Kukosa mtaji wa elfu hamsini kushuka chini ni uzembe

Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
3,052
4,101
Changamoto ya mtaji ni tatizo kubwa kutokana asilimia kubwa ya vijana hatukopesheki hivyo wengi wetu inatulazimu kutafuta mitaji yetu wenyewe, lakini tatizo kubwa ninaloliona kwa baadhi ya vijana kushindwa kupata mtaji wa elfu kumi hadi elfu hamsini jambo ambalo kwangu naona ni uvivu mtu tu kuamua kusema sina mtaji sijui anataka aanzie mtaji wa million ndo aseme mtaji.

Unakuta kijana hana familia anakula kwa mama chakula bure yupo tu mtaani lakini anakwambia sina mtaji.

Vijana kama hawa ndio wanaotusumbua mitaani na mizinga ya buku vocha hakosi kila siku kucheki udaku insta.

Katika mazingira hayo hayo unakuta kuna kijana kwa mtaji wa elf 20 anatembeza mitumba na anapata akiba ya kuongeza Mataji na ndio ilivyo kwa wengi wameanzia chini na sasa wanamitaji mikubwa mfano Mimi.

Cha mwisho cha kusema tuilaumu serikali iliyopo madarakani ila sio sababu ya kukosa mtaji.
 
Dhamira ndo haipo, pesa ya kununua mnyonyo (jeans za kubana) ipo pesa ya mtaji elf 30 ukose...
Japo kweli kuna watu hata jero tu kushika ni mtihani
 
Halaf mtu huyo hyo ana miliki simu ya laki 3-7 bado anakuja kulia lia mtaji huku
 
Dhamira ndo haipo, pesa ya kununua mnyonyo (jeans za kubana) ipo pesa ya mtaji elf 30 ukose...
Japo kweli kuna watu hata jero tu kushika ni mtihani
Na smartphone hasa hizi iPhone sijui, na kuna vitu vinaitwa Brand
 
Mi 50,000 ninayo weka njia ya kuanzia mkuu sio unalaumu na hutoi maujanja.
 
Mkuu;
Fafanua japo kidogo. Elfu 50 ni mtaji au mlo wa siku?? Upo mjini au kijiji?? Mjini upo kwa mama au umetoka mkoani kuja darisalama ya bashite?? Usiudhi watu kuwaita wazembe bila kuwaonesha ulipo huo uzembe wao. Nikuulize tu; we ni me au ke??
 
Aseme tu, chini ya efu hamsini na hata hiyo hamsini elfu ni biashara gani mtu utafanya na kwa mazingira gani? Sipendagi porojo aisee
 
sababu Kama hizo sio kitu kwa mtu mwenye ndoto za kutaka kutaka mafanikio na watu Kama nyinyi hata mpewe Mawazo ya mtaji mdogo huwa mnapotezea tu bila kufanyia kazi wengi mnapenda kuanzia juu mtaji namatumizi yenu huw makubwa
 
Back
Top Bottom