikibidi kuachana nao.
NImeshuhudia vijana wachache wakiliweza sekeseke la namna hiyo, mmoja aliamua kumtupilia mbalia mama yake mzazi kwa muda wa miaka 20. Miaka mitano ya mwanzoni ndugu na marafiki zake hawakumwelewa wakaungana na mama. Hata mimi miaka kumi ya mwanzoni nilimtetea mama yake.
Baadaye nilipotafiti na kuupata ukweli kwamba mama yake mzazi ndiye alikuwa mkorofi iliniuma na sikumsamehe kamwe yule mama maana alisababisha nikamchukia rafiki yangu bure na jamii nzima tukamchukia bila kosa.
Kwa hakika yule kijana hakutaka hata kuhudhuria ugonjwa au mazishi ya yule mama yake. Kwa kweli mimi ni shuhuda wa jinsi mama yule alivyosaidia kumchafua mwanaye kwenye jamii ya ndugu na marafiki.
nImeandika kwa kirefu ili kusaidia kuondoa tatizo ambalo limeshaanza kuenea lakini linafumbiwa macho na linaangamiza. Kuficha tatizo kulitufanya tukapoteza wengi kwa kicho cha ukimwi mwanzoni.
Ugomvi kati ya mzazi na mtoto ni aina mpya ua ukimwi ambao hausemwi. NIlichoona ni kwamba kadiri tunavyonyamaza ndivyo tatizo la baba au mama kugombana na mtoto linaongezeka na hadi kutupana milele linazidi.
Naamini sehemu uliyoko siajabu lipo na ikibidi hata wewe ni mmoja wa wanaopatwa na tatizo hilo kama kijana au mzazi.
Solution ninayoiona ni kwamba tusimame katika ukweli. Jamii ikiona mama au baba ameombana na mwanae, usikimbilie kuhukumu kwamba "mama ni mama". Kama mama yule kakosea basi ni bora uokoe huo ugomvi kwa kumshinikiza huyo mama au baba aende kumwomba radhi au sahamani yule mtoto aliyemkosea.
Kuliko taabu niliyoiona kwa baadhi kwamba "mama hawezi kumwomba msahama mtoto" na matokeo yake huyo mama anaishia kupigwa marufuku na mtoto wake kwamba asikanyage kwake milele.
Watu wanafanya hivi, tena wanafanya kimya kimya kuwakomesha waziazi wakorofi wakijua ukiogombana nay ehadharani jamii itakusumbua.
Wito wangu mwingine ni kwamba kumetungw avitabu tele vya magomvi ya ndoa. Sasa hamisheni nguvu yenu muanze kuandika vitabu kuhusu magomvi ya mtoto anayejitegemea na mzazi.
Vinginevyo itakula kwa wazizi wakorofi maana taratibu watu wameanza kufikia kuona "potelea mbali ngoja nimtupilie mbali huyu mzazi mkorofi" kuliko kumuendekeza wakati amegeuka kuwa binadamu wa kwanza kunidumaza maendeleo yangu.