Kukopeshana ni mwanzo wa Uadui

Kukopeshana ni mwanzo wa Uadui

mimi kumkopesha hata ndugu huwa sitaki kabisa,bora aniombe nimpe kama ninayo nitampa tu ila sio kwa gia ya deni,kuna mtu alikuwa mshikaji wangu kabisa, alipata dharura akaniomba nimuazime kama laki 8 hivi akasema atanilipa baada ya miezi mitatu, aroo leo ni mwaka wa 3 jamaa kajikausha tu.
 
Aisee kukopeshana me hapana. Same things kimetokea kwangu dah. Yaani mtu alikua na shida sana akaomba 200,000/= dah nikajitoa nikampa aisee tokea July 2019 Hadi 2020 kanilipa 50,000 tu viteteo kibao. Sema basi tu life goes on.
Mimi tangu November 2016 nilimpatia 850,000/= Uncle kwa mpango kuwa mwisho wa mwezi atanirudishia lakini hadi Leo hii 2020 hajanipa hata senti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa ya Deni kulipa,sema ndio hivo mtu akija kukopa anakuwa mpole hatari, aaha!! Wakati wa kulipa Sasa maneno mengi badala ya kulipa Deni la watu
 
Ukitaka kuwa huru, Mkopesha pesa kidogo yule anayekuomba mkopo halafu asipokulipa usimdai, hatathubutu kukukopa nyingine.

Hii inasaidia sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom