Kujitoa katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ni sawa na mkulima kula mbegu

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
*Mambo 10 muhimu kuyaelewa kuhusu Hifadhi ya Jamii

Upo mjadala unaoendelea na kufukuta kuhusu uamuzi wa Serikali kupeleka Muswada wa Sheria Bungeni kufanya marekebisho katika Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Muswada huo sijauona na haujawekwa hadharani. Hata hivyo, lililopenyezeka katika vyombo vya habari ni taarifa ya azma hiyo ya Serikali iliyotamkwa katika kikao cha Serikali na wadau kuwa Muswada huo utafuta FAO LA KUJITOA.

Nimefuatilia mjadala huo na kuisoma barua ya wazi ya vyama vya wafanyakazi kwa umma ikilaani vikali nia hiyo ya Serikali na muswada. Nikasikia na kusoma tena kauli mbalimbali za Serikali na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuhusu azma hiyo na mambo mengine mengi yanayoambatana na muswada unaondaliwa. Kwa maelezo hayo, muswada huo una mambo mengi zaidi ya kinachoitwa fao la kujitoa. Aidha, maelezo yao ni kuwa muswada wenyewe haujakamilika isipokuwa ni hatua ya maoni tu.

Ninachokiona kwa haraka haraka ni kuwepo kwa ombwe la taarifa katika suala hili jambo linalofanya mjadala wenyewe kwenda harijojo. Ombwe hili litafanya hata muswada wenyewe ukitolewa tushindwe kuujadili vizuri na kwa nafasi. Kwa sababu hiyo, nimejitolea kuchokoza mjadala kwa kuyaweka bayana mambo 10 ya msingi ya kuyaelewa kuhusu hifadhi ya jamii kama ninavyoyainisha hapa chini.

1. Ipo tofauti kati ya dhana mbili 'AKIBA YA WAFANYAKAZI' na 'HIFADHI YA JAMII' yaani Provident Scheme na Social Security. Provident Scheme inakupa tu jumla ya fedha wewe na mwajiri mliyochangia siku ya kustaafu na mnaachana kimoja. Social Security inahusisha mnyumbuliko wa mafao ikiwemo malipo ya kila mwezi baada ya kustaafu, matibabu kwa mtu na mwenza, gharama za maziko na malipo kwa mjane na kusomeshewa watoto. Kutokana na uchanga wa mifuko hii, mafao bado yanatofautiana kati ya mfuko na mfuko hatimaye mbeleni mafao yanapaswa kufanana katika mifuko yote.

2. Hifadhi ya Jamii ni Haki ya Kikatiba na si suala la hiyari. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa kila mtu anahaki ya kupata hifadhi. Aidha Hifadhi ni Haki ya Binadamu katika Tamko la Haki za Binadamu na Mikataba ya Shirika la Kazi Duniani. Haki hiyo inaambatana na wajibu kwa Serikali, Mwajiri na Mfanyakazi. Serikali kusimamia na kuhakikisha Haki hiyo inatolewa na kupatikana, Mwajiri kumchangia Mfanyakazi na Mfanyakazi kuchangia kwa mujibu wa Sheria.

3. Hakuna kitu kinachoitwa FAO LA KUJITOA kulikuwepo na KUJITOA KWENYE MAFAO. Kwa kuwa mifuko iliyopo iliundwa kwa sheria tofauti kwa nyakati tofauti, baadhi ya mifuko ilikuwa bubu kuhusu kipengele cha kukataza kujitoa hali iliyofanya watu kujitoa bila kukataliwa. Hivyo hakuna FAO LA KUJITOA lililofutwa na hakuna Mfuko wowote wenye fao hilo. Kilichofanyika ni kuoanisha Sheria mbali mbali za Mfuko na kuwa na Sheria moja kurahisisha udhibiti na usimamizi ambapo katika Sheria hiyo ya 2012 imetamka bayana kutokuwepo na kujitoa kuziba ombwe lililoachwa na sheria mbalimbali.

4.. Hifadhi ya Jamii ni KINGA si AKIBA. Hifadhi ya Jamii ni sawa na bima ya kumkinga mfanyakazi na mwanachama dhidi ya majanga yanayoweza kumpata na kumpotezea uwezo wake wa kuzalisha na kujikimu. Majanga hayo ni kama kustaafu,kupata vilema na kamwe si mfuko wa akiba na mikopo, chama cha kuweka na kukopa au upatu. Hivyo michango yako katika hifadhi ya jamii haiwezi kuwa mbadala wa wewe kujiwekea akiba na kuwekeza sehemu ya kipato chako inayobaki kwako baada ya kukatwa mchango wako usiovuka asilimia 10 ya mshahara wako(kwa wale wafanyakazi). Kushindwa kwako kuweka akiba hakuhalalishi kugeuza Mfuko wako wa Hifadhi ya Jamii kuwa ni Benki. Hoja ni kuongeza tija na hatimaye mishahara/kipato na kujenga utamaduni wa kuweka akiba (culture of saving).

5. Michango yetu kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni MBEGU ambayo mavuno yake yanatokana namna tunavyoendelea kuyapalilia na kunyunyuzia dawa kwa kuendelea kuchangia. Huwezi kupanda leo na kuvuna kabla ya mazao kukomaa au msimu wa mavuno kufika. KUJITOA KWENYE MAFAO NI SAWA NA MKULIMA KULA MBEGU.

6. Unapostaafu au kwa sababu yoyote unapolazimika kuhifadhiwa na jamii kwa kupewa kinga una uwezo wa kutumia zaidi ya ulichochangia. Hifadhi ya jamii hutoa kinga kwa kadiri ya uhitaji na si kwa kadiri ya mchango pekee. Hii inatokana na uwekezaji unaofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa upande mmoja na muendelezo wa mitiririko ya michango kwa wale ambao bado wako katika umri wa kuchangia. Mafao yako wewe baada ya kuchukua kiinua mgongo yataendelea kulipwa na wale ambao bado wanachangia. Hivyo, kuruhusu watu kujitoa ni kumomonyoa nguzo ya Hifadhi ya Jamii ya vijana na wanaojiweza kuwafaa wazee na wasiojiweza. Ndivyo ilivyo duniani kote.

7.Skimu za Hifadhi ya Jamii tofauti na iliyokuwa skimu ya mifuko ya Akiba ya Wafanyakazi inapaswa kugusa wananchi wote kwa kuwa ni haki ya kikatiba na si wafanyakazi pekee. Inapaswa kugusa wasiojiweza,wasio na ajira, waliojiajiri,wakulima, wanamichezo na wengine walioko kwenye sekta isiyo rasmi. Tuendako kila mtanzania anapaswa kuwa mwanachama wa hifadhi ya jamii kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea ambako namba yako ya uanachama wa hifadhi ya jamii ndio kitambulisho chako kikuu. Hivyo hoja ya kujitoa katika mfuko ulipwe ukajiajiri haijitoshelezi. Huko tuendako hata ukijiajiri hatimaye itakuwa ni lazima uchangie hifadhi ya jamii kama ilivyo lazima sasa kulipa kodi alimradi una kipato kiwe cha kuajiriwa au kujiajiri. Kujiunga katika hifadhi ya jamii kwa wasio waajiriwa katika sekta rasmi ni hiyari tu kwa sasa katika kipindi cha mpito.

8. Tanzania imeingia katika skimu hii mwanzoni mwa miaka ya 2000 tulipobadilisha mifuko iliyokuwapo. Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi (NPF) ukawa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) ukabadilika kutoka kuwa mfuko wa Mashirika ya Umma tu na kuwa mfuko wa kila mtu, na Serikali kuunda PSPF, LAPF nk. Sisi Tanzania ndio tumeianza safari ya kuelekea kwenye hifadhi ya jamii na bado hatujafikia huko. Katika muda mfupi manufaa yameanza kuonekana kadri uwezo wa mifuko unavyoongezeka na kupata faida. Leo tuna bima ya afya, fao la ulemavu kazini, fao la kujifungua, fao la elimu, fao la afya vijijini nk. Huko tuendako, mafao haya yatafanana katika mifuko yote na upo uwezekano wa mifuko yote ya sasa kuunganishwa na kuwa mmoja. Hatuwezi kufika huko ikiwa wanachama wataruhusiwa kujitoa kila wanapojisikia kufanya hivyo maana itaathiri uimara wa mifuko.

