Kukopa harusi kulipa matanga


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,870
Likes
8,691
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,870 8,691 280
Mwanaume mmoja wa nchini China ambaye alikuwa akisumbuliwa na madeni mengi sana yaliyotokana na tabia yake ya kupenda kucheza kamari amejiua mwenyewe kwa kujilipua kwa bomu ndani ya basi lililokuwa limejaa abiria.
Kwa mujibu wa shirika la habari la China, Xinhua mwanaume huyo alijilipua mwenyewe ili kuepukana na madeni mengi anayodaiwa ambayo alikuwa hana uwezo wa kuyalipa.

Yang Yongshou, 42, ambaye zamani alikuwa muuza madawa ya kulevya kabla ya kuangukia kwenye uchezaji wa kamari, alijilipua kwa bomu aliloliweka chini ya kiti chake kwenye basi la abiria lililokuwa likifanya safari zake katika jimbo la Yunnan lililopo karibu na mpaka wa Vietnam.

"Yang alikuwa hana uwezo wa kulipa yuan 100,000 (Tsh. Milioni 19.8) ambazo alikuwa akidaiwa kwenye kamari", ilisema taarifa ya polisi.

Yang alifariki hapo hapo kutokana na bomu hilo huku abiria wengine 11 wa basi hilo wakipata majeraha mbalimbali.

Tabia ya watu kujilipua kwa mabomu wanapozidiwa na matatizo imekuwa ikiongezeka kwa kasi sana nchini China ambapo sababu kubwa inasemwa kuwa ni uhaba wa kazi na kuongezeka kwa tofauti ya kipato kati ya watu masikini na matajiri.
 
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Messages
408
Likes
4
Points
35
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2009
408 4 35
huyu akili hana, bongo watu wanadaiwa zaidi ya milini 19 na utawaona RG wakishusha bia bila presha
 
J

Jafar

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2006
Messages
1,138
Likes
13
Points
0
J

Jafar

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2006
1,138 13 0
Bongo kuna usemi kuwa "mdaiwa hafungwi" - sasa huyu ni kwa nini alijimaliza, angehamia Bongo kazi kwisha, angepeta na shamba kubwa, kitalu cha kuwinda na ubunge pia angepata.
 
Kisusi Mohammed

Kisusi Mohammed

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Messages
460
Likes
125
Points
60
Kisusi Mohammed

Kisusi Mohammed

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2009
460 125 60
Huyo muoga tu wa maisha, dawa ya deni ni kuwapa sound wadai!
 

Forum statistics

Threads 1,237,272
Members 475,501
Posts 29,283,197