NZURI PESA
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 5,958
- 2,967
Upo Dodoma Mjini eneo gani?Wadau habari za humu ,nina milion tatu na nusu dodoma mjini nahitaji kujenga chumba na sebule ,je itatosha
Upo Dodoma Mjini eneo gani?Wadau habari za humu ,nina milion tatu na nusu dodoma mjini nahitaji kujenga chumba na sebule ,je itatosha
Duh kwa mtindo huu nitajenga kweliKwanza hongera kwa kudhubutu
Kama unamaanisha chumba na sebule bila jiko, stoo wa Dining
Inawezekana
Hesabu itakua kama Ifuatavyo.
1.Utahitaji Tofali 700
Tumia tofali za Nchi 5
Kuzipata Tofali hizi
Nunua Cement Mifuko 18
=15,000x18=270,000
Nunua Mchani gari kubwa maarufu kama Mengi sh. 170,000
Baada ya hapo waie watu wakutengenezee Tofali
Bei yakufyatulia tofali mfuko mmoja ni sh. 4,000 (kwa Dodoma)
Kumbuka Kua mashine na vibao ni juu yao
So kwa mifuko yako 18x4,000 Itakua sh. 72,000
**Mpaka hapa umeshatumia jumla sh. 512,000
Sasa Tuendelee
Muite Fundi kisha Mkubaliane kuchimba msingi peke yake ambapo Makadilio ya Juu ni sh. 100,000 (Gharama hii ni pamoja na kumwaga mchanga kwenye msingi)
Baada ya hapo Anza Ujenzi ambapo Gharama ya Fundi kujenga Boma lote ni sh. 300,000
Utahitaji mchanga kwa ajili ya kujengea
Nunua gari kubwa sh. 170,000
Nunua cement yakujengea mifuko 16
=15,000x16=240,000
***Mpaka hapa utakua umetumia sh.
1,322,000
Tuendelee
Utakua unadaiwa nondo Za Linta pamoja na mkanda wa chini
Zinatakiwa nondo 10
=10x22,000=220,000
Inatakiwa zege nunua lakawaida tu sh. 100,000
Maji weka sh. 70,000
Ring na usafiri sh. 30,000
Mbao zakukodi kwa ajili ya Linta
Sh. 60,000
Mpaka hatua hii gharama zote ni sh.
1,802,000.
Tumeingia hatua yakupaua
Mbao za 4x2 Pc 25x9,000=225,000
Mbao za 2x2 Pc 30x4500=135,000
Misumali sh. 36,000
Fundi kupaua sh. 170,000
Bati 20x22,000=440,000
Misumali ya bati sh. 50,000
Waya wa Kenchi sh. 10,000
Mpaka hapa gharama zote ni sh.
2,868,000
Tunaendelea
Mlango wa mbao sh. 330,000
Madirisha manne sh. 400,000
Naomba kuwasilisha
Kwa Ushauri zaidi 0652 881 000/0684 239106
Nipo Dar es salaam.
Utajenga tu kikubwa Marengo.Duh kwa mtindo huu nitajenga kweli
Ushauri mzuri.Milango anunue used elf 60 mmoja
Huyo anakupiga kweli aiseDaah kumbe Fundi wangu anataka kunipiga eti anataka 1M kujenga msingi tu tena kiwanja chenyewe flat kabisa nyumba ya vyumba 3 sebule,study room jiko na dinning....
HahahahahahaInatosha na kubaki kiasi fulani. Bati bando 2 ( (6laki) Tofari 1000 (1m) , Mbao , cement na Mchanga lorry 2, hizo ni ziada ndogo . kwa uchumu wa 3m, jenga wewe mwenyewe achana na mafundi.
Acha tu dada,nilienda kununua jamaa akantajia hiyo bei nilichoka,sikuwa na jinsi.ilibidi tu nichukue.Mmh mambo yanazidi kubana.... Mfuko ulikuwaga elfu kumi na moja
Cement ya wazo,ya dangote huku adimu sana mzeeHuo mfuko ni wa Dangote au nani? Kwa kuwa unafanya kazi hapo nadhani ulinunua na Sukari kwa ajili ya maswala ya Chai ukaona hali ilivyo tete..
Anakupiga Mkuu. Mi nilipandisha vyumba viwili na sebule na vyoo viwili kwa 1.2 M hadi kozi mbili za juu. Ukitaka naweza kukunganisha na Fundi wanguDaah kumbe Fundi wangu anataka kunipiga eti anataka 1M kujenga msingi tu tena kiwanja chenyewe flat kabisa nyumba ya vyumba 3 sebule,study room jiko na dinning....
Kama hajaelewa na hapa basi akalime Kongwa hukoKwanza hongera kwa kudhubutu
Kama unamaanisha chumba na sebule bila jiko, stoo wa Dining
Inawezekana
Hesabu itakua kama Ifuatavyo.
