Kujishaua mbele za wanaume misibani..

promiseme

JF-Expert Member
Mar 15, 2010
2,708
926
Habari za hasubuhi waungwana,

Jana nilienda msibani huko magondo poromoka, nikiwa na shogha yangu cha ajabu shoga hatulii sehemu moja mara katoka nje mara kaingia ndani nikamuliza kwani vp mbona unawasiwasi kuna nini? Akanijibu hujui kama hapa ndio mpango mzima wanaume wengi hupatikana msibani, lazima nipate kichwa hapa. Nilishangaa nikajiuliza hivi inakuwaje mtu unakwenda msibani halafu akili yako inafikiri mambo machafu.

Kwakweli alinikera na sikurudi nae tuliachana hapo na yy. Msiba haumuhusu ni mke wa shemeji yangu. Hivi wangwana wako watu wanaofanya haya mambo au ni huyu mdada peke yake? Manake sijawahi kuona kiumbe mwenye visa kama hivi...
 
Jiwe Linaloishi

JF-Expert Member
May 24, 2008
3,736
2,135
ni rafiki wako wa kufikia au?? manake kama ni rafiki wa ukweli ungekuwa unajua tabia zake...
 
prianka

JF-Expert Member
Aug 29, 2012
684
168
alikua anatafuta wana wanaume kwa nguvu sasa akakuta soko lenyewe limefiliska loo
 
Tized

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
4,023
5,897
Kile kiapo cha ndoa huwa ni kirahisi sana kuapa au ni kigumu sana kueleweka au ni kirahisi sana kusahaulika? Ni kwamba tamaa za miili yetu tumezipa kipaumbele kuliko hata uthamani wetu na future yetu? Au tunaishi tu ilimradi kukuche kesho? kwamba ukifa leo na ukifa after 30 years haina tofauti kwako???? Mwambie shemejio ajiheshimu na aiheshimu ndoa yake. Mwili huwa haushibi kamwe.
 
Nivea

JF-Expert Member
May 21, 2012
7,458
4,717
huo ndio mpngo mzima wa mujiniiii!!jana nilihudhuria misiba miwili kulikuwa na dada mja mithili hiyo hiyo anajichekesha amevaa sidiria tu na vimikanda vya maji vinaonekana yeye hatulii nikupita pita akaenda kusimama kule kwa wanaume mara akimbie pembeni akicheka huku akipikea simu sikuelew ila nilichukia sana maana nilikuwa na huzuni sana tulikuwa tunazika mtu mzima na mtoto wa miezi 4.kwa upande wangu naona ndio mishe zenyewe ndugu ,angalia wanawake wa siku hizi wanavyojikoki kwenye misiba anaulamba wala hafuniki kichwa tena lol.nahisi ndio mpango wa mujini ndugu lol mkuu promiseme
 
Last edited by a moderator:

Niaibu mwanamke kujishaua mara unaongea na cm mara kulia kwa kwikwi yani full vituko...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom