Sasa dume zima utaendaje
kuishi kwa dadako aliyeolewa??unaamka asubuhi unagombania chai na
h/girl?! kwangu mimi haijakaa poa hata kidogo! Kwani huyo shemeji ameoa
ukoo mzima?labda kama dada hajaolewa it might make sense.
Mtambuzi kuna watu wanasemea haya mambo ya extended family sijui wakati wa kusoma na mambo kama hayo
Ila nayo yana muda wake bana
Huwezi kusema kusaidiana unakaa na kaka yake anafanya kazi ila bado anaishi kwako kisa extended family
Huwezi kuendelea kukaa na kaka yako ambaye amemaliza masomo na hujaona juhudi zake za kutafuta kazi kisa tuu ni kuwa unataka umsaidie
Kuna mipaka na umri pia
Usitake kuniambia kaka yako ana miaka 30 bado yuko kwako unazidi kumsaidia kisa extended family au sijui kwenu kuna matatizo
Duh kuwe na mipaka bana
nyumba kubwa tushapotez avingi sana ambavyo vilikuwa vinatuweka kwenye real nduguMi najua tatizo ni kuiga western culture huku tunasahau kuwa kwa wenzetu serikali zina mfumo wa kuhudumia watu wasio na uwezo/ wasio na kazi na wazee.
Tamaduni zetu za kibantu zinakufa wakati context ilotufanya tuwe na hizi tamaduni haijabadilika...umasikini
Ona Kenyans wanavyotoka. Kuna dada nilikuwa nae huku ugahibuni ananmbia anasomeshwa na ukoo.
Watu wanashindana ili koo zao zisiwe nyuma...sisi tukitoka tunafanya juhudi kuhakikisha hakuna wa kutukaribia ili tuendelee kusujudiwa.
SnowBall hiyo kitu inatokea kwa sababu maalumUnajua braza Mr Rocky kinachogomba hapa ni ile hali ya kuwamis'treat' watu wanaokaa kwa dada zao..yaan jamii imeshakuwa na kama streotype flani kuwa kukaa kwa dada yako ni ushenzi..no matter what. Na kama alivyosema nyumba kubwa na wadau wengine like sakapal et al..kuwa kuna kuishi kwa dada kwa nia ya wewek ujijenga na pia inaweza kuwa ukoo wenu mmetanguliwa na wanawake. So kwa vyovyote vile lazima dadaako atakuwa na 'stake' kwenye makuzi yako.
Hatukatai mtu mvivu kufukuzwa na kuambiwa akajitegemee..but how do you consider the entire saga?..Does this happen to rescue the love of the two hata kama wana nyumba kubwa ya kuishi????
kuna watu sijui wanaogopa maisha au wanapenda tu kukaa kwa watu. sio wote wanaokaa kwa watu wanastahili.acha tu nipite.....
maana sidhani kama kuna mtu anapenda kuishi kwa dada au kaka yake au ndugu yoyote....
nadhani ni ugumu na matatizo ya dunia....
sema kwa vile mtu hatembei na bango la matatizo yake mtu huwezi kuona wala kujua zaidi ya kunyoosha vidole...
hivyo acha nisonge mbele.....
nyumba kubwa tushapotez avingi sana ambavyo vilikuwa vinatuweka kwenye real ndugu
Yaani vile vitu tulivyokuwa tunajivunia vimeushikkilia undugu havipo tena
Tena kwa upande mwingine watu wanawaogopa ndugu zao kupindukia
Maana seme umpe ndugu biashara yako asimamie ndo anakuangusha
ukimpa mtaji afanye biashara ili umnyanyue yeye na yeye awanyanyue wengine ndio kama umempa hela ya kwenda kufanya starehe
Ukisema umpe hata kazi fulani asimamie yeye ndio anashirikiana na wengine kuhakikisha kuwa hiyo kazi haikamiliki au kukuibia
Sijui vile vitu vilitufanya tupendane na tufanye mambo ya maendeleo kunyanyuana vimeishia wapi
Ila tuseme ukweli we kaka mtu mzima kukaa kwa dada hata sio kabisa, unakutana na shem wako ametoka kumshughulikia dada yako haaaaa!!!!!! hapana alafu afadhali uwe unapatana na shem wako kama hampatani lol ndio atakuoneshea kiburi kabisa kwamba kama ifuatavyo ndio naenda kujimegea kiulaiini. kweli mi sishauri labda kama huna jinsi.
Dada yako atashughulikiwa tu whether unakaa nae au unakaa mbali. Lol.
Ila tuseme ukweli we kaka mtu mzima kukaa kwa dada hata sio kabisa, unakutana na shem wako ametoka kumshughulikia dada yako haaaaa!!!!!! hapana alafu afadhali uwe unapatana na shem wako kama hampatani lol ndio atakuoneshea kiburi kabisa kwamba kama ifuatavyo ndio naenda kujimegea kiulaiini. kweli mi sishauri labda kama huna jinsi.
acha tu nipite.....
maana sidhani kama kuna mtu anapenda kuishi kwa dada au kaka yake au ndugu yoyote....
nadhani ni ugumu na matatizo ya dunia....
sema kwa vile mtu hatembei na bango la matatizo yake mtu huwezi kuona wala kujua zaidi ya kunyoosha vidole...
hivyo acha nisonge mbele.....
kuna watu sijui wanaogopa maisha au wanapenda tu kukaa kwa watu. sio wote wanaokaa kwa watu wanastahili.
kuna siku nilimtembelea rafiki yangu. jioni ilipofika shemeji yake akarudi toka kazini. ni mtu mzima na ana mke na watoto ambao wanakaa mji mwingine. ana kazi nzuri na mshahara wa kutosha tu lakini anasema hawezi kupanga nyumba miji mi2, i.e. nyumba ambayo mkewe anakaa na watoto, na hapo anapokaa yeye, kwa hiyo kaamua anakaa kwa kaka yake mpaka further notice, lol!
Ni kwamba hata sabuni ya kuogea mwenyewe na colgate ni vile vya watoto na hg kule bafu la common, nini kuchangia chumviHuyu shemeji naye kiboko, lakini anachangia 'mafuta' kidogo au ndio tena hawezi kununua mafuta ya miji miwili?
Kwa nini huyu ionekane ni sahihi kukaa kwa shemejie mito ?
Kwani naye si anakaa kwa shemejie kwani huyu hawabani????
This Message Has been Deleted By Shemeji.
Reason:Kaambiwa na Dada aifute