Huu utamaduni wa kuchangiana harusi kwakweli itabidi ufe
La msingi zichuje angalia za muhimu wape mchango wengine wachunie maana siku hizi mtu hata ukikutana kwenye daladala ukisalimiana nae ukamchekea anakupa kadi anakwambia mpwa wake anaoa/olewa
Huu utamaduni wa kuchangiana harusi kwakweli itabidi ufe
La msingi zichuje angalia za muhimu wape mchango wengine wachunie maana siku hizi mtu hata ukikutana kwenye daladala ukisalimiana nae ukamchekea anakupa kadi anakwambia mpwa wake anaoa/olewa
Kadi za harusi? We acha tu! Kuna wakati zilinisababishia headache mpaka nikachanganyikiwa. Ikafika kipindi nikaweka mkakati kuwa hata nipewe kadi kumi, nitachangia kadi mbili tu kulingana na closeness na wahusika. Zinazobaki kapuni.
Vikao vya harusi? Huwa inategemea kama nina nafasi au la. Otherwise, napiga chini. Unajua jumapili mara nyingi ndiyo huwa muda wa kupumzika hivyo hakuna haja ya kubeba majukumu mengine ukajikuta unaenda kazini jumatatu ukiwa hoi.
Tusielewane vibaya jamani, lakini haya mambo tunapoelekea yatarudi kuwa ya kifamilia kama ilivyokuwa zamani!
Lakini ndiyo mwanzo wa kuwapoteza
Wadau mwenzenu nimejaaliwa kuwa na marafiki wengi sana ukiachilia mbali wale niliofahamiana nao katika maisha ya shule na nika-maintain urafiki nao, lakini bado katika mazingira ya kazi na maisha ya mtaani napendelea sana ku keep in touch na watu wengi sana ambao nakutana nao. Kama mjuavyo watu wengi maisha huanza kwa kuwa wapangaji, hapa Dar maisha nilianzia Manzese nilikaa mwaka mmoja na nikajikuta nina marafiki kibao, nikahamia Sinza nikapata marafiki kibao, Nikahamia Tabata nikajipatia marafiki kibao, nikahamia Mbezi Tank Bovu nikajipatia marafiki pia, na mwisho nipo Tegeta nako nimepata marafiki wapya wengi tuu na kama kawaida huwa na keep in touch Miaka yoote nimekuwa nafanya hivyo kwa makusudi kabisa kwasababu nimekuwa nikisikia kwamba kujuana na watu wengi(Networks) ni kitu muhimu sana.
Mpaka sasa sijajua umuhimu wa kujuana na watu wengi zaidi ya Usumbufu, kwa mfano hapa nilipo nina kadi kumi na nane 18 za michango ya Harusi, Send offs, Vipaimara, Anniversaries nk. Haishii hapo nina SMS Tatu zinaniomba nihudhulie hizi weekend mbili bila kukosa vikao vya kwanza vya Harusi na Sendoffs.
Kujuana na watu wengi kumenifanya ghalama zangu za kuishi ziwe kubwa sana. Nifanye nini ili uwingi wa marafiki zangu na mimi uninufaishe???
Kujuana na watu wengi ni faida kubwa ila ukiangalia faida ya kitu utaona hakuna maana!napili kuna mkundi yakujuana hivyo unaweza kuwa na kundi la marafiki lakini ukiwa na shida ya ukweli hakuna rafiki hivyo yakupasa uwe mwangarifu sana na marafiki!!mimi binafsi napenda marafiki lakini marafiki wangu ni wale wakutoa ushahuri siyo wakuwalilia shida!Mfano unaenda baa umekunya pombe zako mara polisi wamekuja wanamtafuta mtu kaua kakimbia lakini mavazi ya huyo aliyekimbia nikama yako wanakuchukua na wanasema niwewe jambazi uliye ua kwa bunduki&na wanataka hiyo smg wewe unasema siyo mimi jamani wanasema niwewe!je katika marafiki zako wote kuna mtu anaweza akapiga simu kuongea na Kova,au IGP,Vua Naodha,au watu wa sampuli hiyo?kama unao basi hao ndo marafiki wako na wakuwaintateini.
Kwasababu ni rafiki yako!!!Niwapoteze kwasababu sichangii vitu ambavyo sio vya msingi? Acha niwapoteze tu. Kama wana shida, ugonjwa, hawana chakula naweza hata nikakopa kwaajili yao ila mambo ya harusi hapana. Kwanini mimi nigharamie sifa za mtu mwingine?
Kwasababu ni rafiki yako!!!