Kuigawa Mbeya: Ushauri wa JF Kuhusu Mlowo

Kuigawa Mbeya: Ushauri wa JF Kuhusu Mlowo

Hivi Tanzania itaishia kuwa na mikoa mingapi iwapo kila mara mikoa inagawanywa? Jee ni kweli uongezaji wa idadi ya mikoa/wilaya una tija?
 
Nasema watu wa kyela tulinyonywa sana na watu wa rungwe ndio mana tukamua kujitenga na kuunda kanisa letu la moriavian kyela, mi ni mtu wa kyela mkuu
hahahah hivi mkuu mbona kama kuna siku niliona wamwambia ndumyana kuwa wewe ni wa Kyela
 
Last edited by a moderator:
Hujanielewa mkuu nlicho maanisha ni kua kyela na tukuyu kwenda mbeya ni mbali kuliko moshi to arusha au dar to kibaha, si kwamba nataka kyela iwe mkoa hapana mkuu, kyela huiwezi kuipa mkoa make ni ndogo sn ni kati ya wilaya ndogo apa nchini na kyela haifai hata kugawanywa iwe na majimbo mawili hapana,. Kyela inaki kua wilaya na jimbo moja,. Rungwe iwe mkoa mbapo ichukue wilaya ya ileje na mbeya vijijini itakua sio mbaya,. Kama utakua umenielewa ntashukuru,. Ila wazo la kuugawa mkoa wa mbeya halina maana yoyote zaidi ya siasa
Mkuu, hivi kweli unaweza kusema kwa moyo kwamba Chunya hakuna watu ila Kyela na Tukuyu ndiko kuna watu wakuhitaji mkoa!. Uko sahihi kwa mawazo yako.

Ni kwa vigezo gani unaweza kulinganisha population za mikoa ya Arusha na Moshi ni sawa na Tukuyu na Kyela? Kyela kuwa mkoa ajili ya nini? Ka kijiji kale kenye vitongozi ipinda, kasumulu, kapwili, kalumbulu, Itunge, Ngyeke sijui wapi Usale, na Ipande sijui kwa wauaji ndiyo ipewe mkoa? Naomba jamani tuwe serious na hasa linapokuja suala la maendeleo ya taifa.

Roho ya ubaguzi wa huko Kyela mnataka sasa iingie katika mfumo wa taifa? Naomba usiwe mmoja wa wale wanaojiita wakumyetu wanaowish usiku na mchana kufukuza wageni wote, wabaki peke yao. Na sasa unataka kuhalalisha mupewe mkoa kwa sababu hata mkipewa mkoa bado nia ya kutaka kujibagua ama kubagua wengine haitatimia. Bado mtahitaji michango mbli mbali kutoka sehemu na watu wa sehemu zingine duniani.

Twende vizuri tu. Tujadiliane kwa hoja na amani tutafikia muafaka sahihi. Tukiendekeza u mimi , ukabila na ukwetu, tutaend up tena ku split na kuanza kupeana fursa kwa misingi ya koo, n.k.
 
Hivi Tanzania itaishia kuwa na mikoa mingapi iwapo kila mara mikoa inagawanywa? Jee ni kweli uongezaji wa idadi ya mikoa/wilaya una tija?

Watakupatia vigezo vya idadi za watu na maelezo mengine rundo. Lakini huwezi kuapata ushahidi mahali popote kwamba kuna nchi iligawanya makao makuu ya serikali kuu kwa sababu watu wameongezeka kutoka milioni 9 (tisa) 1961 hadi watu milioni 40 miaka 40 baadaye. Kugawanya mikoa badala ya kuboresha huduma na miundombinu ni upuuzi ambao kwa kweli unachocheo ukabila na kuondoa muingiliano wa makabila. Kugawagawa mikoa badala ya kuboresha miundombinu na huduma hakuna tija! Sana sana kunastawisha ukabila na kuongoeza gharama za kuendesha serikali.
 