9. Kama ilivyo kanuni ya msingi kwa sheria yoyote, katika kila sheria lazima kuwepo na mazingatio (exceptions). Zipo aina ya sekta au kazi ambazo kwa mazingira yake ya asili ya shuruba zake hakuna mfanyakazi anayeweza kuhimili kuwa na uwezo wa kufanya kazi hizo hadi miaka 55. Aina hizi za kazi humfanya mfanyakazi apoteze uwezo wake wa kufanya kazi na kuchangia kutokana na sababu za kiafya (na)au ulemavu. Lazima sheria itambue watu wa aina hii na kazi za aina hii ili kuwawezesha hawa kuanza kunufaika na hifadhi ya jamii kabla ya umri wa kisheria uliowekwa wa kuchangia kwa miaka 15 au kupata mafao ya kiinua mgongo kabla ya miaka 55 kwa hiyari na 60 kwa lazima. Hawa wanahitajika kuwekewa FAO lao (si kujitoa) mahsusi la kuwahifadhi, kuwasitiri na kuwakinga dhidi ya kudhalilika na kufadhaika katika jamii. Hawa wanahitaji hifadhi. Mjadala wetu wafaa kuelekezwa hapo tunapojadili kuhusu marekebisho ya Sheria. Pia tujadili pendekezo la fao la kukosa ajira na ikiwezekana kama tunaweza kutumia michango yetu kama dhamana kukopea nyumba, kujisomesha nk na si kujitoa. Tusipoteze lengo kwa kile alichokisema Mwl. Nyerere, 'Tukipoteza muda mwingi kugawana KIBABA tutapoteza wasaa wa kugawana PISHI'.

10. Mimi na wewe hatuiujui kesho yetu wala hatuna uhakika wa msaada wa ndugu zetu na rafiki zetu pale tutakapofikwa na uzee au janga. Hifadhi ya Jamii ndio mbeleko yetu ya kujishikizia. Mimi na wewe na wengi wetu ambao ndio wafanyakazi wengi wa Tanzania ambao hatujachangia mifuko kwa zaidi ya miaka 15 kuweza kustahili mafao ya pensheni tuna maslahi gani na kujitoa kwenye mafao? Hao viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wanaotutia hamasa mbona wote umri wao umeshakwenda na wamekaa mkao wa kufaidika na pensheni? Tukumbuke Ujana Ukuta na Fainali Uzeeni.

Inawezekana kabisa sijatoa majawabu na ieleweke haikuwa lengo langu. Lengo langu ni kuchokoza tu mjadala. Tujadili.

Ndugu Kibaja Kariongo ni mdau wa harakati za wafanyakazi
 
Hakuna justification yoyote ile ya msingi kumzuia mtu asichukue pesa zake kwenye hio mifuko, sio watu wote wanamipango ya kuajjriwa maisha yote na kupata hio pension inayoanzia 50,000-100,000 kwa mwezi baada ya kustaafu, nadhani ulimsikia profesa wao aliekosa hoja zenye mashiko kuconvince watu waendelee kuziweka hela huko
 
Si kweli kwani mtu anapochangia mchango yake apewe pindi atakapoihitaji asipangiwe matumizi
 
Hivi ukimuajiri House boy nyumbani akapiga KAZI, Ukawa inamtunzia sehemu ya mshahara wake, baada ya Miaka miwili umgeuke kwa kumuambia siku akiacha KAZI hutamlipa ile Pesa uliyo mhifadhia. Je

Akisema umemdhulumu utakataa?

Akisema boss ameishiwa utabisha?
Hiyo Pesa muda Huyo NI yako au ni sehemu ya ujira wake?

Kungekuwa na akaunti Maalumu ya kuhifadhi hiyo Pesa ambayo HATA wewe huruhisiwi kuichukua, je ungepata jeuli ya hayo uliyo sema?

Kwanini Pesa yangu nipangiwe matumizi?
 
