Kuishiwa nguvu za iganja vya mikono

Uncle Rukus

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
2,415
398
Habari wana JF Kheri ya mwaka mpya

Siku za hivi karibuni nimekubwa na hali ambayo sijaweza kuielewa kama ni ugonjwa au la, ni kwamba kila niamkapo asubuhi au mda wowote kama nilikuwa nimelala, na kuwa siwezi kushika kitu chochote kwa dakika kama 5 hivi,viganja vya mikono vinakuwa havina nguvu kabisa, kama vile vimekufa nganzi flani hivi. Kuponyeza simu kwa wakati huo ndio zoezi gumu kuliko yote..

Je naomba kujua huu ni ugonjwa ama ni kidu gani? na kama ni ugonjwa ningependa kupata ushauri kutoka kwenu naweza je kuondokana na tatizo hili.
 
hujatuambia una miaka mingapi? na hayo maradhi yako yamekuanza lini? na unapokuwa umelala mikono yako huwa unailalia? inaonyesha una matatizo ya ganzi kwenye viganja vyako vya mikono jaribu kumuona upesi Daktari akupe

dawa na unapo amka asubuhi jaribu kuifanyisha masaji viganja vyako vya mikono na uwe unakunywaa maji ya

uvuguvugu glasi 2kabla ya kunawa uso ukisha nawa uso kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi moja kisha kaa dakika

45 ndio waweza kula chakula na mchana kunywa glasi moja maji ya uvuguvugu kisha kaa dakika45 ndio waweza kula

chakula chamchana na usiku kabla ya kula chakula cha usiku kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi 1 kaa dakika 45

kisha kula chakula cha usiku na wakati wa kulala kunywa glasi mojamaji ya uvuguvugu kisha lala usingizi anya hivyo

kila siku utapona inshallah.
 
Asante MziziMkavu , Nina umri wangu ni zaidi ya miaka 40, ili tatizo limejitokeza kama miezi mitatu sasa. wakati mwingine hiyo hali inapotea na kujirudia.... Nitazingatia ushauri wako mkuu.
 
Asante MziziMkavu , Nina umri wangu ni zaidi ya miaka 40, ili tatizo limejitokeza kama miezi mitatu sasa. wakati mwingine hiyo hali inapotea na kujirudia.... Nitazingatia ushauri wako mkuu.
Mkuu Uncle Rukus Hiyo ni Dalili ya

Upungufu wa Vitamini mwilini nakupata ugonjwa wa Ganzi na kutokana na umri uliokuwa nao huo kila kitu huwa kinaanza hapo kubadilika

ndani ya mwili wako uwe muangalifu sana nenda kamuone daktari na pia uwe unatumia dawa za Vitamini Multi vitamin itakuondoshea

hayo matatizo ya kuishiwa nguvu kwenye viganja vyako na pia uwe ukimaliza kunywa maji ya uvuguvugu Asubuhi ukae dakika 45 kisha

kula tunda moja la Apple,Tango moja na chungwa moja kila siku asubuhi fanya hivyo utaondokewa na hayo matatizo yako pole sana.
 
MziziMkavu wewe ni daktari mzuri sana wa afya za watu. Naomba nikuombe kwa msaada wa wengi tuombe JF wafungue sub-forum ya health tofauti na ile ya JF doctor iwe maalum kwa ajili ya issues za kuimarisha afya. Hii itasaidia sana watu walioko busy hasa wale wanaotumia vyombo ambayo kwa namna moja au nyingine vina mionzi na divyo vinaharibu afya zetu. Kwa mfano afya zote zihusuzo na minimization ya impact ya kuwa kwa computer muda mrefu ukifanya kazi!! Vinginevyo tunapata madhara na watanzania wengi masuala ya health diet ni kitendawili.
 
Habari wana JF Kheri ya mwaka mpya

Siku za hivi karibuni nimekubwa na hali ambayo sijaweza kuielewa kama ni ugonjwa au la, ni kwamba kila niamkapo asubuhi au mda wowote kama nilikuwa nimelala, na kuwa siwezi kushika kitu chochote kwa dakika kama 5 hivi,viganja vya mikono vinakuwa havina nguvu kabisa, kama vile vimekufa nganzi flani hivi. Kuponyeza simu kwa wakati huo ndio zoezi gumu kuliko yote..

Je naomba kujua huu ni ugonjwa ama ni kidu gani? na kama ni ugonjwa ningependa kupata ushauri kutoka kwenu naweza je kuondokana na tatizo hili.

Kupooza kwa muda kwa viungo au mwili mzima husababishwa na sababu nyingi.......

Inaweza kusababishwa na sababu ndogo isiyohatarisha kwa mfano kutopumua vizuri wakati wa kulala au kulala vibaya (kulalia kiungo kwa muda mrefu)...

Pia huweza kusabibishwa na sababu kubwa na za hatari kama Stroke, Botulism , amyotrophic lateral Sclerosis nk...

Labda nikuulize...unatumia pombe/sigara , una historia ya kisukari au shinikizo la damu au cholesterol (uzito mkubwa)...Kama ni ndio angalau kwa moja ya haya inawezekana ukawa na stroke (sehemu ya ubongo haipati damu)...

Jaribu kufika hospitali uonane na wataalamu usipende kujitibia nyumbani mpaka mwili wote ushindwe kufanya kazi..Waone wataalamu wa mfumo wa fahamu (neurologists) nadhani utasaidiwa haraka...

Ugua pole na tafadhari utupatie feedback ya ugonjwa wako ili nasi tuendelee kujifunza....
 
Back
Top Bottom