Oxpower
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 2,161
- 3,054
Wakuu habari za kazi.
Baada ya salam naomba niende moja kwa moja kwenye mada
Mimi ni kijana ambae toka muda mrefu nimekua nikitamani sana jeshi na sheria lakini kidogo mazingira yakaniletea shida na hii ni kutokana na mkinzano wa mawazo.
Nlipomaliza kidato cha sita nikataka kujiunga na maombi nikatuma lakini mama yangu akaniambia mbona umefanya vizuri kwanini usiende kusoma hiyo sheria na mimi nlitaka kusoma sheria Mlimani tu.
Mwaka wetu ndo tulianzia kuomba kupitia TCU na ilikua unajaza facult kama 8 hivi.
Nikajaza lakin sikuweka education, baadae baba akanambia mbona hujaweka education na wewe umesoma arts subjects na huu mwaka wenu unaonekana sio mzuri sana.
Basi mimi nkaedit nikatoa moja na nikajaza education.
Ile post zimetoka tu, nkakuta ni education na mimi sikuwahi kuwaza, nkaenda hivyo hivyo kwa lengo la kubadilisha, lakini nlipofika wakanigomea.
Basi nikaendelea na education na baadae nikafurahi sana kusoma education na mwaka jana nmeajiriwa na nimekua mwalimu na naufurahia uwalimu wangu japo haikua ndoto yangu.
Sasa kilichonifanya nije kwenu kuomba ushauri ni hiki, hivi karibuni nmejikuta tamaa yangu ya jeshi imerudi na muda mwingi nashinda jeshini mazoezini, mazoezi ya mpira wa kikapu.
Nmejikuta tamaaa yangu imezidi, nataman kwenda jeshini ila sijui haya.
1:Nikituma maombi ya kujiunga na jeshi, je inatakiwa nitoe taarifa kwa mwajiri wangu
2:Na je ikitokea JWTZ hawajanichukua baada ya kumaliza JKT nawezaje kurudi kwenye kada yangu.
3:Je inawezekana nikajiunga na JWTZ bila kupitia JKT
Kwa wenye kujua lolote au waliowahi kufanya hivyo nawategemea sana
Alafu mmetumia simu na inasumbua kidogo, kwa hiyo kuna sehemu naweza nikawa nimekosea, naomba elewa tu na usiifanye iwe mada.
Natanguliza shukran kwa wote mtakaochangia