Kukamatwa kwa Dkt. Mashinji na Viongozi wengine wa CHADEMA: Maoni ya Dkt. Slaa

Dr Willibrod Slaa

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
675
1,523
Ndugu zangu Watanzania,

Nimesoma kwa umakini "Taarifa" ya kukamatwa na kupelekwa Kituoni Katibu Mkuu wa Chadema na Viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa na Kanda, kule Mbamba Bay, wakiwemo Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz. Mara kadhaa viongozi wa vyama mbali mbali pia wamekamatwa. Nimeshindwa kuelewa hasa tatizo la Msingi ni nini kwa kuwa Taarifa zinatolewa kwenye mitandao ya Jamii ki ushabiki zaidi. Hivyo mtu yeyote makini mwenye nia ya kulisaidia Taifa au kwa kushauri au kukemea anashindwa kwa kuwa " facts za msingi" haziwekwi wala kujadiliwa; wala na mtoa " thread/post au hata na wachangiaji. Namshukuru Mkurugenzi Kibatala, Wakili Msomi Mallya na wasaidizi wake mara kadhaa wamejaribu kutoa ufafanuzi katika hatua ya kesi lakini bila facts za matukio. Ni wazi katika hatua hiyo siyo jukumu lao kutoa facts kwa kuwa itaharibu kesi yao.

Hata hivyo, baada ya kusoma mara kadhaa Taarifa ya matukio haya nimepaswa kurejea Political Parties Act, ( RE 2002) na Kanuni zake zote.

1) Kimsingi, Watu wengi wanaamini kuwa Vyama vya siasa viko huru kufanya Mikutano ya ndani bila kutoa " Taarifa" ( Notice) Taarifa kwa Mamlaka husika ya Police katika eneo. Kifungu cha 11 (1-7) chahusika. Hii ni imani iliyojengwa visivyo, na utaratibu huu usipofuatwa wahusika hulalamika kuwa wanakandamizwa na kunyimwa haki za kidemokrasia na yote yanayoendana na hayo.

Ili sisi tusioegemea upande wa Chama chochote, bali ni Wapenzi wa Taifa na kwa Taifa lolote katika ulimwengu wa leo vyama imara ni muhimu kwa maendeleo ya Kiuchumi na kisiasa. Ninaomba mwenye facts za matukio haya atuwekee ili tuweze kujadili with " objective and unbiased observations". Ebu tuachane na kauli zisizojengwa katika misingi ya kisheria kuwa " mikutano ya ndani haihitaji utoaji wa Taarifa". Ni kweli Mikutano ya Vyama vya siasa iwe ya nje au ya ndani haihitaji " Kibali cha yeyote wakiwemo Polisi ( Hukumu ya Mahakama Kuu).

2. Pamoja na maelezo hayo kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa niliyotaja hapo Juu, mamlaka ya Polisi katika kudhibiti vyama vya siasa yapo pale pale iwapo utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na utaratibu uliowekwa na Sheria na Kanuni haukufuatwa. Utaratibu huo ni pamoja na kutoa " Notice" ( Taarifa) kwa Mamlaka husika ya Polisi katika eneo husika.

a) Iwapo utaratibu wa kutoa Taarifa umefuatwa, Mamlaka ya Polisi hayawezi kukataza mkutano ulioombwa ( wa ndani au wa nje) isipokuwa kwa sababu zilizotajwa ndani ya Sheria.

b) Taarifa za Ki-inteligensia au kugongana mikutano ya vyama ni sababu mojawapo ya mamlaka husika kuzuia mkutano uliotolewa Taarifa. Lakini Mamlaka hiyo inatakiwa kutoa siku/ muda mwingine au hata eneo lingine/ uwanja mwingine Mkutano huo unapotakiwa kufanyika. Hili ni hitaji la kisheria na siyo hisani ya mtu au kiongozi yeyote,

3) Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vya Siasa vina haki ya kufanya mikutano ya kisasa, ya ndani na ya hadhara kwa lengo la kutafuta wanachama. Haina mantiki kuwa na "ndoa" ambayo wana ndoa hao wanawekewa masharti wasipate watoto kwa utaratibu ulioko ndani ya masharti ya Taratibu zilizoko katika Imani iliyowaunganisha katika ndoa hiyo. Kufanya hivyo ni kumaliza kizazi cha wana ndoa hao. Mimi siamini na sijaona mahali popote "Decree" ( Amri ya Rais) inayozuia Mikutano ya vyama ya nje wala ya ndani. Aliyeiona aniwekee humu jukwaani, Hivyo siamini kabisa kama kuna Katazo la Rais, ukiacha matamko ya kisiasa. Kauli ya Rais si sheria na haiwezi kuvunja Sheria iliyotungwa na Bunge ( Sheria na 5 ( RE 2002 ni sheria halali iliyotungwa na Bunge). Ninaamini kabisa kama kuna amri yeyote ya Rais, chama makini kingeli " challenge" amri hiyo chini ya vipengele vya sheria vya " Prerogative Orders za Certiorari, Prohibimus na Mandamus". Wanasheria wanajua vizuri matumizi ya sheria hizo katika kudhibiti matumizi mabovu ya mamlaka ya kuiongozi yeyote. Hivyo, tusitafute majibu mepesi katika " udikteta". Ni muda mwafaka sasa kutafuta majibu sahihi penginepo.

4) Ni wazi kabisa, na nimemsikia Waziri wa Mambo ya ndani akitamka mara kadhaa kuwa mikutano ya Vyama ( ya hadhara na ya ndani ) haijapigwa marufuku alimradi utaratibu unafuatwa. Ni kwa msingi huu, ningependa sasa wapenzi wa vyama kuanza kubana viongozi wao kujua kama kweli " Taratibu" zote zilizowekwa na sheria zimefuatwa katika maandalizi ya mikutano ya vyama vya siasa. Tukumbuke Sheria yetu ya Vyama vya Siasa ni ya 1992 ( RE -as amended 2002) na Kanuni zake na tukumbuke Sheria inayoongoza Jeshi la Polisi ni za 1959 ( kama sikosei- sijacheki- na marekebisho madogo madogo kadhaa yakiwemo ya 2002). Hivyo Rais aliyeko madarakani kwa kutambua uwepo wa sheria hizo na kuzisimamia kama alivyoapa kusimamia Katiba na sheria hawezi kulaumiwa. Tangu ameingia madarakani siku takriban 600 zilizopita Rais aliyepo chini yake hapajatungwa sheria yeyote ya kudhibiti vyama na wala hakuna marekebisho yaliyofanyika, labda kama yamenipita pembeni, basi nielimishwe.. Katika hali hiyo tusipende kutafuta majibu mepesi kishabiki bila kufanya utafiti wa kina wa Tatizo linalosibu Taifa na Demokrasia yetu.

5) Ni kweli Pia kuwa Polisi kwa kutumia Sheria za zamani zisizoendana na wakati, na bila waendesha Kesi wa Serikali ( kama ilivyo desturi katika kesi nyingi) kufanya maandalizi mazuri kesi nyingi zinazofunguliwa chini ya kinachoitwa kesi za " uchochezi" ( ambazo mimi mwenyewe kama Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama nilifunguliwa) au hasiendelei, au hatimaye hushindwa mahakamani kwa kukosa maandalizi hafifu ya Prosecutors au kwa kesi zenyewe au ukamataji kukosa misingi ya kijinai katika mazingira halisi ya leo. Ni wazi kesi hizi huchafua siyo tu jina la Serikali iliyoko madarakani bali pia sifa nzuri ya Taifa letu. Ni muhimu Maofisa Polisi kutimiza majukumu yao kwa umakini mkubwa na uangalifu mkubwa, na hasa kufuata misingi ya kisheria na kulinda Sheria za nchi bila kufanya mambo kwa kumpendeza mtu yeyote awaye. Taifa ni letu sote, mambo yakiharibika, sote tutaumia pamoja na mamlaka zenyewe za polisi, kwani leo uko kwenye madaraka kesho atakuwepo mwingine.

6) Maelezo kuwa Chama Tawala kinafanya "Mikutano" ( ya ndani au ya nje) haiwezi kuwa hoja yenye nguvu. Kwani kama " wametimiza hitaji la " Notice" inayohitajika kisheria kama utaratibu wa kisheria unavyotaka lazima wapige "mbiu" au wawatangazie. Nani kafanya utafiti kwenye ma faili ya mamlaka husika kuwa "hawakufuata" utaratibu wa kisheria. Hii ni hoja dhaifu sana kuhalalisha "kutotafakari na kufanya utafiti" katika wa kina.

Nimalizie tu kwa kusema kuwa, inauma kila siku kuona viongozi wa vyama wakikamatwa, na baada ya muda kuachiwa mahakamani. Ni dhahiri kuna dosari mahali. Au waliokamata hawakuwa makini, au walikuwa wakitaka kumpendeza au wanajipendekeza kwa malengo wanayojua wenyewe. Au kama nilivyoeleza Waendesha Mashtaka wa Serikali, DPP na wasaidizi wake wakiwemo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hawajiandai vizuri.

Kwa kumalizia nirudie tena kuwa wakati ufike sasa Wapenzi wa Vyama na wapenda demokrasia kwa ujumla tusipende sana kujadili mambo kwa ushabiki bali tuanze kuwa na "Critical analysis" ya hali inayokabili demokrasia yetu na kuanza kuhoji viongozi wetu wa vyama. Viongozi wawe wazi kama wamefuata Taratibu za kisheria au wamezoea kufanya mambo kwa " mazoea tu". Hakuna mahali popote sheria inapotamka kuwa "Mikutano ya ndani ya Vyama" haihitaji " Notice". Wala Mamlaka ya Polisi hasa vifungu vya 43, 44 etc vya Police Ordinance, ( kama sijakosea) havijarekebishwa wala kuondolewa, hivyo vikitumika tusilalamike, bali tuwalalamikie viongozi wetu kwa kutokuwa " Proactive" vifungu hivyo vilivyotungwa wakati wa ukoloni vifanyiwe marekebisho ya msingi ili demokrasia ya kweli iweze kujenga msingi katika Taifa letu. Wanasheria wa vyama ningelipenda wawasaidie wapenzi wa vyama katika kutoa elimu ya msingi, lakini pia kuwashauri vizuri pia viongozi badala ya kusubiri " kesi mahakamani".

Nawasilisha.
 
Ni Kwanini unaamini kwamba hawakuomba kibali je umeshindwa kuwapigia na kuwauliza au una kinyongo nao tangia walipokuudhi?

Kama wanakamatwa na kushinda kesi mahakamani unajifunza nini juu ya aliyewakamata? Umesema Watu waongee fact ambalo Ni jambo jema unadhani wewe umeongea fact gani? Uko Canada na unajua siasa za vyama vingi Tanzania Ni Kweli hukusikia Raisi aliposema hakuna mikutano ya hadhara?

Wakati ule unatangaza list of shame ulipata kibali? Unadhani leo unaweza kuwa na nafasi hiyo kama hiyo bila kuwekwa ndani? Unadhani wakati wote ulipowekwa ndani ulikuwa hukufuata taratibu?
 
Ni Kwanini unaamini kwamba hawakuomba kibali je umeshindwa kuwapigia na kuwauliza au una kinyongo nao tangia walipokuudhi?

Kama wanakamatwa na kushinda kesi mahakamani unajifunza nini juu ya aliyewakamata? Umesema Watu waongee fact ambalo Ni jambo jema unadhani wewe umeongea fact gani? Uko Canada na unajua siasa za vyama vingi Tanzania Ni Kweli hukusikia Raisi aliposema hakuna mikutano ya hadhara?

Wakati ule unatangaza list of shame ulipata kibali? Unadhani leo unaweza kuwa na nafasi hiyo kama hiyo bila kuwekwa ndani? Unadhani wakati wote ulipowekwa ndani ulikuwa hukufuata taratibu?
Umemuliza maswali ya msingi...
 
...Kwa kumalizia nirudie tena kuwa wakati ufike sasa Wapenzi wa Vyama na wapenda demokrasia kwa ujumla tusipende sana kujadili mambo kwa ushabiki bali tuanze kuwa na "Critical analysis" ya hali inayokabili demokrasia yetu na kuanza kuhoji viongozi wetu wa vyama...
Bahati mbaya kuna watu hawapendi kabisa kusikia ushauri murua kama huu.
 
Daktari Slaa,

Najua wewe sio mgeni wa siasa zetu, umeshiriki katika harakati nyingi za kuieneza chadema.

Najua yanayotokea sasa yalishawahi tokea huko nyuma ww ukiwa ni katibu mkuu wa chadema.

Uzuri tunakumbuka ulikuwa mmoja wa kupinga haya yanayotokea sasa kipindi kile ukiwa katibu mkuu, na hata wewe mwenyewe uliwahi katazwa kufanya mkutano wa kisiasa.

Sidhani kama Chadema wameshindwa kufuata taratibu za kufanya mikutano yao ya nje ndio iwe sababu ya wao kukatazwa kufanya mikutani ya kisiasa.

