Sasa dume zima utaendaje kuishi kwa dadako aliyeolewa??unaamka asubuhi unagombania chai na h/girl?! kwangu mimi haijakaa poa hata kidogo! Kwani huyo shemeji ameoa ukoo mzima?labda kama dada hajaolewa it might make sense.
kwa issue kwa sster si issue,naomba kwanza ni declare interest hili jambo linanigusa moja kwa moja,ubaya wa kuishi ni pale mtu anapoishi kwa sister bila dira na hujisghulishi na shughuli za shule au ajira kama umemaliza shule inakuwa tatzo zaid mhusika anapokuwa mtoto wa kiume,kwa hiyo ni vyema kuisha kwa sister kuwe very timed sio unajiachia kama vile ndo umefika ,kuwa timed while unadesign next move>
Tuseme ameolewa yuko na mumewe hapo hapo home
Huoni kama unamyima raha kufanya kile ambacho angefanya kwa mkewe
Maana yeye anajua amemuoa dada yako na ana uwezo wa kumkiss na kufanya utundu wowote na mkewe
Sasa akiwa anafanya huo utundu wewe kaka yake unafeel vipi
Kwa hiyo issue ni muda wa kukaa..
Ukikaa muda mfupi its okay?
acha tu nipite.....
maana sidhani kama kuna mtu anapenda kuishi kwa dada au kaka yake au ndugu yoyote....
nadhani ni ugumu na matatizo ya dunia....
sema kwa vile mtu hatembei na bango la matatizo yake mtu huwezi kuona wala kujua zaidi ya kunyoosha vidole...
hivyo acha nisonge mbele.....
Mbona umekuwa too general..
Huo upoa unaoutaka wewe ni upi labda?
Unadhani kuishi na dadaako akiwa hajaolewa ndio ina make sense?..how?
akiwa hajaolewa at least inaeleweka ni kama vile kuishi nyumbani kwa wazazi pamoja..
Akishaolewa ni case tofauti kabisa just imagine dadaako akipishana kauli na mumewe upo unawasikiliza, shemejio akitaka kujiachia hata kwa kiss na dadaako siting room wakicheck pembeni na wewe upo unakodolea tv, sometimes unakuta wote mnategemea kipato cha shemeji what a shame?! Siku dada ako akimbore shemeji yako mnatimuliwa wote?? Mambo mengine ni aibu za kujitakia akhaaa!
tatizo hao wanaonangwa ni wale watto wa mama kula kulala miaka hata mimi hawa siwafagilii ila wa kukaa mwezi miezi hadi upate pa kusimama mbona poa tu.
To my view yoote hii inasababisha na extended family ambazo tunazo waafrica. Kukaa na ndugu yako mkubwa au mdogo inategemea familia yenu ikoje kama dada ndo ametoka kwenye familia na ameolewa na mume mwenye uwezo ni sawa kusaidia ndugu zake ila wakikubaliana na mumewe na kama mume hataki huwezi kuta ndugu wako pale hata kama kwao wanataabika.
Mwalimu gfsonwin nimeipenda hii..
Lakini mbona watu hawasemi anakaa kwa kakaake hata kama ni mdada???..has it something to do with mfumo dume?