Kuingilia Mawasiliano ya Viongozi: Rais Magufuli anajitapa hadharani kuvunja Katiba ya nchi

Sam Naipenda

Member
Mar 1, 2018
97
720
Wakuu, nitaendelea kuwakumbusha uhatari wa “Mfumo Jiwe” na madhara yake.

Nigusie vituko viwili viliyojitokeza kwenye bongo muvi ya leo hapa ikulu vinavyoelezea mfumo huu:

Moja: Rais anatangaza hadharani kwamba yeye anasoma meseji za watu wengine. Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 utaona wazi kwamba uhuru wa faragha ya mawasiliano na kupata habari ni moja ya haki za msingi kabisa za raia zinazotolewa na kulindwa na katiba. Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kisheria ya kudukua mawasiliano ya mtu mwingine kwa sababu yoyote ile. Sio rais, sio Jeshi la Polisi, sio TISS, sio baba ya mtu, sio mume wa mtu wala mke wa mtu.

Hata vyombo vya Usalama vinapofanya hivyo kwa sababu za kiusalama hawatangazi hadharani. Ila tuna Rais wa nchi ambaye aliapa kulinda na kuiheshimu Katiba anatangaza kwamba huwa anasoma meseji binafsi. Hii ni hatari kwa usalama wa nchi na raia mmojammoja.

Mtakumbuka kijana wake (Makonda) naye alitangaza kwamba ana teknolojia ya kuweza kujua watu walioweka video za ngono kwenye simu zao (hii hata waliotengeza simu hawana ila Makonda anayo). Huu ndio #MfumoJiwe.

Mbili: Rais kwa ujasiri kabisa anatumia nafasi yake kama Rais wa nchi na Mwenyekiti wa chichiemu kumtisha mbunge aliyechaguliwa na wananchi kwa sababu za ugomvi binafsi alionao na Mkuu wa Wilaya. Pia anatoa maagizo mbele wa spika dhaifu wa bunge asiyejielewa kwamba mbunge huyo akaombe radhi mbele ya Bunge kwa ugomvi binafsi na mke wa mtu.

Tangu lini Bunge limekuwa mahali pa kuombea radhi magomvi binafsi? Kwanini huyo mke wa mtu aliyetukanwa asiende kushtaki Polisi ili mahakama itoe hukumu na badala yake Rais ndio anakuwa Jaji na Bunge linakuwa jukwaa la kuombea radhi? Huu ndio “Mfumo Jiwe”

Spika Ndugai alipopokea ripoti ya kamati ya kina Waziri mpya wa Madini (Biteko) ambayo badala a kuiwasilisha bungeni ijadiliwe aliipeleka moja kwa moja kwa bosi wake Rais Magufuli, alisema alipokuwa anateua Kamati alimuuliza Rais amteue nani. Hivyo ni wazi Magufuli ndio aliyeagiza Biteko awe Mwenyekiti wa Kamati. Leo Magufuli anatumia tukio na kituko hichohicho kujaribu kuonesha kumfagilia Spika dhaifu anayeongoza Bunge dhaifu kwamba eti Biteko ni matokeo ya uchapaji kazi wa Bunge. Huyu ndio Magufuli mtengeneza matukio kwenye “Mfumo Jiwe”
 
Nilichogundua ukitaka usilale usiku au usiende likizo basi anza kudukua na kusoma meseji za wenzio hakika hutalala usingizi.

Kuna bwana yupo na yumomo kwao nilimwomba apatapo muda usiku nimpigie ili tuongee mambo yetu lakini alinishauri nimwone ana kwa ana siku inayofuata, nilipomwona tuliongea yetu lakini mwisho nikamuuliza kwanini hakutaka nimpigie simu usiku? akajibu kweni hujui kuwa tumepata msaada toka Israel? haraka sana nikakubaliana naye!
 
Back
Top Bottom