Yaani naacha au nafukuzwa kazi au mkataba wangu wa kazi umeisha nikiwa na umri wa miaka 32, na sina mpango wa kuajiriwa tena, alafu ile milioni 10 yangu iliyopo PSPF niisubirie mpaka nifikishe miaka 60, yaani nisubiri mpaka mwaka 2044!!!
Kwanza uhakika wa kufika huo mwaka 2044, pili nikifika huo mwaka 2044 hiyo milioni 10 kipindi hicho itakuwa na thamani gani, tatu uwezekano wa kutunza hizo nyaraka zinazo hitajika ili uweze kupewa hizo fedha hali ya kuwa upo nje ya ajira kwa miaka 28 ukijikita katika kujiajiri mwenyewe.
Mimi hii napata tafasiri kwamba atakayeacha au kuachishwa kazi au mkataba wake kuisha akiwa na umri mdogo na hasiajiriwe tena, hiyo pesa yake ya kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii atakuwa ametoa sadaka na kwa lugha halisi amedhulumiwa. Kwa hiyo lengo la mswada huu ni kumdhulumu pesa za watu, na mleta uzi upo hapa kutetea dhuluma, na kwa taarifa yako hakuna atakaye kuunga mkono isipokuwa dhalimu mwezio kama wewe.
Wewe utakuwa Mbunge wa CCM basi palekeni mswada na mafao ya Wabunge wasipewe mpaka wafike miaka 60
 
Hivi haujiulizi ata wabunge wenyewe hawataki wachukue wakiwa na 55 ila wafanyakazi wengine ndio mpaka wafikishe hiyo 55, pili nikiugua nikaona siwezi endelea na kazi je, na ni kwanini wasiwahite wafanyakazi watoe maoni yao kujua wangapi hawaungi hoja yao mkono, kwanini watake iwe lazima? Kwanini wasipitishe pia iwe hiari kuchangia waone watawapata wangapi? Je nisipifika hiyo 55? Poor decisions, poor Tanzanians
 
Wasomi wa kasumba mnatia hasira sana...I,e badala ya kutafuta masuluhisho ya matatizo ya jamii zinazowazunguka kisayansi(kwa tafiti mlizofanya kwenye jamii yenyewe)...nyie mnakimhilia solution walizo hangaika wenzenu huko Ulaya kutatua matatizo ya jamii zao ...mnazi copy & paste huku kwenu na kuanza kusema dunian kote_mkireferr Ulaya...aaaaagrr...sijui ni uvivu wa kufikiri ama ni mitaala ya elimu tunayoipata ..?
 
Na
ametumwa huyu
Na inawezekana ni Prof.huyu mkuu....waafrica sijui nani katuroga....hapo atakuja na matheory kibaooo ya kukopi toka Ulaya....ataanza kukakamaa shingo na kutoa mapovu.....elimu zetu ni hovyo sana I,e kadri unavyoelimika ndio hivyo unavizidisha ukasuku wa ulaya....
 
*Mambo 10 muhimu kuyaelewa kuhusu Hifadhi ya Jamii

Upo mjadala unaoendelea na kufukuta kuhusu uamuzi wa Serikali kupeleka Muswada wa Sheria Bungeni kufanya marekebisho katika Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Muswada huo sijauona na haujawekwa hadharani. Hata hivyo, lililopenyezeka katika vyombo vya habari ni taarifa ya azma hiyo ya Serikali iliyotamkwa katika kikao cha Serikali na wadau kuwa Muswada huo utafuta FAO LA KUJITOA.

Nimefuatilia mjadala huo na kuisoma barua ya wazi ya vyama vya wafanyakazi kwa umma ikilaani vikali nia hiyo ya Serikali na muswada. Nikasikia na kusoma tena kauli mbalimbali za Serikali na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuhusu azma hiyo na mambo mengine mengi yanayoambatana na muswada unaondaliwa. Kwa maelezo hayo, muswada huo una mambo mengi zaidi ya kinachoitwa fao la kujitoa. Aidha, maelezo yao ni kuwa muswada wenyewe haujakamilika isipokuwa ni hatua ya maoni tu.

Ninachokiona kwa haraka haraka ni kuwepo kwa ombwe la taarifa katika suala hili jambo linalofanya mjadala wenyewe kwenda harijojo. Ombwe hili litafanya hata muswada wenyewe ukitolewa tushindwe kuujadili vizuri na kwa nafasi. Kwa sababu hiyo, nimejitolea kuchokoza mjadala kwa kuyaweka bayana mambo 10 ya msingi ya kuyaelewa kuhusu hifadhi ya jamii kama ninavyoyainisha hapa chini.

1. Ipo tofauti kati ya dhana mbili 'AKIBA YA WAFANYAKAZI' na 'HIFADHI YA JAMII' yaani Provident Scheme na Social Security. Provident Scheme inakupa tu jumla ya fedha wewe na mwajiri mliyochangia siku ya kustaafu na mnaachana kimoja. Social Security inahusisha mnyumbuliko wa mafao ikiwemo malipo ya kila mwezi baada ya kustaafu, matibabu kwa mtu na mwenza, gharama za maziko na malipo kwa mjane na kusomeshewa watoto. Kutokana na uchanga wa mifuko hii, mafao bado yanatofautiana kati ya mfuko na mfuko hatimaye mbeleni mafao yanapaswa kufanana katika mifuko yote.

2. Hifadhi ya Jamii ni Haki ya Kikatiba na si suala la hiyari. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kuwa kila mtu anahaki ya kupata hifadhi. Aidha Hifadhi ni Haki ya Binadamu katika Tamko la Haki za Binadamu na Mikataba ya Shirika la Kazi Duniani. Haki hiyo inaambatana na wajibu kwa Serikali, Mwajiri na Mfanyakazi. Serikali kusimamia na kuhakikisha Haki hiyo inatolewa na kupatikana, Mwajiri kumchangia Mfanyakazi na Mfanyakazi kuchangia kwa mujibu wa Sheria.

3. Hakuna kitu kinachoitwa FAO LA KUJITOA kulikuwepo na KUJITOA KWENYE MAFAO. Kwa kuwa mifuko iliyopo iliundwa kwa sheria tofauti kwa nyakati tofauti, baadhi ya mifuko ilikuwa bubu kuhusu kipengele cha kukataza kujitoa hali iliyofanya watu kujitoa bila kukataliwa. Hivyo hakuna FAO LA KUJITOA lililofutwa na hakuna Mfuko wowote wenye fao hilo. Kilichofanyika ni kuoanisha Sheria mbali mbali za Mfuko na kuwa na Sheria moja kurahisisha udhibiti na usimamizi ambapo katika Sheria hiyo ya 2012 imetamka bayana kutokuwepo na kujitoa kuziba ombwe lililoachwa na sheria mbalimbali.

4.. Hifadhi ya Jamii ni KINGA si AKIBA. Hifadhi ya Jamii ni sawa na bima ya kumkinga mfanyakazi na mwanachama dhidi ya majanga yanayoweza kumpata na kumpotezea uwezo wake wa kuzalisha na kujikimu. Majanga hayo ni kama kustaafu,kupata vilema na kamwe si mfuko wa akiba na mikopo, chama cha kuweka na kukopa au upatu. Hivyo michango yako katika hifadhi ya jamii haiwezi kuwa mbadala wa wewe kujiwekea akiba na kuwekeza sehemu ya kipato chako inayobaki kwako baada ya kukatwa mchango wako usiovuka asilimia 10 ya mshahara wako(kwa wale wafanyakazi). Kushindwa kwako kuweka akiba hakuhalalishi kugeuza Mfuko wako wa Hifadhi ya Jamii kuwa ni Benki. Hoja ni kuongeza tija na hatimaye mishahara/kipato na kujenga utamaduni wa kuweka akiba (culture of saving).

5. Michango yetu kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni MBEGU ambayo mavuno yake yanatokana namna tunavyoendelea kuyapalilia na kunyunyuzia dawa kwa kuendelea kuchangia. Huwezi kupanda leo na kuvuna kabla ya mazao kukomaa au msimu wa mavuno kufika. KUJITOA KWENYE MAFAO NI SAWA NA MKULIMA KULA MBEGU.

6. Unapostaafu au kwa sababu yoyote unapolazimika kuhifadhiwa na jamii kwa kupewa kinga una uwezo wa kutumia zaidi ya ulichochangia. Hifadhi ya jamii hutoa kinga kwa kadiri ya uhitaji na si kwa kadiri ya mchango pekee. Hii inatokana na uwekezaji unaofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa upande mmoja na muendelezo wa mitiririko ya michango kwa wale ambao bado wako katika umri wa kuchangia. Mafao yako wewe baada ya kuchukua kiinua mgongo yataendelea kulipwa na wale ambao bado wanachangia. Hivyo, kuruhusu watu kujitoa ni kumomonyoa nguzo ya Hifadhi ya Jamii ya vijana na wanaojiweza kuwafaa wazee na wasiojiweza. Ndivyo ilivyo duniani kote.

7.Skimu za Hifadhi ya Jamii tofauti na iliyokuwa skimu ya mifuko ya Akiba ya Wafanyakazi inapaswa kugusa wananchi wote kwa kuwa ni haki ya kikatiba na si wafanyakazi pekee. Inapaswa kugusa wasiojiweza,wasio na ajira, waliojiajiri,wakulima, wanamichezo na wengine walioko kwenye sekta isiyo rasmi. Tuendako kila mtanzania anapaswa kuwa mwanachama wa hifadhi ya jamii kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea ambako namba yako ya uanachama wa hifadhi ya jamii ndio kitambulisho chako kikuu. Hivyo hoja ya kujitoa katika mfuko ulipwe ukajiajiri haijitoshelezi. Huko tuendako hata ukijiajiri hatimaye itakuwa ni lazima uchangie hifadhi ya jamii kama ilivyo lazima sasa kulipa kodi alimradi una kipato kiwe cha kuajiriwa au kujiajiri. Kujiunga katika hifadhi ya jamii kwa wasio waajiriwa katika sekta rasmi ni hiyari tu kwa sasa katika kipindi cha mpito.

8. Tanzania imeingia katika skimu hii mwanzoni mwa miaka ya 2000 tulipobadilisha mifuko iliyokuwapo. Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi (NPF) ukawa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na uliokuwa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) ukabadilika kutoka kuwa mfuko wa Mashirika ya Umma tu na kuwa mfuko wa kila mtu, na Serikali kuunda PSPF, LAPF nk. Sisi Tanzania ndio tumeianza safari ya kuelekea kwenye hifadhi ya jamii na bado hatujafikia huko. Katika muda mfupi manufaa yameanza kuonekana kadri uwezo wa mifuko unavyoongezeka na kupata faida. Leo tuna bima ya afya, fao la ulemavu kazini, fao la kujifungua, fao la elimu, fao la afya vijijini nk. Huko tuendako, mafao haya yatafanana katika mifuko yote na upo uwezekano wa mifuko yote ya sasa kuunganishwa na kuwa mmoja. Hatuwezi kufika huko ikiwa wanachama wataruhusiwa kujitoa kila wanapojisikia kufanya hivyo maana itaathiri uimara wa mifuko.

9. Kama ilivyo kanuni ya msingi kwa sheria yoyote, katika kila sheria lazima kuwepo na mazingatio (exceptions). Zipo aina ya sekta au kazi ambazo kwa mazingira yake ya asili ya shuruba zake hakuna mfanyakazi anayeweza kuhimili kuwa na uwezo wa kufanya kazi hizo hadi miaka 55. Aina hizi za kazi humfanya mfanyakazi apoteze uwezo wake wa kufanya kazi na kuchangia kutokana na sababu za kiafya (na)au ulemavu. Lazima sheria itambue watu wa aina hii na kazi za aina hii ili kuwawezesha hawa kuanza kunufaika na hifadhi ya jamii kabla ya umri wa kisheria uliowekwa wa kuchangia kwa miaka 15 au kupata mafao ya kiinua mgongo kabla ya miaka 55 kwa hiyari na 60 kwa lazima. Hawa wanahitajika kuwekewa FAO lao (si kujitoa) mahsusi la kuwahifadhi, kuwasitiri na kuwakinga dhidi ya kudhalilika na kufadhaika katika jamii. Hawa wanahitaji hifadhi. Mjadala wetu wafaa kuelekezwa hapo tunapojadili kuhusu marekebisho ya Sheria. Pia tujadili pendekezo la fao la kukosa ajira na ikiwezekana kama tunaweza kutumia michango yetu kama dhamana kukopea nyumba, kujisomesha nk na si kujitoa. Tusipoteze lengo kwa kile alichokisema Mwl. Nyerere, 'Tukipoteza muda mwingi kugawana KIBABA tutapoteza wasaa wa kugawana PISHI'.

10. Mimi na wewe hatuiujui kesho yetu wala hatuna uhakika wa msaada wa ndugu zetu na rafiki zetu pale tutakapofikwa na uzee au janga. Hifadhi ya Jamii ndio mbeleko yetu ya kujishikizia. Mimi na wewe na wengi wetu ambao ndio wafanyakazi wengi wa Tanzania ambao hatujachangia mifuko kwa zaidi ya miaka 15 kuweza kustahili mafao ya pensheni tuna maslahi gani na kujitoa kwenye mafao? Hao viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wanaotutia hamasa mbona wote umri wao umeshakwenda na wamekaa mkao wa kufaidika na pensheni? Tukumbuke Ujana Ukuta na Fainali Uzeeni.

