Kujitambulisha walimu wapya

Kujitambulisha walimu wapya

nakusubiri huku tule bata...... vipindi hamna wanafunzi wachache yaaani full raha ila usiwe umesomea sayansi iyo itakula kwako hasahasa somo la hesabu... kuna jamaa hapa tumempa mkokoteni wa kubebea vitabu maana anafundisha shule nzima.

Mimi ni mwalimu wa GK wait nije kijijini then bata ziendeleeeeeeee.

Yani kama najiona vileeee
 
Doh unafaa sana chichi, so unatufanya tutabasam na kusahau vikwazo tunavyokutana navyo kazn
 
na mbwembwe zote hizi unaweza usipangwe .uliza Wa mwaka jana ilikuwaje
 
Haya majina ya jf yananifuahishaga sana MTU ana ID,ikisimama panda,nyani ngabu,kashaijabutege,omujumbajumba gwa kagologolo nk,ni hatareeee
 
SERIKALI imesema ajira za walimu wapya
zitaanza rasmi Mei Mosi, mwaka huu huku
ikiweka wazi kuwa walimu hao wasitegemee
kupangiwa katika maeneo ya majiji,
manispaa na miji.
Walimu hao wametakiwa kutotegemea
kupangiwa katika maeneo hayo kutokana na
idadi ya walimu waliopo ni kubwa na inakidhi
mahitaji, huku maeneo yaliyopewa
kipaumbele ni vijijini na halmashauri ambazo
zina mahitaji na upungufu mkubwa wa
walimu.
Idadi ya walimu wapya watakaoanza ajira
zao mwezi ujao ni 31,056 ambapo kwa
walimu wa ngazi ya Cheti ni 11,795,
Stashahada (Diploma) 6,596 na wenye
Shahada (Degree) 12,665.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
ajira mpya za walimu kwa mwaka
2014/2015.
Alisema kwa mwaka huu ajira hizo
zimechelewa kutokana na TAMISEMI pamoja
na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kufanya ufuatiliaji wa kina hadi katika ngazi
ya shule ili kubaini kwa uhakika mahitaji
halisi ya walimu kwa kila halmahauri na
shule.
“Ufuatiliaji huo umebaini kuwepo kwa
halmashauri na shule hasa za mjini zenye
walimu wa ziada na zingine hasa za vijijini
zina upungufu mkubwa wa walimu,” alisema
Sagini.
Alisema taarifa hizo zimesaidia kuwapanga
walimu wapya kwa usawa ili kuondoa
uwiano usioridhisha kwenye maeneo mengi
ya vijijini. Alisema kwa sasa wanakamilisha
taratibu za kupata kibali kwa ajili ya ajira za
walimu na fedha za kuwalipa stahili zao ili
waanze ajira zao rasmi mwezi ujao.
Aidha, alisema orodha ya walimu na vituo
watakavyopangiwa vitawekwa katika tovuti
ya Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ambayo
ni www.pmoralg.com na ya Wizara ya Elimu
www.moe. go.tz ifikapo Aprili 24, mwaka
huu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa
TAMISEMI, Zuberi Samataba alisema, pia
ufuatiliaji huo ulikuwa ni kuhakikisha
wanakuwa na taarifa sahihi za walimu
wanaoajiri wote ni wapya ambao
hawajawahi kuajiriwa ili kuepuka usumbufu
kwa walimu ambao hawatoi taarifa.
Alisema baadhi ya walimu ambao
wameshaajiriwa wanapoenda kusoma,
hupangiwa upya vituo na hawatoi taarifa
hivyo kuleta usumbufu wa kuchelewa
kutopata mishahara yao.
“Kuna baadhi ya walimu wameshaajiriwa
kwa hiyo jina linapoingizwa katika taratibu
za malipo, linagoma kuingia ndipo ukifuatilia
unajua alikuwa ameajiriwa, inabidi
umwambie arudi kwa mwajiri wake.
Kwa hiyo kwa hawa walimu wapya
nawashauri waende kuripoti katika vituo
walivyopangiwa na wakubali kufanya kazi
katika maeneo hayo, sio waripoti halafu
waondoke,” alisema.
 
Cc makamanda 2lio shiba doso hatuokopi, tope , wachawi wala vijiji vya ndani au vya nje hapo ni mwendo wa GUZMACH,range,kukroo, na wepesi wa combat karate..AAAAACH !
Hi kwenu nyote bila kumsahau mwenyekiti we2 chichimizi na chapchap ac..0712860468 naachia line.
 
Cc makamanda 2lio shiba doso hatuokopi, tope , wachawi wala vijiji vya ndani au vya nje hapo ni mwendo wa GUZMACH,range,kukroo, na wepesi wa combat karate..AAAAACH !
Hi kwenu nyote bila kumsahau mwenyekiti we2 chichimizi na chapchap ac..0712860468 naachia line.

Afande umeivaaaaaa
 
Afande umeivaaaaaa..kama kawa jomba nasikia j.mosi 25 ndo kinanuka bac kama itakua hivo..2naomba post hizo zing'ae na hapa jf.
 
Hongera Sana Kaka! Kunawa2 Wenye Akili Finyu Wa2miao Matako Kufikili Badala Ya Kichwa! Walikuwa Wamefurahi Sana Baada Ya Kusikia NO AJIRA!
Lakini Ukweli Ni Kwamba M2 Aliyesomea Ualim Hata Siku1 Hawezi Kosa Ajira Labda Ajila Itacheleweshwa2
 
"My name is Sir Chichi, I will be with you in English and History. I need your cooperation, thenk yuu
pwaa pwaaaaa." (makofi)

Najua ndo nakoelekea huko! usinishangae!! sijapenda kuanza mazoezi ya kujitambulisha ila ni kwa sababu ya kumbukumbu nilizonazo kuhusu msoto nilioupitia.

Ndiyo ni msoto believe me, ukiachana na jinsi nilivosoma shule kwa mbinde kingine ni hii miezi miwili iliyopita imenitesa mpaka sina hamu. We fikiria tu kuwa najifurahisha lakini nakwambia usithubutu kukutana na Bwana tetesi 'No Ajira' au kitu ajira july...weee kichwa kinavurugwa unaweza jikuta una msalimu shikamoo hata mtoto wa miaka minne na nusu.

Hiyo miezi iliyopita habari za redioni, magazetini au kwenye tv hazikua habari kwangu mpaka wagusie suala la ajira za ualimu.

Nasikia hapo katikati kuna issue za kitaifa kama katiba pendekezwa na suala la mb8 zilijitokeza,! hahahaaa nilikua nazipata lakini ndo nimezielewa juzi mara baada ya kauli ya ajira za wapiganaji wa taifa hili walimu.

Miezi hiyo miwili yan february na Mr March ndiyo iliyofanya hata wale walochaguaga Ilala na Moro Manispaa waseme mbele ya haraiki kuwa mi hata wakinitupa kijijini naenda tena kiroho safi kabisa! duu laiti kama tamisemi wangekua wanajua au kumpitia kila mwl tarajali ndani ya huo mda kupata maoni nadhan ajira zingetoka kama zawadi ya pasaka kwa wapiganaji.

Anyway ngoja tuache hayo na kutumia mda huu mfupi kuombea yafuatayo;

Walimu wote wapate ajira na pia waliokuwa na matatizo kama carry nao wawemo kwenye list hiyo kama inavokuaga miaka mingine.

Kingine ni uzima, afya na kudumishwa kwa ushirikiano baina yetu na jamii kwa ujumla.

Mwisho nawatakia kila la kheri wote watakaohusika kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha tunafikia ile adhma yetu ya kuajiriwa mfano atakayeweka majina yetu kwenye web ili asiipoteze flash yake yenye majina, watangazaji wote watakaoitangaza hii habari, pia mitandao na Mb8 zao siku hiyo kusiwe na shida ya mtandao bora mtandao usumbue leo mana nimetingwa hapa naandaa TO DO LIST cjui nimesahau nini cha muhimu:

Tar 17-18 kufua nguo na kukusanya madeni

Tar 19 - kuulizia bei ya mahitaji muhimu kama godoro na power bank ya kuchajia simu kule kijijini

Tar 20 - 23 kusalimia ndugu na kupanga nguo kwenye begi

Tar 24 asubuhi kuunga vifurushi kwenye line zangu 2, line moja dkk za kuongea nyingine internet

Tar 25 kufuata cheti chuo

Tar 28 kuaga ndugu na kukata tiketi

Tar 29 kutembelea ofisi za mkurugenzi

Duuh utata utaanzia siku nikifika huko site cjui nitaanzia wapi mana cna hata kijiko cha kuanzia ila all in all mambo yatajipa in the name of Jesus Christ, amen.

Walimu wenzangu wish u all da beste

Yaan nimejikuta nasoma uzi wako ad mwisho thou mrefu nami mvivu. Jaman frankly umeniua kwa kucheka. Yaan nimechekaaa. Hasa hapo "to do list" na pale kwenye utambulisho. .hahaa.. jaman my jioni!
 
Yaan nimejikuta nasoma uzi wako ad mwisho thou mrefu nami mvivu. Jaman frankly umeniua kwa kucheka. Yaan nimechekaaa. Hasa hapo "to do list" na pale kwenye utambulisho. .hahaa.. jaman my jioni!

Hahahaaa usihofu ndugu tuko pamoja
 
Back
Top Bottom