Kinachotokea hapa nyumbani, ni wazi Mkuu wa nchi bado ana hofu ya kuyumbishwa kwa wananchi kwa anayo yatenda.

Mkuu wa nchi hataki kupingwa, hataki kusemwa vibaya. Mkuu wa nchi anataka yale ambayo anayatenda basi asifiwe na kupongezwa kwa maandamano.

Hii ni moja ya mikakati ya kumrahisishia katika uchaguzi ujao asitumie nguvu nyingi kujinadi kwani mabaya yake yatakua hayajulikani.

Tatizo demokrasia hii ambayo tumeirithi toka huko kwa wazungu hatukuandaliwa kuipokea, na haya ndio matokeo yake.
 
Daktari Slaa,

Najua wewe sio mgeni wa siasa zetu, umeshiriki katika harakati nyingi za kuieneza chadema.

Najua yanayotokea sasa yalishawahi tokea huko nyuma ww ukiwa ni katibu mkuu wa chadema.

Uzuri tunakumbuka ulikuwa mmoja wa kupinga haya yanayotomea sasa kipindi kile ukiwa katibu mkuu, na hata wewe mwenyewe uliwahi katazwa kufanya mkutano wa kisiasa.

Sidhani kama Chadema wameshindwa kufuata taratibu za kufanya mikutano yao ya nje ndio iwe sababu ya wao kukatazwa kufanya mikutani ya kisiasa.

Kinachotokea hapa nyumbani, ni wazi Mkuu wa nchi bado ana hofu ya kuyumbishwa kwa wananchi kwa anayo yatenda.

Mkuu wa nchi hataki kupingwa, hataki kusemwa vibaya. Mkuu wa nchi anataka yale ambayo anayatenda basi asifiwe na kupongezwa kwa maandamano.

Hii ni moja ya mikakati ya kumrahisishia katika uchaguzi ujao asitumia nguvu nyingi kujinadi kwani mabaya yake yatakua hayajulikani.

Tatizo demokrasia hii ambayo tumeirithi toma huko kwa wazungu hatukuandaliwa kuipokea, na haya ndio matokeo yake.
Siyo kama hajui ila anajifanya tu.
 
Kwanza nashukuru umeupandisha huu uzi hapa jamvini wewe mwenyewe nilipouona kule Facebook jana nimefanya juhudi ya kuupandisha nadhani mods wameuondoa kupisha huu hapa.

Lakini ni vyema nikaweka maoni yangu hapa pia. Dk Slaa ni kweli yawezekana ukawa na nia njema na unayoyaongea siyapingi yote ila kuna vielementi vya kubadilika labda ni ule ubinadamu wanasema usinukuu kauli za mtu akiwa hai hachelewi kuzikanusha ndiyo maana watu husubiri mtu akifa ndiyo huanza ku quote zile ambazo zimesimama hazijakanushwa mpaka mauti. Kuna mambo ambayo pengine ukiri mwenyewe kwamba ulitupotosha wakati ule au sasa ndiyo unatupotosha, ulituambia kwamba hatuhitaji kutoa notice kwa mikutano ya ndani na huo msimamo uliusimamia Iringa 2012 na kwingineko. Leo kipi kimekubadilisha?.

Nisiwe na mengi zaidi ni kwamba siasa zile za kipindi chako na hizi za Mashinji zina utofauti mkubwa kwa sasa kuna ukandamizwaji mkubwa wa demokrasia na mpaka huwa najiuliza akina mbowe wameruhusu haya yatokee? Wana mpango gani? Imefika wakati tunaishia tu kukomenti humu Katibu kakamatwa, oh mdee masaa 48 kweli tutafika kwa upole huu?

Nadhani ni wakati wa viongozi kuja na lugha ambayo itaeleweka vyema kwa polisi na viongozi wengine wa serikali kama Kenya waliweza why sisi tushindwe?

Ahsante
 
Hahahahaa...kwamba awaache mpambane na hali zenu enh?
Kasahau kipindi mchumba Josephine wanataka waoane zengwe lilioanzishwa na kina Sophia Simba wakishirikiana na Rose Kamili pale bungeni sembuse mambo ya vibali?

