Kukojoa damu

nyamva

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
235
144
Habarini zenu wataalam,Nisikuchosheni nakuja kwenu nikiwa na tatizo la kukojoa damu yaani kifupi niligundua tatizo hili nilipokuwa chooni, Choo kilikuwa cha shida Sana kulingana na nguo niliyokuwa nimevaa haikunipa uhuru WA kupata Choo kwa urahisi (ilibana mapaja),
Mimi ni ME mwenye miaka 38,baada ya kujikamua Sana nilipata Choo Ila baada ya hapo mkojo ulitoka baadaye ikafuata damu!!,
Nilijipa Moyo kuwa huenda nimeubana Sana uume hivyo kupasua mishipa YA damu.
Maisha yaliendelea nikiwa napata mkojo BILA damu Ila kukawa na vimaumivu flani baada ya kukojoa.

SHIDA IMEKUJA nikishiriki tendo la ndoa nikifikia mshindo shahawa inatoka Ila baada ya dakika chache damu inatoka,Jambo hili linanivuruga sio Siri.Hali hii imetokea mara tano hivi

Humu naamini kuna mkusanyiko WA wataalam ambao nina IMANI watanipa A BC za kuanzia nawakaribisha Kwa ushauri N.B Sijawahi kutumia dawa yoyote.

NAOMBA KUWASILISHA
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
19,839
55,257
Huko uliko hakuna hospitali kubwa? Wahi ukapate vipimo na matibabu sahihi.
 

Mbomozo

JF-Expert Member
Dec 23, 2019
361
915
Yawezekana ni Gonorrhea GONO kwaio nenda kapigwe sindano ya shimoni ukimaliza ivyo akili itaingia kuwa ni muhimu kutumia kinga
 

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
21,283
61,003
Najua sio vibaya kuomba ushauri hapa JF lakini kwanini mtu ukae na hali hiyo mda wote huo zaidi ya mara tano unaona hali hiyo ila hauendi kutafuta matibabu hospitali?
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom