Kujitambulisha walimu wapya

Kujitambulisha walimu wapya

chichimizi

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
1,074
Reaction score
339
"My name is Sir Chichi, I will be with you in English and History. I need your cooperation, thenk yuu
pwaa pwaaaaa." (makofi)

Najua ndo nakoelekea huko! usinishangae!! sijapenda kuanza mazoezi ya kujitambulisha ila ni kwa sababu ya kumbukumbu nilizonazo kuhusu msoto nilioupitia.

Ndiyo ni msoto believe me, ukiachana na jinsi nilivosoma shule kwa mbinde kingine ni hii miezi miwili iliyopita imenitesa mpaka sina hamu. We fikiria tu kuwa najifurahisha lakini nakwambia usithubutu kukutana na Bwana tetesi 'No Ajira' au kitu ajira july...weee kichwa kinavurugwa unaweza jikuta una msalimu shikamoo hata mtoto wa miaka minne na nusu.

Hiyo miezi iliyopita habari za redioni, magazetini au kwenye tv hazikua habari kwangu mpaka wagusie suala la ajira za ualimu.

Nasikia hapo katikati kuna issue za kitaifa kama katiba pendekezwa na suala la mb8 zilijitokeza,! hahahaaa nilikua nazipata lakini ndo nimezielewa juzi mara baada ya kauli ya ajira za wapiganaji wa taifa hili walimu.

Miezi hiyo miwili yan february na Mr March ndiyo iliyofanya hata wale walochaguaga Ilala na Moro Manispaa waseme mbele ya haraiki kuwa mi hata wakinitupa kijijini naenda tena kiroho safi kabisa! duu laiti kama tamisemi wangekua wanajua au kumpitia kila mwl tarajali ndani ya huo mda kupata maoni nadhan ajira zingetoka kama zawadi ya pasaka kwa wapiganaji.

Anyway ngoja tuache hayo na kutumia mda huu mfupi kuombea yafuatayo;

Walimu wote wapate ajira na pia waliokuwa na matatizo kama carry nao wawemo kwenye list hiyo kama inavokuaga miaka mingine.

Kingine ni uzima, afya na kudumishwa kwa ushirikiano baina yetu na jamii kwa ujumla.

Mwisho nawatakia kila la kheri wote watakaohusika kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha tunafikia ile adhma yetu ya kuajiriwa mfano atakayeweka majina yetu kwenye web ili asiipoteze flash yake yenye majina, watangazaji wote watakaoitangaza hii habari, pia mitandao na Mb8 zao siku hiyo kusiwe na shida ya mtandao bora mtandao usumbue leo mana nimetingwa hapa naandaa TO DO LIST cjui nimesahau nini cha muhimu:

Tar 17-18 kufua nguo na kukusanya madeni

Tar 19 - kuulizia bei ya mahitaji muhimu kama godoro na power bank ya kuchajia simu kule kijijini

Tar 20 - 23 kusalimia ndugu na kupanga nguo kwenye begi

Tar 24 asubuhi kuunga vifurushi kwenye line zangu 2, line moja dkk za kuongea nyingine internet

Tar 25 kufuata cheti chuo

Tar 28 kuaga ndugu na kukata tiketi

Tar 29 kutembelea ofisi za mkurugenzi

Duuh utata utaanzia siku nikifika huko site cjui nitaanzia wapi mana cna hata kijiko cha kuanzia ila all in all mambo yatajipa in the name of Jesus Christ, amen.

Walimu wenzangu wish u all da beste
 
bajeti ya kununua solar electricity equipments umesahau bwana
 
Hii ndo post ambayo nimesoma huku nikitabasamu mwanzo hadi mwisho... Chichi na walimu tarajali wengi nawatakia kila la kheri
 
Hii nayo tetesi jamaa kaamua kutoa ya moyoni kila la heri endapo utapata hiyo chance
 
Kama nakuona vile Mwalimu chichimizi, kila la Heri mkuu huko Kazulamimba utakapopangiwa.

attachment.php
 

Attachments

  • mojawapo-ya-darasa-shule-ya-msingi-selous-Darasa-la-sita-Namtumbo.jpg
    mojawapo-ya-darasa-shule-ya-msingi-selous-Darasa-la-sita-Namtumbo.jpg
    45.6 KB · Views: 2,765
Je jina lako una uhakika limo mkuu chichimizi!!!!!! hebu ngoja nikuombee maana ukiikosa mhhh!!!!!
 
Jamani jf kuna vipuri. Ningekuwa na uwezo ningechora picha nilizokuwa naziona za mwalimu chichimizi. Post hii imenichekesha hadi nimepaliwa na mate. Viva jf
 
MAJIBU.....
Nitafurahi mkifuata ushauri wangu. Fungua ac NMB bank branch iwe jirani na
halmashauri/ manisipaa ulikopangiwa, hii itakusaidia endapo kutatokea tatzo kwenye
mshahara wako inakua rahsi kuprocess na mara nyingi ikitokea tatzo unaambiwa kalete bank statement ama nenda kaulize benki hivo kama ipo
jirani na ofisi ya halmashhauri ako inakua simple
kusolvika haraka.

lingine mishahara nmb inawahi 4 days before other banks
lingine ukipewa pesa ya kujikimu ni rahsi cheque kua procesed mapema within a day hii inatokanna na cheque hyo kua from nmb to nmb...but kama unapeleka other banks na upo ktk mkoa ambao BOT haipo cheque hyo itachukua more than 8days.

lingine mikopo na interest rate zao ni simple na ndogo respectvelly .
Kumbuka kufungua CHAPCHAP ac kwani ina zero charges na kufungua ni ndani ya nusu saa unakua na atm yako.

Pia kama una ac in other banks bado utalipwa stahki zako zote but utapata changamoto hzo hapo juu.

Ikitokea unataka kubadlisha ac inawezekana pia but inahakikisha umemtarifu hr wa LAWSON
 
ndio mwl chichimizi inshort have got u......our problem was about employment........thnk it was a great crying ....until our parents thought that we ar failed examz...nichukue muda huu kumshukur sana aliee sikia kilio chetu KATIBU MKUU -TAMISEM...shukuran za dhati kwake mziki kuripot
 
nakusubiri huku tule bata...... vipindi hamna wanafunzi wachache yaaani full raha ila usiwe umesomea sayansi iyo itakula kwako hasahasa somo la hesabu... kuna jamaa hapa tumempa mkokoteni wa kubebea vitabu maana anafundisha shule nzima.
 
Back
Top Bottom