kuitambua simu mahali ilipo kwa uwezo wa internet'''

kuitambua simu mahali ilipo kwa uwezo wa internet'''

Mr. Somebody

Member
Joined
Sep 12, 2013
Posts
76
Reaction score
24
ni application gani rahisi y KUUNGA SIMU KATIKA UTAFUTAJI WAKE KAMA IMEPOTEA AU IMEIBIWA??????:tonguez:
 
Ungetaja aina ya simu ingekuwa vizuri ili upewe jibu la moja kwa moja
 
Download netquin manager ina option ya kuset simu yako kuwa ikipotea utatumiwa sms yenye namba ya sim card iliyochomekwa.....hata ikibadilishwa mara nyingi bado utapokea ujumbe bila mwizi wako kujua.

Kama unatumia simu ya android download avg antivirus kisha utakuwa naoption ya anti theft pia.
 
Sasa kaka isack tatizo ni moja wezi wasiku hizi hawaweki line kwanza wanaenda kuziflash au wana format...Apo unasemaje mkuu?
 
Ikitokea simu ikawa flashed au kama mwizi wako ni mimi jambo la kwanza ni kuondoa program zote kwenye simu.
Wezi wengi huflash simu kwa lengo la kuziuza.
Ili mwizi asihangaike kuiflash simu yako usiweke password za aina yoyotebkwenye simu. Believe me njia rahisi ya kulinda simu yako ni kwa kutokuiwekea security....hapa mwizi hatakwa na sababu ya kuiflash.
 
hamna haja ya software major os zote sasa hv unaweza track simu yako online.

1.kama unatumia iphone au kifaa cha ios click link hii

What to do if your iOS device is lost or stolen

2. kama unatumia nokia au windows phone click link hii

How to Find your Lost or Stolen Windows Phone 8

3. kama una samsung au simu ya android click link hii

How to Locate Your Lost or Stolen Android Phone (and Wipe if Necessary)

maelezo yote yapo kwenye hizo links.

WARNING
watu wanatabia mambo yakishakua too late simu ikishaibiwa ndo wanaomba msaada. vitu hivi vya kudhibiti wizi au kupata simu iliopotea vinahitaji uwe umeshafanyia simu yako configuration.
 
Pia kuna njia nyingine za kujua simu yako ililo....
1. Google Latitude: ingia kwenye mtandao huu kisha ingiza imei namba kama watakavyokuelekeza......sekunde chache baadae kwa kutumia gps iliyo ndani ya simu watakuonesha simu yako ilipo hata kama imeflashiwa. hawa jamaa wanaweza kuitrack simu yoyote hata kama ni kanokia ka tochi.

2. icloud....kwa wale wenye iphone download na ujisajili humu.....mara tu simu yako itakapopotea, tumia simu ingine au kompyuta kuingia icloud. Kwa akaunti ya simu iliyopotea watakutumia sehemu simu yako ilipo. Tatizo ni kuwa mwizi wako akiweza kuidisable icloud simu inakuwa imepotea. Ila kama utamuwahi na ikawa ametoa line yako tayari utaweza kuifunga simu yako isitumike kabisa.

3. Plan B....kwa simu za android unaweza kudownload plan B hata baada ya simu yako ya android kupotea. Hii itakusaidia kwa kushirikiana na seva za plan B kugundua simu yako iko wapi na namba inayotumika baada ya kuibiwa.

4.IMEI number: kama unaijua imei number yako wasiliana na mtoa huduma yako wa simu. Hawa wanaweza kuitambua simu popote ilipo na inatumika kwenye mtandao gani. Ni njia rahisi zaidi. Mwaka 2012 niliibiwa simu na nikaenda ofisi za airtel nikiwa na imei namba na hakika niliweza kumpata mwizi wangu akiwa hotelini kama nilivyoelekezwa.

5. Uliza rafiki zako...wakati mwingine huenda baada ya kufurahia usiku kucha haukumbuki sehemu simu yako ilipo. Cha kufanya chukua simu ingine na upige namba yako. Inawezekana rafiki alikutunzia au inawezekana iko kwenye begi na utasikia mlio uliouzoea wa simu yako.

6. Tangaza zawadi.Kama namba 5 haikufanikiwa basi una hakika simu yako imepotea. Wakati mwingine wezi wanaiba simu kwa sababu ya njaa. Unajua wazi kuwa mwizi hawezi kula simu yako. Tangaza kutoa zawadi inayoendana na thamani ya simu yako. Kumbuka kupoteza simu unapoteza pia namba za mawasiliano, unapoteza pia file muhimu na pia picha zako za kumbukumbu au video. Unapotangaza zawadi kwa atakayerudisha simu yako muhakikishie hautachukua hatua za ziada kumuwajibisha.

Ukishindwa njia ya 6 nenda namba 1-4
 
hamna haja ya software major os zote sasa hv unaweza track simu yako online.

