Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

kiredio Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2024
634
1,202
Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Nimegundua mzazi wangu hana imani naye tena na sijui ni kwanini, nitamuuliza anipe sababu za kubadili mawazo yake ya awali.

Naombeni ushauri wenu juu ya hili bila kejeli na maneno mabaya
Asanteni.....
 
Samahani ila ndio ukweli halisi.

Wewe ni mama boy una mtoto unatarajia kuoa na kuwa na familia ila bado upo attached/umejishikiza kwa mama yako mzazi sababu amekuzaa.

Umefanya ujinga na umeruhusu mama yako amchoke mzazi mwenzako. Sikiliza ndugu, mama yako anampimia binti wa watu kwa kipimo ambacho sicho!!

By the way, huo ni utamu wako na amekuzawadia mtoto huhitaji kupata validation kutoka kwa mama yako.

Funga ndoa, oa na chukua mke wako na mtoto wako mkaishi kivyenu achana na mama yako ni chakula cha baba yako tu asivuke mipaka.

Sorry kama nimetumia lugha Kali mimi ni mubaba wa kunyoosha.
 
Umefanya ujinga na umeruhusu mama yako amchoke mzazi mwenzako. Sikiliza ndugu mama yako anampimia binti wa watu kwa kipimo ambacho sicho!!

By the way, huo ni utamu wako na amekuzawadia mtoto huhitaji kupata validation kutoka kwa mama yako.

Funga ndoa, oa na chukua mke wako na mtoto wako mkaishi kivyenu achana na mama yako ni chakula cha baba yako tu asivuke mipaka.

Sorry kama nimetumia lugha Kali mimi ni mubaba wa kunyoosha.
Bora umemwambia, yes he is mamas boy, maamuzi anafanyiwa na mama wakati familia anajenga ni yake
 
Samahani ila ndio ukweli halisi.

Wewe ni mama boy una mtoto unatarajia kuoa na kuwa na familia ila bado upo attached/umejishikiza kwa mama yako mzazi sababu amekuzaa.

Umefanya ujinga na umeruhusu mama yako amchoke mzazi mwenzako. Sikiliza ndugu, mama yako anampimia binti wa watu kwa kipimo ambacho sicho!!

By the way, huo ni utamu wako na amekuzawadia mtoto huhitaji kupata validation kutoka kwa mama yako.

Funga ndoa, oa na chukua mke wako na mtoto wako mkaishi kivyenu achana na mama yako ni chakula cha baba yako tu asivuke mipaka.

Sorry kama nimetumia lugha Kali mimi ni mubaba wa kunyoosha.
Dont make mistake ya kumtupa mwanamke huyo kisa mama hajampenda. Unaenda kuishi nae wewe si wazazi wako. Wouka kufanyiwa maamuzi na wazazi
 
Mara nyingi nimekuwa nikisikiliza maamuzi ya Mama Hadi katika personal issues lakini mambo yakija kwenda ndivyo sivyo mama anajitoa utadhani siyo yeye aliyekuwa ananishauri.Hii kitu ilinifunza kujitegemea mwenyewe katika maamuzi yangu nayoyaona yanafaa.Kuliko kuishia Kuambiwa Pole na Mama na kujitetea sikujua.
 
Mama amekataa ndoa, atakuwa amesoma nyuzi za humu
1000011282.jpg
 
Attachments

  • 1000011282.jpg
    1000011282.jpg
    83.1 KB · Views: 3
Mara nyingi nimekuwa nikisikiliza maamuzi ya Mama Hadi katika personal issues lakini mambo yakija kwenda ndivyo sivyo mama anajitoa utadhani siyo yeye aliyekuwa ananishauri.Hii kitu ilinifunza kujitegemea mwenyewe katika maamuzi yangu nayoyaona yanafaa.Kuliko kuishia Kuambiwa Pole na Mama na kujitetea sikujua.
Ni kweli sio kila kitu lazima mzazi ashauri, lakini jambo kama hili ni muhimu kumpa nafasi ya kushauri, pia Mama yangu ni mtu wa hekima sana, namuamini katika maamuzi yake
 
Mimi sipo tayari kumkwaza Mama yangu, japo mimi ndyo nina maamuzi ya mwisho lakini ni lazima nisikilize ushauri wake
Hujakomaa kuweza kuyabeba majukumu ya kindoa. Ndoa sio lile tendo la ndoa peke yake, ndoa ni majukumu thabiti ya kifamilia yanayohitaji maamuzi sahihi hasa kutoka kwa mwanaume.

Sio jambo la kuogopesha lakini ni zaidi ya kurusha dege kuuuuubwa la kivita NDOA.

Unaoa mke kwaajili yako wewe na wala si kwaajili ya mama yako. Man up brother
 
Naelewa majukumu yote ni yangu katika kufanya maamuzi, lakini still bado nahitaji kujifunza na kupata ushauri kuhusu mambo haya kwani mimi bado ni kijana ambaye sina experience na mambo ya Ndoa
 
Mimi sipo tayari kumkwaza Mama yangu, japo mimi ndyo nina maamuzi ya mwisho lakini ni lazima nisikilize ushauri wake
Mama boy kipeuo cha pili wewe!
Kwa hiyo mama yako unamruhusu amkwaze binti wa watu sababu hajamzaa?
Kwa hiyo akikushauri umuache binti wa watu na umemzalisha utakubali?
Mbona alishindwa kukushauri usivae kondomu au umwage nje?

Familia uliyoianzisha mwenyewe ni muhimu kuliko familia uliyotoka.
 
Back
Top Bottom