Kujenga maisha nayoyatamani

Kujenga maisha nayoyatamani

2v2

Senior Member
Joined
May 7, 2025
Posts
168
Reaction score
238
Leo nimeamua kuanza kuandika mawazo yangu kuhusu safari ya kujenga maisha ninayotamani.

Sina uhakika nitafika mbali kiasi gani, lakini najua jambo moja: miaka ijayo nataka niweze kurudi hapa na kuona nilikotoka.

Ninajifunza biashara, teknolojia, kilimo na namna ya kujenga vyanzo vya mapato vinavyoweza kudumu kwa muda mrefu.

Kila hatua nitakayopiga, kila kosa nitakalofanya na kila somo nitakalojifunza nitajaribu kushirikisha hapa. Lakini si kila kitu nitakiandika hapa.

Labda nitawahamasisha wengine.
Labda nitajihamasisha mwenyewe.
 
Hongera mkuu..

Kuwa updated muda wote

Kuwa unique

Pendelea kuandika andika ulipofikia na na wapi na namna gani ufike zaidi

Usiwe over excited au mfadhaiko
Katika maamuzi ya plan, tulia relax

Achana kutafuta hamasa humu, kuna mazombi yaliofeli maisha.
 
Hongera mkuu..

Kuwa updated muda wote

Kuwa unique

Pendelea kuandika andika ulipofikia na na wapi na namna gani ufike zaidi

Usiwe over excited au mfadhaiko
Katika maamuzi ya plan, tulia relax

Achana kutafuta hamasa humu, kuna mazombi yaliofeli maisha.
Sawa mkuu
Hongera mkuu..

Kuwa updated muda wote

Kuwa unique

Pendelea kuandika andika ulipofikia na na wapi na namna gani ufike zaidi

Usiwe over excited au mfadhaiko
Katika maamuzi ya plan, tulia relax

Achana kutafuta hamasa humu, kuna mazombi yaliofeli maisha.
Sawa mkuu
 
Je uhitaji wako katika maisha hukuweka katika hali gani?.

Siku baada siku zimepita, ni wiki kadhaa zimeisha, kama si 2 basi 3 zimepita, mambo nilivyotarajia hayajatimia, hivyo basi moyo wangu ukaugua, akili yangu ikanipa ufahamu, nikakumbuka Mithali 13:12 Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima., ubongo ukanikumbusha kuwa uone michongo inapofeli, huyo ni dizasta vina katika wimbo wa karibu duniani.

Katika wiki, moja ya siku, jana yake nilitafutwa nikawa sipatikani, maana nilitalajia kuanzima pesa hivyo sikuwa na bahati, uaminifu, ukweli, upole bado havina nafasi, vipi kukopa kukopeshwa kwako vina nafasi, moyo huugua unapokosa hitaji, nagundua moyo haupo katika nafasi, rejea katika kitabu cha mathayo 13:7-9-22... Mathayo 13:7, 9, 22
7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;

9 Mwenye masikio na asikie.

22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.

pia rejea katika mathayo 9:13...Mathayo 9:13 Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Masaa yakasonga hatimaye nuru ikatoka azimio nikatimiza, miminiko la furaha likamwagika, ni nini hiko basi, ni> freezer, pesa nilizotarajiwa kuanzimwa nikapata, asante ni wakati wa kuzirudisha sasa.

Kuna kitu nimejifunza katika safari hii ya kununua freezer, maana nilikuwa nalipia kidogo kidogo, lakini nilijijenga kimchakato wa kifedha hatua hiyo ilinipa utayari wa kwenda kuanza kulipia kidogo kidogo hadi kumaliza. hata kama nimeanzima pesa basi ni kiasi kidogo ambacho naweza kulipa ndani ya muda mfupi.

Moja ya malengo yangu ya mwaka huu yalikuwa ni kuwa na freezer, kwa maana naona linakwenda kuongeza kipato changu na kupiga hatua nyingine ya kimaisha.
 
Nikiwa mdogo, baba yangu aliweza kununua pikipiki na hata gari.

Lakini mara nyingi sikupenda kufikishwa shule kwa usafiri. Sikupenda kujiona au kuonekana tofauti sana na wenzangu.

Kadri ninavyokua, nimegundua kuwa sipingi mafanikio. Ninayapenda na ninayatafuta kwa juhudi zangu mwenyewe.

Tofauti ni kwamba napenda mafanikio yawe sehemu ya maisha, si maisha yote. Napenda maendeleo yanayoambatana na unyenyekevu na maisha ya kawaida.

Je, mafanikio yana thamani gani kama yanatufanya tusahau kuwa watu wa kawaida?
 
Mkuu. Natamani nikuone TU kwenye Forbes List. Kuja kuandika humu mapito yako haisaidii. The end justify the Means.
 
Leo nimejifunza somo muhimu kutoka kwenye mpira wa miguu. Timu bingwa haishindi kwa sababu imeshinda kila mechi. Inashinda kwa sababu imekusanya pointi za kutosha katika msimu mzima.

Maisha yanafanana na season ya ligi. Watu wengi hujilaumu wanapokutana na changamoto moja au wanaposhindwa kufikia lengo fulani kwa wakati waliotarajia. Lakini ukweli ni kwamba mafanikio si matokeo ya siku moja, wiki moja au mwezi mmoja. Ni matokeo ya maamuzi madogo yanayofanywa kwa muda mrefu.

Katika V12S 26/27 nimeamua kuangalia maisha kama season. Kila hatua ninayopiga ni pointi kwenye jedwali langu. Kujifunza jambo jipya, kuongeza mtaji, kuboresha biashara, kuendeleza kilimo au kusogea karibu na ndoto yangu ya teknolojia ni ushindi unaonikaribisha kwenye lengo la mwisho.

Sihitaji kushinda kila mechi. Ninahitaji kuendelea kukusanya pointi.

Mwisho wa season, kinachohesabika si mechi moja niliyopoteza, bali nafasi niliyomalizia kwenye jedwali la maisha yangu. 🚀 📖🌾👨🏾‍💻
 
Back
Top Bottom