Nasikitika kuna kipindi huyo mzee nilikuwa na mu idolise namuona mtu wa maana katika siasa, nikisoma posts zake kama hizi naona ule ni muda niliopoteza kuwa na role model wa aina hii
 
Dr Slaa

Ingawa umejitahidi kuwa 'impartial' maelezo yako ya mwisho yanaonyesha hoja yako ilipo

Kuna mambo mawili matatu unayochanganya

Kwanza, kuna hoja ya mikutano ya ndani. Wakati unazungumzia notice za mikutano kama kitu cha lazima, hujazungumzia uhuru wa mikutano ya nje kama haki ya kikatiba

Kwa maneno mengine unakubali zuio la mikutano yote bila kujali demokrasia na katiba

Pili, kuna suala la kuvunja sheria ambalo mhusika anatakiwa afikishwe mbele ya sheria
Je, huoni kuweka watu mahubusu bila kuwafungulia mashtaka ni kukiuka haki ?

Tatu, kuna trend ya kukamata watu siku ya Ijumaa ili walale mahabusu hadi Jumatatu
Baada ya hapo wanaaachiwa huru, je huoni matumizi mabaya ya nguvu na madaraka

Nne, kuna tukio la mtu kuzindua kitabu na mkutano kuzuiwa.
Je, suala kama hilo linahitaji kibali na kinatoka wapi?

Kuwa CCM au Chadema kunaondoaje haki ya kufanya mambo ya maisha nje ya siasa!

Tano, ikiwa unaamini CCM wanafuata taratibu na inaweza kuwa kweli, ni taratibu gani zinazowawezesha kufanya mikutano ya nje ambayo wapinzani hawaruhusiwi?

Hoja hailengi kutetea wanaokiuka taratibu, imelenga kuhakikisha haki inatimia.

Haki inatekelezwa kwa mtuhumu kumfikisha mtuhumiwa mbele ya sheria.
Ikiwa kuna uvunjifu wa sheria , adhabu ni haki.

Tuna sheria za watu kuwekwa ndani 48hr. Kama tutaendelea na mtazamo wako, abuse hiyo itaendelea tu tukijua wanaofanya hivyo ni makada wa chama wenye kofia za serikali

Kesho wapinzani watawekwa mahabusu 48 kwasababu tu kuna mtu ana mamlaka
 
Pamoja na mazingira ya kisiasa kwa upinzani yamekuwa magumu, lkn upinzani umeshindwa kubadilika kutokana na mazingira.

Kwa sasa dunia ni ya digitali, Jamii kubwa ya watanzania wanatumia internet.

Chadema na upinzani wanaweza fanyia mikutano yako kupitia mitandao na kueneza itikadi yao, kueleza mazaifu ya serikali na kujitangaza zaidi.

Kuendelea kulalamika, haitosaidia mwisho wa siku uchaguzi unakaribia.
 
Dr. Slaa umejenga hoja safi kama wewe ungekuwa hujawahi kuishi Tanzania au kushiriki siasa za Tanzania wewe ni Gwiji wa siasa za Tanzania unazielewa vizuri kuwa matumizi ya vibali yapo kwa ajili tu ya kupambana na wapinzani na hata mahala ambapo vibali vimeombwa havitolewi hati kwa sababu sheria inasema wahusika waombe vibali kabla ya kufanya mkutano haimaanishi kuwa kibali kitatoka umeishi Tanzania and i am sure you are aware of that.

Ushahidi mzuri mkutano wako wa kufungua Tawi huko Iringa Nyororo mpaka ikapelekea kifo cha Mwangosi, polisi walichokifanya unakijua, ufunguzi wa tawi na mkutano wa ndani ya tawi.

Kinachoshangaza ni wewe kutojua tamko la Rais la kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwani dunia nzima inajua na maafisa wa polisi wanatumia Tamko hilo kupinga mikutano ya hadhara pamoja na kwamba ni kinyume cha sheria lakini wewe unaijua Tanzania sheria zinatumika tu kwa lengo maalum na wavunja sheria wamekuwa wakizawadiwa mfano mzuri RPC Iringa aliyesimamia mahuaji ya Mwangosi.

Kosa kubwa linalofanyika ni moja tu nalo ni ofisi ya DPP kukubali kutumika kama weapon au political football na Serikali ya CCM kupambana na wapinzani ushahidi mzuri ni kesi ya Lema ambapo jaji wa mahakama ya Rufaa alilaani kitendo cha dpp kutumia mamlaka yake vibaya kumkatalia Lema dhamana wkt kosa linaruhusu dhamana.

Goodluck Dr Slaa we miss u.
 
Back
Top Bottom