Kujiamini sana ndiko kulikomponza yuda eskariote aitwe msaliti hadi hii leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujiamini sana ndiko kulikomponza yuda eskariote aitwe msaliti hadi hii leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ebaeban, Jul 14, 2012.

 1. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Samahani wana JF sikujitambulisha mimi ni myahudi naittwa EBA na baba ni pure myahudi anaitwa EBAN , mama ni mgogo wa kijiji cha Sejeli Kongwa.


  Mheshiwa NDUGAI mbunge wa Kongwa, naibu spika wa bunge la muungano (kiyahudi knisset) anajiamini kupita kiasi amekuwa overconfidence. Kujiamini sana ndiko kulikamponza Yusa Eskariote aitwe msaliti hadi leo. Injili zote nne (Yaohana,Marko,Yuda na Matayo) zinamwelezea Yuda kuwa alikuwa ni mfuasi wa Yesu (au Issa bin Marium) hivyo Yuda alikuwa yupo kila mahali Yesu anapokwenda, alikuwa anajionea mwenyewe kwa macho yake ile miujiza mikuu Nabii Yesu aliyokuwa anaifanya mfano kufufuwa waliokufa, kutakasa wakoma, vipofu kuona, viwete kutembea n.k. Sasa wale wayahudi walipomwendea wampe vincenti ili akawaonyeshe Yesu akakubali, kukubali kwake ukifikiri haraka utazani Yuda alikuwa na tama ya hela, siyo Yuda aliwashangaa wale wayahudi moyoni alisema hawa wanamfahamu Yesu au wanamsikia aliwakubalia akachukua zile hela akawaonyeshe Yesu maana kwa kujiamini kwake sana kama Mheshimiwa Ndugai anavyojiamini alijua watashindwa kumkata halafu awacheke na kisha awarudishie vincenti vyao. Maskini Yuda kitu amabcho hakujua ni kwamba ilibidi mtu afe ili neno litimie, matokeo yake Yesu alikamatwa na Yuda ni msaliti hadi leo.

  Mheshimiwa Ndugai amelewa madaraka , akikaa kwenye kiti anajiamini , anaona mbingu zimeshuka ndio maana bila kusita anawatoa wabunge inje , anawazodoa wapiga kura wao kwamba wamechagua kituko mfano wa aliowazodoa akiwa kwenye kiti cha enzi ni Mheshimiwa Padri Msigwa na wapiga kura wake wa Iringa mjini Mheshiwa Halima Mdee na wapiga kura wake, na hatimae Mheshimiwa Dr. Ndungulile na wapiga kura wake.

  Kama Yuda Eskariote kitu ambacho Mheshiwa Ndugai hakijui ni kwamba na sisi wapiga kura wake tunamchora na tunamchora kweli,anafikiri anatufurahisha ,kumbe angejuwa.

  Kwa wale mliokuwepo miaka ya sabini mtaikumbuka ile kashifa ya Watergate iliyoyokea Marekani enzi za utawala wa Richard Nixson . Mwaka 2005 kashifa kama hiyo ilitokea wilaya ya Kongwa, mwanzoni Mheshiwa Ndugai alipochaguliwa kuwa mbunge wa Kongwa kwa mala ya kwanza na kumtupa Shamsa Mwangunga kwenye kura za maoni (wengine mliuliza Mwangunga alikuwa Ubungo, siyo Ubungo kenda 2010) kulitikea sisi wanakongwa tunaita kashifa ya Jackson Samwel. Mapema katika safu yake ya uongozi Mheshimiwa Rais alimchagua jamaa moja anaitwa Jackson Samwel kuwa mkurugenzi wa halimashauri ya Kongwa na Dr Fatuma alikuwa ndio Mganga Mkuu wa wilaya akawa na uhawala na Mheshimiwa Ndugai hilo halina ubishi, pia walikuwepo wakuu wa idara wengine, si ndio likaibuka suala la mashirika ya kupamabana na Tracoma (vikope) kwisha mda wake na kutaka kurenew, pakawepo na suala la kuomba mlungula, mzungu mmoja akiitwa Jane Turner wa HKI kwa niaba ya wenzake akawatolea inje, mda si mrefu wakuu wa idara wote waliokuwepo wakati ule wakahamishwa kwa mpigo akiwepo na Dr, Fatuma halafu na Mkurugenzi Jackson Samwel akarudi ofisi ya waziri mkuu. Wakaanza kusema mkurugenzi katuchoma alikuwa spy, kumbe tulikuwa tunafanya kazi na shushu hivi na vile ndo kuitwa kashifa ya Jackson Samwel,. Sasa wale wakuu waliohamishwa chapuchapu ndio waliotowa siri kwamba kinara wa kudai mlungula kwa mashirika alikuwa ni Dr Fatuma wengine walilalamika hadharani kabisa kuwa wamekuwa victim of circumstance, wamehamishwa wakati mambo yao yalikuwa yameanza kunaga Dr. Fatuma kawaponza.

  Na nyuma ya pazia akitajwa Mheshimiwa Ndugai maana rushwa iliyoombwa ilikuwa ni kubwa, ni wazi wakati huo mheshimiwa alikuwa anahitaji sana hela maana alikuwa ametumia fedha nyingi sana kwenye kampeni na alikuwa ameishiwa na madili ya ubunge yalikuwa bado hayajaanza

  SASA CHAKUWAFUKUZA WENZIE KWENYE BUNGE HADI INJE YA GATE NI NINI?

  Naomba kuwasilisha

  Leo nimekuja kivingine juzi mlisema nimekuja na chupi nimetukana.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Ndugai ni janga la kitaifa hawa dawa yao ndogo sana!! 2015 harudi mjengoni huyu!
   
 3. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Yuda Iskariote unamlinganisha na Ndugai? Uyahudi wako una uzito gani ktk maelezo yako? A kind of illogical ordering!!!
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kuna haja ya kubadili kanuni ili spika na naibu wake watoke nje ya wabunge hata ikiwezekana wasiwe wanachama wa vyama vya siasa.
   
 5. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Nimemringanisha kutokana na kujiamini kwake kupita kiasi(overconfidence) kama huoni logic yoyote basi your brain is on your knee.
   
 6. D

  Deofm JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni vigumu sana kushinda nguvu za asili ya Nigeria. Piga ua kurudi atarudi tu, hakuna mwenye uwezo wa kumzuia pale kongwa.
   
 7. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,291
  Likes Received: 1,214
  Trophy Points: 280
  Nguvu ya asili ya kinaigeria!?
   
 8. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  NI KWELI Nigeria, jamaa huwa anaenda mara kwa mara huko "i think" ili mambo yake yakae sawa. Huyu jamaa ukibahatika kukaa naye kwenye maongezi yake huwa anamfagilia sana EL, nadhani pengine ni kwakuwa huwa kwenye hizo safari zake za Nigeria huwa yupo na EL, na wanachokwenda fanya huko ndicho wanachokiamini na pengine ndo sababu ya jeuri/kiburi/dharau afanyazo Mjengoni pengine kupima nguvu ya KINGA hiyo.

   
 9. D

  Deofm JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  unashangaa nini? uliza wenyeji wa Kongwa watakujuza mengi, wataalamu kutoka huko huwa wanakuja na ku-pause hapo kwenye ka-mji kadogo, ohoo!!
   
 10. t

  tubadilike-sasa JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 677
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  Kuana kitu anataka kusema lakini ameshindwa tu namna ya kuchagua topiki na kupanga alichotaka kusema
   
Loading...