Lazima mume awe na uwezo eh?
BTW sakapal salama??
SnowBall acha hiyo habari hata kijana kukaa kwa kaka mtu mawifi huwa wanawatesa sana mimi nina kaka yangu anasoma hapo udsm alikuwa akifunga chuo anajiegesha kwa kaka yangu lo alikuwa anafanyiwa visa mpaka eeehu basi mimi mdogo wake nikamwambia isiwe shida njoo kaa kwanguuuu ila mbona haokuwa shda inategemea sana huyo mme wa dadayak akoje ukikuta ndio kamwokota baa basi atawanyanyasa wote
Mr Rocky Is this the reason?..Na je kama kama yupo kaka au mdogo wa mume?..is it acceptable?
Mi nawaonea wivu kabisa wanaoishi na wadogo zao/kaka zao wa kiume kwa kuwa najua wanatoka kwenye familia ambayo iko blessed..
Nakubaliana na mawazo ya gfsonwin na ya kwako SnowBall
Kwa vyovyote vile najua ugumu wa wewe kijana kama mwanachuo unahitaji usave ili upambane na maisha
Au ni wewe mwanafunzi wa sekondari unatakiwa ujibane ili upate sehem ya kukaa na kusoma
Kwa malengo hapo nakubaliana na wengi kuwa kuna muda kweli hali hairuhusu inabidi ujibane kwa sister ili kukidhi lengo na huku ukifanya fanya na vikazi vya pale home kusaidia
Ila sasa inapofikia ni kijana wa kiume umri umeenda sio kwa malengo ya kumaliza shule uondoke zako ila unakaa kwa sister bila mpango wowote
Awe ndugu wa mume au wa mke unapojikuta katika mazingira ya kuishi kwa dada yako huna mpango wowote umekaa kaa tuu khasara hapo tena huna cha kujitetea
Unawanyima watu uhuru wao ambao wanautaka
Well said nyumba kubwa ..
How do you consider issue ya time?
How long shall a person stay to his/her relatives..in this case kwa dada?
Badala ya kusema ndugu yako amekaa kihasara kwa nini usimsaidie ili naye atoke???
Ni sahihi kumwambia aende anakokujua kwa kuwa ana dira ya maisha?? Akijiua utalia??
Unless huyo ndugu awe mvuta bangi ambaye nae anaweza kupata ushauri nasaa...badala ya kumdhiaki ndugu yako kuwa anakaa kula kulala unapaswa ufikirie ni jinsi gani ya kumsaidia ili nae ajitegemee. Hakuna anayependa kuwa tegemezi..kuna sababu kama kukosa capital au elimu.
Kwenda kumsalimia kwa siku moja au mbili na kuondoka sio tatizo. Ila kuhamisha kabisa majeshi unakaa utadhani upo kwako haifai. Mwanaume lazima apambane kuwa na kwake siyo kuishi kwa mtu mwingine hata kama ni dada yako. Kama dada ameolewa iko siku mtatukanwa ukoo wenu mzima na shemeji kisa kakorofishana na mkewe ambaye ni dada yako.
Mhhh SnowBall kun amambo ambayo kweli huwezi kufanya na kuna mipaka ya kuka akwa dada
Sijaona faida wala la maana kwa kaka mztu mzima kukaa kwa dada yako awe ameolewa au hajaolewa
na sio mbaya kwa dada kumlea kaka yake
Ila je uhuru wako au uhuru wake ukoje
Tuseme ameolewa yuko na mumewe hapo hapo home
Huoni kama unamyima raha kufanya kile ambacho angefanya kwa mkewe
Maana yeye anajua amemuoa dada yako na ana uwezo wa kumkiss na kufanya utundu wowote na mkewe
Sasa akiwa anafanya huo utundu wewe kaka yake unafeel vipi
Na je kama hajaolewa uhuru wake wa kuja na mwanaume wake ukoje huoni kama unamuingilia na hayuko huru
Maana pale ni kwake yuko huru kuja na mwanaume wake maana ni nyumba yake
Na je wewe nawe kama mwanaume unaweza kuja na gal wako pale na dada yako anakuonaje
na sio mmoja tuu kama kaka mtu anawabadilisha kama nguo hapo ikoje kwa dada
Kwenye nyumba dada najiamini anatoka na kanga moja maana yuko kwake mkakutana kwenye corridor hapo inakuwaje
Ahh mambo mengine sio ya kuombea au kuzungumza mkuu
Tata why so many people think in that way?..Nadhani ni kuwavunjia heshima wakwe..i bet hata kama mtu umekosana na binti huwezi kutukana ukoo wake!!..unless the reason ya tatizo iwe ndugu wenyewe..which also is rare as most problems kwenye ndoa zinakuwa inflicted na infedility..