Inawezekana kabisa sijatoa majawabu na ieleweke haikuwa lengo langu. Lengo langu ni kuchokoza tu mjadala. Tujadili.

Ndugu Kibaja Kariongo ni mdau wa harakati za wafanyakazi
SINA CHA KUONGEZA ILA KWA AKILI ZA WANAHARAKATI WAKIONGOZWA NA EXTREMIST LAWYERS KAMA LISSU NA KIBATALA WENGI WETU TUMESHAJITOA UFAHAMU
 
Kwa maelezo yako hifadhi ya jamii ni kwa baadhi ya wanajamii yaani watumishi katika sekta rasmi na sio kwa jamii nzima.

Tuachane na hayo; inakuwaje waheshimiwa wabunge wanapewa chao soon baada ya miaka mitano? Au wao hifadhi baada ya 55/60 haiwahusu? Tatizo ni kutokuwepo level ground kwa wote badala yake inakuwa case by case which sometimes seems to be unfair.
 
Mifuko yetu ya Hifadhi ya Jamii haina faida kwa wastaafu, haiangalii value of money, wanalipa wastaafu wanachotaka wao.

Haiingii akilini mtu amechangia kuanzia 1968 halafu ifikapo muda wa kustaafu 2002 akiba inasomeka kwa kiwango ulichochangia, WIZI mtupu.

Vv
 
kama mifuko iliweza kujiendesha kwa utaratibu mzuri tu na kukua kwa kasi hakuna sababu ya kuibua mizozo na wafanyakazi nchini pamoja na wachangiaji wengine. utaratibu wa kuwalipa mafao wale wote pale wanapojitoa mara baada ya kuachishwa kazi,au kupunguzwa kama sheria inavyotaka uendelee kama ulivyokuwa. upande wa timu ya serikali bado ziko changamoto za kuja na njia nyingine nyingi kuongeza mapato ya serikali. mawazo ya kutegemea kukopa fedha za mifuko yasiwe msingi wa kujipatia mikopo nafuu.
 
Kama kweli wanataka kufuta fao la kujitoa na kuanzisha fao la kukosa ajira, na kama kweli wanafanya hivi kwa manufaa ya wafanyakazi basi pendekezo langu hilo fao la kukosa ajira liwe ni 75% ya mshahara wa huyo aliyeacha kazi au kuachishwa kazi au mikataba wake kuisha, na alipwe hivyo mpaka pesa yake aliyochangia itakapoisha au atakapopata ajira nyingine
Hii iwahusu na wale waliyoacha kazi kwa hiyari yao kwa sababu hakuna anayeacha kazi bila ya kuwa na sababu za msingi. Hata yule anayeenda kujiajiri anahitaji muda wa kujipanga ili biashara yake iende vizuri, na mwisho wa siku hiyo pesa ni yake na siyo msaada anaopata kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii.
Serikali tafuteni vyanzo vingine vya pesa kwa ajili ya maendeleo acheni kumdhulumu pesa za wafanyakazi kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii. Munachukua pesa kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwekeza kwenye Mirada ya muda mrefu, matokeo yake mifuko hinakosa pesa mwisho munakuja na miswada yenye kusudio la kumdhulumu pesa za wafanyakazi kwa kisingizio cha hifadhi ya jamii. Acheni huu utapeli mara moja.
 
The case well presented..,I have seen the response.

Ingawa nakubaliana na baadhi ya hoja na michango lakini sehemu kubwa ya wachangiaji wamejielekeza kwenye uchama na hata kujaribu kumjadili mtoa mada...hawa hawakuwa na nafasi, mjadala huu haukuwa sehemu yao.

By the way, at least naendelea kuwaelewa watu tunaopaswa kuwaongoza.

Mimi nikiandika hoja yeyote kwenye jukwaa hili najiandaa kwa namna zote za response...mtoa mada naona ameshindwa kuja kujadili kwa namna response zilivyoelekezwa kwake na chama chake na kuwa personal attacks badala ya hoja...hii ndio JF ninayoijua.
 
Back
Top Bottom