stardust JK
JF-Expert Member
- Jan 7, 2018
- 2,975
- 4,207
Maamuzi ya kipuuzi na ya kukurupuka
Dodoma na kilimanjaro ni mbingu na ardhi
Dodoma na kilimanjaro ni mbingu na ardhi
hata akiyafanya yawe kijiji poa tu. si ataondoka au huyu ni wa maisha?Kama rais anaamka na kuamua Manispaa fulani iwe jiji halafu tunakenua badala kumuuliza kama taratibu zimefuatwa, tunaelekea pabaya.
Kuna siku atakuja kuamka na kuya fanya majiji yasiyoipenda CCM kuwa Manispaa.
Tusikubali Rais aamue, bali taratibu zifuatwe.
kama kuomba omba ni maisha mazuri nakubaliHilo halina ubishi!
Mkuu kwa point ya idadi ya watu hapana nakukatalia soma vzuri data za sensa ya watu na makazi Dodoma inazidiwa idadi ya watu na geitaDodoma ni mji wa 4 kwa idadi ya watu ikiipita mbeya huku ikiipumulia Arusha kisogoni,next sensa nadhani itakuwa nyuma ya mwanza baada ya Dar
Bila shaka umekidhi viwango in terns of population,mpangilio wa mji,mapato,viwanda na makao rasmi ya serikali
Acha ujinga wewe. Dodoma ni mji mkuu wa nchi kuwa jiji ni lazima sababu maendeleo ya pale kuanzia sasa hiwezifananisha na sehemu ingineNi maamuzi ya kipuuzi tu lakini Dodoma haina hadhi ya Kilimanjaro. Maamuzi ya kukurupuka yanaligharimu sana Taifa la Watanzania.
Eehhh mkuu, maana hivyo ndio viwanda.... tehteehhhHaha hakuna namna kwa kweli
Jaribu kujiridhisha hapa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa ww umeisha hapo Dodomya linganisha vigezo hv km vinakidhi.Nimeishi hapo Dodoma mika 4 Iliyopita! Sijui Kama ndani ya hii miaka minne kama Dom imefikia hadhi ya kuitwa jiji kwa mjibu wa vigezo na sheria zilizopo! Au limekuwa jiji la kisiasa.
Rais anaishi kwenye halmashauri ya wilaya ya Chamwino,hata hadhi ya manispaa haijafikia maana ndio ikulu ilipo!Utafiti ulishafanyika, hata hivyo rais hawezi kuishi kwenye manispaa, hiyo ni kura ya veto, kwa vigezo mmmmmmmmmmm
unajua hata mie nimeona hivyo vigezo Dodoma inavyo vyote tena toka 2014 (mara ya kwanza naingia dom)Haya mnayoyataja mbona yapo?? Au nyie mnaijua dodoma Ipi??
Waswahili walisema kutangulia si kufika na kwamba mwenda pole hajikwai, hatimaye leo Dodoma imekuwa Jiji wakiitangulia Manispaa ya Moshi Hongereni sana Wagogo na Warangi......Dodoma hoyeeee!!!
Kwa Moshi bado sana kuwa Jiji kwa sababu za Kihistoria, Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.
Kihistoria, Mji wa Moshi haukujengwa na wenyeji. Kwa hiyo Wachaga hawana sense of responsibility and ownership na Mji wa Moshi.
Kiuchumi, Mji wa Moshi na Kilimanjaro kwa ujumla wake hauna rasilimali wala shughuli za kiuchumi za kuwezesha kuujenga hadi kufikia hadhi ya kuwa Jiji. Hii ni kwa sababu hata majengo makubwa yaliyopo yameshindwa kupata Wapangaji wa kuyajaza. Mfano ni Jengo la NSSF.
Kijamii, Wachaga ni muungano wa Vikabila Vingi ambavyo vinaenzi zaidi sehemu zao asilia kuliko mji wa Moshi. Wachaga wote popote walipo huwaza zaidi kujenga vijijini kwao kuliko Moshi Mjini. Hii inaufanya Mji wa Moshi kuendelea kubaki na muonekano wake wa zamani.
Hata wale wachache wanaothubutu kuwekeza katika Mji wa Moshi hukutana na vikwazo kutoka kwa Maaliwatani wa Mjini na hivyo kuwakatisha tamaa.
Kwa upande wa Kisiasa, Mji wa Moshi unaathiriwa kwa kiasi kikubwa na siasa za Kinafiki si kwa Chadema wala CCM. Wote ni wachumia Tumbo na hawana utashi wa kiasa wa kuujenga mji wa Moshi. Kilichopo ni jitihada binafsi za watu wachache za kutaka Moshi iwe Jiji lakini ukichunguza kwa undani, hutashindwa kubaini kuwa ni wachungulia dili tu wakiwa na lengo la kupata manufaa binafsi mwisho wa siku.