Mkuu Rocky amenisemea yote, lakini pia jamii ina mchango mkubwa sana katika kuliweka hili jambo kuwa kama kitu kisichopendeza.................
nyumba kubwa ngoja nikuambie kitu
Kuna watu ambao wanasaidiwa na hawajui thamani ya msada unaowapa
Kuna watu wanashauriwa ila hawajui thamani ya huo ushauri wala hawausikilizi
Kuna watu wanapewa hadi mitaji kwa ajili ya kujiendeleza au kupewa elimu ila bado anarudi kwako bila kuwa na lolote la kumsaidia maishani mwake
Sio kwamba watu hawapendi kukaa na ndugu ila mazingira yanayosababishwa na wale ambao hawajui thamani hiyo ndio yanayowafanya watu wadoubt
acha tu nipite.....
maana sidhani kama kuna mtu anapenda kuishi kwa dada au kaka yake au ndugu yoyote....
nadhani ni ugumu na matatizo ya dunia....
sema kwa vile mtu hatembei na bango la matatizo yake mtu huwezi kuona wala kujua zaidi ya kunyoosha vidole...
hivyo acha nisonge mbele.....
Hizo exceptional cases zipo nakubali.
Ila kuna watu ambao wala hawajaribu.
Tena wakiwa na maisha mazuri hata kwao huko vijijini hawakanyagi kwa kuwa ndugu zake ni wa chini sana yeye ni matawi. Na ukute kaoa familia bora ndio kabisaaaa. Hata watoto hawatakaa wakanyage kwa bibi na babu...yani mtu anajitenga na familia.
Kusaidia ni muhimu sana ingawa najua msaada unabidi uwe ndani ya uwezo wako na si kuitesa familia na watoto.
Nina aunt yangu ni mwalimu wa primary lakini amesomesha wadogo zake na sasa ni maofisa; na wengi walikuwa wanakaa kwake mpaka wameanza kujitegemea. Wanaume hawanaga roho mbaya ila ni sisi wanawake hatutaki saidia ndugu zetu. Mume anayekupenda hawezi chukia ndugu zako.
Mtambuzi kuna watu wanasemea haya mambo ya extended family sijui wakati wa kusoma na mambo kama hayo
Ila nayo yana muda wake bana
Huwezi kusema kusaidiana unakaa na kaka yake anafanya kazi ila bado anaishi kwako kisa extended family
Huwezi kuendelea kukaa na kaka yako ambaye amemaliza masomo na hujaona juhudi zake za kutafuta kazi kisa tuu ni kuwa unataka umsaidie
Kuna mipaka na umri pia
Usitake kuniambia kaka yako ana miaka 30 bado yuko kwako unazidi kumsaidia kisa extended family au sijui kwenu kuna matatizo
Duh kuwe na mipaka bana
acha tu nipite.....
maana sidhani kama kuna mtu anapenda kuishi kwa dada au kaka yake au ndugu yoyote....
nadhani ni ugumu na matatizo ya dunia....
sema kwa vile mtu hatembei na bango la matatizo yake mtu huwezi kuona wala kujua zaidi ya kunyoosha vidole...
hivyo acha nisonge mbele.....