1.kama unatumia iphone au kifaa cha ios click link hii

What to do if your iOS device is lost or stolen

2. kama unatumia nokia au windows phone click link hii

How to Find your Lost or Stolen Windows Phone 8

3. kama una samsung au simu ya android click link hii

How to Locate Your Lost or Stolen Android Phone (and Wipe if Necessary)

maelezo yote yapo kwenye hizo links.

WARNING
watu wanatabia mambo yakishakua too late simu ikishaibiwa ndo wanaomba msaada. vitu hivi vya kudhibiti wizi au kupata simu iliopotea vinahitaji uwe umeshafanyia simu yako configuration.

CHief umenena vyema....ni vyema kuanza kuilinda simu yako mara unapoinunua tu. Kuna mitandao mingi online inayotoa huduma za kutrack simu ila pia lazima ujue imei yako na pia mara unapoipata simu uweze kuthibitisha ni ya kwako... hapa uwe na risiti yako kama itahitajika hususan polisi.
 
ni application gani rahisi y KUUNGA SIMU KATIKA UTAFUTAJI WAKE KAMA IMEPOTEA AU IMEIBIWA??????:tonguez:
kwa IOS 6 or earlier

kama simu yako ni iPhone weka 'Find My iPhone' app, link na icloud service alafu enable restrictions kupitia settings ya simu yako. ukiEnable restrictions utaweza kuRestrict unInstalation ya program yoyote kwenye simu yako, restriction ya kuSign out Apple ID yako au account yoyote, restriction ya kuzima locations service 'GPS', hivyo kama mtu akiiba simu na akafanikiwa kubadilisha line utaweza kuitrack, kuErase contents, kuiLock au kuifanya ipige alarm. hii yote utafanya kupitia icloud service kwenye computer au find my iphone app kwenye apple device nyingine. weakness yake ni kwamba huyo mwizi akiRestore basi kila kitu kitafutika na hautaweza kuitrack. unaweza usiweke keylock au security lock ili huyo mwizi aweze kuitumia simu na kubadilisha line tu ili asishawishike kwenda kuiRestore. ikiwa hivyo utaweza kuitrack simu yako.

kwa IOS 7

IOS 7 wameImprove kidogo usalama wa simu yako. kama uliLink simu yako na iCloud na ukaireport as stolen and then Erased it, basi huyo mwizi hata akaflashi/Restore vipi hawezi kupita Activation screen. itakuwa inamdai aweke Apple ID iliyokuwa kwenye simu kabla haijaibiwa. kwahiyo hataweza kuitumia simu asipoweza kufanya activation. hii feature mpya inasaidia sana watumiaji wa bidhaa za apple.
activation-lock.png
 
kwa IOS 6 or earlier

kama simu yako ni iPhone weka 'Find My iPhone' app, link na icloud service alafu enable restrictions katika simu yako. ukinable restrictions utaweza kuRestrict unInstalation ya program yoyote kwenye simu yako, restriction ya kuSign out Apple ID yako au account yoyote, restriction ya kuzima locations service 'GPS', hivyo kama mtu akiiba simu na akafanikiwa kubadilisha line utaweza kuitrack, kuErase contents, kuiLock au kuifanya ipige alarm. hii yote utafanya kupitia icloud service kwenye computer au find my iphone app kwenye apple device nyingine. weakness yake ni kwamba huyo mwizi akiRestore basi kila kitu kitafutika na hautaweza kuitrack. unaweza usiweke keylock au security lock ili huyo mwizi aweze kuitumia simu na kubadilisha line tu ili asishawishike kwenda kuiRestore. ikiwa hivyo utaweza kuitrack simu yako.

kwa IOS 7

IOS 7 wameImprove kidogo usalama wa simu yako. kama uliLink simu yako na iCloud na ukaireport as stolen and then Erased it, basi huyo mwizi hata akaflashi/Restore vipi hawezi kupita Activation screen. itakuwa inamdai aweke Apple ID iliyokuwa kwenye simu kabla haijaibiwa. kwahiyo hataweza kuitumia simu asipoweza kufanya activation. hii feature mpya inasaidia sana watumiaji wa bidhaa za apple.
activation-lock.png

Hii imekaa vizuri lakini ni kumfanya mwizi wako asiweze kutumia iphone yako tena na si kuipata
 
Hapa nimejifunza kitu,naomba kuuliza swali la nyongeza je kwa kutumia maujanja mlioueleza hapo juu naweza kujua simu ya mtu mwingine mahali ilipo kwa kutumia simu yangu yaani niwe napata taarifa mahali simu ya muhusika ilipo?
 
Msaada nina sony Ericsson Xperia x10i nashindwa kuupdate version yake kwani nindogo iliyopo ni 2.6
 
Back
Top Bottom