Kuipa Dodoma hadhi ya Jiji ni lazima kujadiliwe

Ieleweke kwamba Sina kinyongo kwa mji mdogo na duni kama Dodoma kupewa hadhi ya jiji

Lakini je Kauli au amri ya Kiongozi ina uhalali wa kubadili Mji mdogo kuwa Jiji ? Huo ndio utaratibu wa kupata majiji uliotumika kwa miaka yote ?

Ili mji uwe jiji unapaswa kuwa na sifa zipi , je Dodoma inazo sifa hizo ?
La hasha Dodoma haikuwa si mji mdogo ilikuwa manispaa. Baada ya manispaa ukikidhi vigezo ndo huwa jiji. Vigezo vinavyo angaliwa ni pamoja na huduma za kijamii kuwepo kwa ajili ya kuwahudumia watu
 
Bado sana dodoma kuwa jiji nina vigezo

1.Population (inatakiwa kuwa na 800k) yake ni ya watu 2M na dodoma urban ina wat 450k ambapo density yake ni 140/km2 wakati dar ni 3000/km2
2. 80% ya wakazi wanatakiwa wawe na vipato ambavyo tunaita non-agricultural income
3. 99% ya mapato wanapaswa kujitegemea kwa kila kitu pasipo ruzuku kutoka serikalini
4. Viwanda vya processing angalau 5

ntaendelea
Respect br
 
Mi nakumbukumbuka hata nyerere alikuwaga na mpango huo.sema tuu labda ni kwa vile Sheria imetolewa na magufuli ndo maana inazua mjadala.
 
Ieleweke kwamba Sina kinyongo kwa mji mdogo na duni kama Dodoma kupewa hadhi ya jiji

Lakini je Kauli au amri ya Kiongozi ina uhalali wa kubadili Mji mdogo kuwa Jiji ? Huo ndio utaratibu wa kupata majiji uliotumika kwa miaka yote ?

Ili mji uwe jiji unapaswa kuwa na sifa zipi , je Dodoma inazo sifa hizo ?
Haina sifa ila end jusfy the means. Tujadili jinsi ya kuufanya mji uwe jiji period.
 
Yaani Dodoma ina hadhi ya kuitwa jiji kuliko moshi? hii kali aisee
Hivi moshi kweli unafananisha na Dodoma?? Moshi ni mji mdogo sana in all angles mku, hailingani na dodoma. Ni mwaka tu nilikuwa hapo Moshi kwa mwezi mzima.
 
IMG-20180427-WA0001.jpg


Someni hii pia kifungu cha 14

CC: Erythrocyte
Mwana Mtoka Pabaya vigezo na ushahidi ndiyo msingi wa majadiliano na si matusi wala vinginevyo.
 
ukweli dodoma imepewa hadhi ya jiji sio kwa vigezo vya maendeleo yani imetunukiwa kama vile wanasiasa wanavyopewa u Dr/Prof wa mezani bila kusomea. issue inakuja Dodoma itapata faida na hasara gani na hadhi ya jiji?
 
Hakuna mji wowote Afrika Mashariki na Kati uliojengwa na kupangiliwa kitaalamu kama Dodoma.Zaidi ya asilimia 90 Manispaa ya Dodoma maeneo yote yamepimwa.Huwezi kuta mtu yeyote kajijengea ovyoovyo.

Hii inatofautisha hata na majiji mengine yote yaliyotanguliwa kupewa hadhi ya Jiji Tanzania.Nimefika majiji yote Dar,Arusha,Mbeya,Tanga,Arusha kwa upande wa mipango miji hawafiki hata robo ya Dodoma.

Barabara,Miundombinu ya manispaa ya Dodoma ipo kimpangilio na ni mfano wa kuigwa Afrika ndio maana Wanaigeria walikuja kuchukua master plan ya mji wa Dodoma na kwenda kuifanyia kazi kwenye mji wao wa Abuja.

Kwa sasa ndio manispaa pekee Tanzania yenye hospitali 4 za rufaa ambazo ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Benjamin Mkapa Hospitali -Udom,Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa ya Akili -Mirembe,Hospitali ya Rufaa ya magonjwa ya Macho -Mvumi.

Uwepo pia wa vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu kama Chuo Kikuu cha Dodoma,St John University, CBE,Chuo cha Mipango,Chuo cha Madini,Chuo cha Biblia-TAG,Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo n.k
Kwa ujumla Dodoma "facts" zote zinakubaliana na hadhi ya Dodoma kuwa Jiji na Makao Makuu ya nchi.
Ni kweli Tanzania majiji well planned ni Tanga na Dodoma. Arusha, Dar na mwanza ni miji iliyojengwa ovyo sehemu kubwa bila kufuata mipango miji.

Kwa kweli inasikitisha watu kutumia siasa kupingapinga kila kitu.
 
Back
Top Bottom