Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Hivi karibuni kuna watu wameuwawa kinyama msikitini mkoani Mwanza na juzi dada wa marehemu bilionea Msuya kauwawa kinyama huko Dar-es-salaam. Kama haitoshi,siku chache zilizopita watu saba wa familia moja nao waliuwawa kinyama huko Mwanza. Hii ni mifano michache tu ya mauji ya kikatili miongoni mwa matukio mengi ya aina hii bila kusahau mauji ya ndugu zetu Albino.
kwa mtazamo wangu,watu hawana hofu ya kuua kwasababu hakuna anaenyongwa licha ya wengi kuhukumiwa adhabu ya kifo na hii ni kutokana na kusubiri idhini ya Raisi kabla ya kutekeleza hukumu ya kunyonga na hili ndio kosa kubwa.
Ukweli ni kwamba,Raisi kama binadamu,anaona tabu kusaini mtu anyongwe hasa kwa kuzingatia imani zetu za kidini.Hivyo basi,ili kuondoa tatizo hili,katiba/sheria ibadilishwe kuruhusu mtu anaepatikana na hatia ya kuua anyongwe mpaka kufa bila kusubiri idhini ya Raisi na sheria itamke bayana kuwa muuaji anyongwe ndani ya siku kadhaa tangu hukumu kutolewa vinginevyo unyama huu hauwezi kupungua na huenda ukazidi.
Nafahamu kuwa utekelezaji wa adhabu ya kifo hautamaliza kabisa tatizo hili ila naamini utapunguza tatizo hili kwa kiasi fulani na utafanya watu wawe waogo na ingefaa zaidi kama hukumu hizi zingetekelezwa hadharani hata kwa kutumia firing squad kama wanavyofanya Iran na kwingineko.
Nafahamu tutapata upinzani kutoka kwa watu wa haki za binadamu lakini katika hili tusiwape nafasi kabisa.
Hembu soma habari hii hapa chini kama ilivyoandikwa na gazeti la Mwananchi la siku ya leo:
Siku moja baada ya kifo cha dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth imebainika kuwa msaidizi wa ndani aliondoka saa sita mchana kwa kuacha funguo nyumba ya jirani.
Akizungumza nyumbani kwa dada wa marehemu, Mbezi Juu, mama mdogo wa marehemu Lilian Benjamin alisema msaidizi huyo alimpigia simu bosi wake mchana na kumwambia anaondoka na hataendelea na kazi.
Alisema marehemu alilazimika kuomba ruhusa mapema kazini ili arudi nyumbani kwake Kibada lakini ilimlazimu kukaa nje ya nyumba kwa saa mbili baada ya kufika saa tisa alasiri na kukuta mlango umefungwa.
Mama huyo alisema baada ya kusubiri kwa muda aliwauliza majirani wakamweleza kuwa walipelekewa funguo na mwanafunzi wasiyemfahamu akadai kuwa alipewa na dada mmoja aliyemuelekeza aipeleke nyumba hiyo. Haifahamiki mpaka sasa mahali alipo mfanyakazi huyo anayedaiwa kuwa mwenyeji wa Arusha.
Dada mkubwa wa marehemu, Happy Msuya alisema marehemu aliwaeleza mambo hayo baada ya kupigiwa simu na msichana huyo wa kazi.
Dada mwingine wa marehemu ambaye ni wa nne kuzaliwa kati ya watoto saba wa Elisaria Msuya, Ester, alisema wauaji hao hawakuwa na nia ya kuiba, bali ni kuua kwa sababu hawakuchukua kitu chochote zaidi ya televisheni ambayo nayo waliitupa mbali na nyumbani.
Ester alisema mara ya mwisho kuonana na marehemu ilikuwa Mei saba walipokutana benki na mazungumzo yao yalihusu hali ngumu ya maisha.
Alisema hakuwahi kumwambia kama ana ugomvi na mtu kwa sababu alikuwa mpole na msiri.
Akielezea tukio hilo alisema inaonekana kulikuwa na purukushani kubwa chumbani kwa sababu besela la kitanda lilikuwa limevunjika na neti ilikuwa imetoka, huku nyaraka zikiwa zimepekuliwa na kusambazwa karibu kila kona ya chumba.
“Walikuja kuua, kuna kitu walikuwa wanatafuta katika nyaraka pia, ooh... Aneth umekufa kinyama, umechinjwa kama mnyama,” Ester alishindwa kuendelea na kuanza kulia na baadaye kidogo alisema wauaji walimkata marehemu koromeo lakini hawakutenganisha kichwa na kiwiliwili.
Simulizi ya mtoto
Mtoto wa marehemu mwenye umri wa miaka minne ambaye alikuwa akiishi na mama yake alisema: “Walikuja watu watano weusi usoni, wakanifanya na kitu shii usoni, nikalala kwenye kiti mbu wameniuma hadi niliposikia gari la shule likiita pipii, nikaamka na nikamuamsha mama anivalishe nguo za shule lakini akakataa kuamka, ”alisema mtoto huyo na kuongeza.
“Nikavaa mwenyewe nguo za shule na nikamwambia mama nitaendaje shule huku sijafanya “Home work” lakini mama hakujibu, mbu walining’ata pale kwenye kochi nilipolala, nikatoka nje nikakuta gari limeshaondoka, nikaenda kwa mama Salum,” alisema.
Alisema alienda huko akale kwa sababu njaa ilikuwa inamuuma hakula jana yake baada ya ‘wageni’ hao kuja na yeye kulala.
Alieleza kuwa alipowaambia mama yake hamjibu amelala tu alirudi na dada ambaye amemsahau jina kutoka hapo kwa mama Salum ambaye alipofika nyumbani kwao na alipomuona mama yake alianza kupiga kelele.
Ester alisema mwili wa marehemu utasafirishwa Jumatatu ijayo kuelekea kijijini kwao Kairo, Simanjiro mkoani Manyara.
Mtu wa karibu na familia ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema mbali ya kaka yao Erasto kuuawa kwa risasi, dada yao Ester akiwa na mumewe katika Baa ya Hongera, Dar es Salaam alipigwa risasi na kunusurika kufa.
Hata hivyo, alipopigiwa simu kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Gilles Muroto alisema hakuna habari mpya; “kwa sababu imeshazungumzwa sana.”