1.Utahitaji Tofali 700
Tumia tofali za Nchi 5
Kuzipata Tofali hizi
Nunua Cement Mifuko 18
=15,000x18=270,000
Nunua Mchanga gari kubwa maarufu kama Mengi sh. 170,000
Baada ya hapo waite watu wakutengenezee Tofali
Bei yakufyatulia tofali mfuko mmoja ni sh. 4,000 (kwa Dodoma)
Kumbuka Kua mashine na vibao ni juu yao
So kwa mifuko yako 18x4,000 Itakua sh. 72,000
**Mpaka hapa umeshatumia jumla sh. 512,000
Sasa Tuendelee
Muite Fundi kisha Mkubaliane kuchimba msingi peke yake ambapo Makadilio ya Juu ni sh. 100,000 (Gharama hii ni pamoja na kumwaga mchanga kwenye msingi)
Baada ya hapo Anza Ujenzi ambapo Gharama ya Fundi kujenga Boma lote ni sh. 300,000
Utahitaji mchanga kwa ajili ya kujengea
Nunua gari kubwa sh. 170,000 (Mchanga plaster utabaki)
Nunua cement yakujengea mifuko 16
=15,000x16=240,000
***Mpaka hapa utakua umetumia sh.
1,322,000
Tuendelee
Utakua unadaiwa nondo Za Linta pamoja na mkanda wa chini
Zinatakiwa nondo 10
=10x22,000=220,000
Inatakiwa kokoto nunua zakawaida tu sh. 100,000
Maji weka sh. 70,000
Ring na usafiri sh. 40,000
Mbao zakukodi kwa ajili ya Linta
Sh. 50,000
Mpaka hatua hii gharama zote ni sh.
1,802,000.
Tumeingia hatua yakupaua
Mbao za 4x2 Pc 25x9,000=225,000
Mbao za 2x2 Pc 30x4500=135,000
Misumali sh. 36,000
Fundi kupaua sh. 170,000
Bati 20x22,000=440,000
Misumali ya bati sh. 50,000
Waya wa Kenchi sh. 10,000
Mpaka hapa gharama zote ni sh.
2,868,000
Tunaendelea
Mlango wa mbao sh. 300,000
Madirisha matatu sh. 300,000
Fundi kupiga plaster na floor sh. 150,000
Cement ya kupigia plaster & Floor mifuko 15x15,000=225,000
Mpaka hapa gharama zote ni 3,843,000.
Naomba kuwasilisha
Kwa Ushauri zaidi 0652 881 000/0684 239106
Nipo Dar es salaam.
heri yenu, sisi wa 20,000 tusemeje?Nimenunua mfuko wa cement Leo asubuhi 15000 acha tu
Duh,hatari sana hii aiseeheri yenu, sisi wa 20,000 tusemeje?
HahahahahahaInatosha kujenga mkuu... Lakini wakikuvamia majambazi usiku watakuuliza tukojelee nyumba ibomoke tuingie au utufungulie mwenyewe? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Usiseme haitoshi hauwezi jua labda alishanunua vyote hivyo akawa navyo ndiyo akabakiwa na hiyo pesa anataka kujua kama fundi akijenga atatumia yote hiyo 3 iliyobakiaHaitoshi Mkuu.
Tofali elfu 1=1,000,000
Cement 20. 300,000
Fundi. 600,000
Nondo
Mchanga
Kokoto
Mbao za kupaua
Bati
Nashindwa kuendelea ila jipange taratibu Mkuu.
Huwezi kumaliza ila jitahidi
Ili nyumba idumu chini lazima upige mkanda mkuu nyumba zangu zote napenda hivyo km ni mfinyanzi panachimbwa msingi unajazwa mchanga kwanza wanalaza tofari inchi 6 kama coz 2 km sijakosea inasukwa nondo inamwagwa zege ( mkanda) ndio inanyanyuka wakifika juu tena ktk linta wanamwaga tena mkanda hutaona nyufa za kijingaVipi tukipiga chini mkanda
Mwenzio anataka nyumba ya milion 3 mi ndo nampa option ya kupunguza gharama.,Ili nyumba idumu chini lazima upige mkanda mkuu nyumba zangu zote napenda hivyo km ni mfinyanzi panachimbwa msingi unajazwa mchanga kwanza wanalaza tofari inchi 6 kama coz 2 km sijakosea inasukwa nondo inamwagwa zege ( mkanda) ndio inanyanyuka wakifika juu tena ktk linta wanamwaga tena mkanda hutaona nyufa za kijinga
Hajasema anataka.Mwenzio anataka nyumba ya milion 3 mi ndo nampa option ya kupunguza gharama.,