Kukata cheni ya kizazi cha umaskini

Kukata cheni ya kizazi cha umaskini

KING ASSENGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
929
Reaction score
1,494
Kama Kikwete kizazi chake kinavyorithishwa kushika nafasi za uongozi wa nchi hivyo hivyo ndio kizazi cha familia nyingi kina ridhishana umaskini.

Unavyompondea baba yako na kumwita maskini usisahau watoto wako nao watakuita hivyo hivyo kama hautabadilisha maisha uliyonayo na kujidekeza ukijiita mtoto wa maskini na wanao watakuwa nao hivyo hivyo wakijiita mtoto wa maskini kizazi chenu chote kitakuwa ni watoto wa maskini. Nani basi wa kuivunja hii cheni ya umaskini.?

Kwanza tatizo kubwa linalotesa wengi wazidi kuishi kwenye umaskini ni mtazamo finyu aliokutana nao kwenye maisha ya wazazi na hata majirani.

Inawezekana hakuna hata tajiri kijijini kwenu ili uweze kupata mtazamo wa kitajiri na kukusudia kuwa tajiri na kubadilisha maisha ya kijijini kwenu na familia yenu na kizazi chenu kiwe kizazi cha kukua kadiri siku zinavyoenda .

Pia marafiki ulionao wote wanamtazamo wa kupotezea maisha. Hawana habari na maisha hakuna aliyechangamka kutafuta maisha. Lingine ni kuona kesho nayo ipo bila kujua leo ikishapita imepita kesho nayo itapita na mabadiliko unapaswa kuanza sasa hivi.

Hatutegemei kabisa familia ya mohamed dewji ije ishuke kiuchumi bali tunategemea kabisa itazidi kupaa inawezekana tena mtoto wa Mo akafanya makubwa kuliko baba yake.

Familia nyingi akibahatika mtoto mmoja kufika chuo basi ni nadra sana wanaomfuata kuishia njiani. Ukiniuliza sababu ni mtazamo wanaofuata wakifeli wataonekana wazembe lakini mtangulizi akifeli ni nadra sana wengine kufaulu.

Inahitaji neema ya Mungu. Kuna familia zina pambana bado angalau ziwe na mtoto aliyehitimu kidato cha nne na bado hazijafaulu.

Nikushauri kijana mwenzangu . Ukitaka kuvunja umaskini wa familia tumia nguvu jitahidi upate laki 6 nenda sehemu za mkoa wa pwani au chanika kule sehemu ambazo kwa hela yako utapata heka mbili.

Ukishafanya hilo jitahidi tena lirasimishwe hilo eneo . Endelea zako kupambana kuuondoa umaskini kivingine kwa mapambano makali angalau miaka 10 . Natumaini dhamani ya hilo eneo itakuwa sio ya kitoto.

Na utakuwa umepiga hatua nzuri ya kuvunja umaskini wa familia badala ya unge risk hiyo fedha kwenye biashara nyingine umaskini haukwepeki kirahisi huko.
 
Huyu mzee anaiharibu sana hii nchi.

Anataka kutengeneza ufalme ambao kiuhalisia haitawezekana.

Tamaa mbaya sana.

Hataki kutuacha huru.
 
Huyu mzee anaiharibu sana hii nchi...
Mlishindwa kutumia vyema nafasi mliyopewa mkawa mnapiga nyundo wenzenu badala ya kujiimarisha sponsa kapotea kidogo tu full malalamiko
 
Mlishindwa kutumia vyema nafasi mliyopewa mkawa mnapiga nyundo wenzenu badala ya kujiimarisha sponsa kapotea kidogo tu full malalamiko
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.

Hata hawa wanaotamba sasa watapita kama upepo na watasahaulika haraka sana kwakua hakuna ambalo wamefanya la kugusa mioyo ya watu zaidi ya kuwaibia.
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.

Hata hawa wanaotamba sasa watapita kama upepo na watasahaulika haraka sana kwakua hakuna ambalo wamefanya la kugusa mioyo ya watu zaidi ya kuwaibia.
Mkiendelea hivyo mpaka vitukuu watakufa kwa kwashakoo
 
Huyu jamaa mbona ana nondo ivoo. Naomba kujua ndio life style lake au anafanya ekitini, Je yuko mentally fit
Nilitumiwa tu Chief sijui hata ni wapi hukoo.
 
Back
Top Bottom