Umenena vema Ileje. Ni kweli kwamba lengo la uzi huu ambalo pengine halikutegemewa linaweza likawa haja ya kutumbua hiki kijipu cha kuusambaratisha mkoa wetu. Nani hasa mwanzilishi wa wazo hili? Lakini pia kuna faida gani tunapata katika kusambaratika huku. Je serikali imechukua hatua sahihi katika kushughulikia suala la kuusambaratisha mkoa?

Nikubaliane na wewe kwamba Chunya wamekosa miundo mbinu mingi kwa miaka mingi na kuleta shida kwa ndugu zetu Wabungu kuna wakati huwa napata wasiwasi kama wanajisikia ni wakazi wa Mkoa wetu. Nina mdogo wangu anaishi Chunya mjini kajenga kule. Sijawahi kuenda kule kumjulia hali kwa sababu tu ya shida ya usafiri. Lakini hilo la kusahaulika ni kweli kuhusu Ileje Pia. Nina biashara ambayo inanipa nafasi ya kujua kwamba wafanyabiashara wenzangu wanaokaa Chunya na Ileje wanalipia gharama kubwa sana kufadhili safari za mafundi kutoka Mbeya Mjini kwenda ama Chunya, ama Ileje. Fundi wa mashine akisikia neno Chunya, au Ileje, anajua hiyo ni kazi ya siku mbili hadi tatu, wakati ambapo anaweza kwenda Tunduma, Kyela Vwawa--au hata Makambako akafanyakazi na kurudi kulala nyumbani Mbeya.

Nirudi kwenye hoja: Rungwe wanataka kujitenga. Hilo limezaa Wazo la kuitenga Chunya, lakini pia limezaa wazo la Mbozi na Ileje kutaka kujitenga. Kwa mtizamo huo Rungwe wameleta utengano katika mkoa.

Serikali imefanya sawa katika lile ambalo imefanya? Kwa mara ya kwanza naomba niseme ndiyo. Serikali imekwepesha Rungwe ikiwa inajua hilo linaweza kuleta shida kati ya Kyela na Rungwe yenyewe huko mbele. Yanaweza kuzuka masuala ya Ruzuku za Serikali na mtawanyo wa maendeleo watu wakakatana mapanga na kuchomeana nyumba pale. Kwa hiyo dawa ni kuwabakiza hawa katika pool moja inaitwa Mkoa wa Mbeya. Serikali wamefanya sawa kuwanyima Rungwe Mkoa kwa sababu Mkoa huo ungelazimisha Kyela, na pengine Ileje kuwa ndani, na Rungwe wangewasumbua sana Kyela na Ileje kwa misimamo ya wazi na ya siri kuwa wao ndo haswa wakubwa, ambao waliomba mkoa na wakaupewa! Nadhani wewe pia umeafiki mtizamo wa serikali. Hapo tupo pamoja.

Kuhusu Chunya kutengwa ama kujitenga--kama wanataka--hili niseme lingejadiliwa na WanaChunya wenyewe waangalie kama kuna faida kwenye lipi: Pesa za kuugawa mkoa ziboreshe miundombinu Chunya na Ileje hasa, ama pesa hizo zipewa makandarasi wa kujenga majengo ya makao makuu ya Mkoa wa Chunya ili watu wa Ileje wabaki na miundo mbinu mibovu kama ilivyo sasa na kulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata makao makuu Chunya.

Binafsi nadhani kitu sahihi ni kuboresha miundombinu kwenye haya maeneo mawili: Hivi Tukiwa na Lami safi kati ya Mbeya Mjini na Chunya Mjini, halafu tukaweka Lami safi kati ya Mbeya mjini na Ileje--hasa kupitia njia mkato inayoanzia Njia panda ya Iyula, kuelekea Idiwili , kupitia Hezya hadi Itumba. Huoni kama Mbeya mjini patafikika kirahisi sana kati kwa kila mtu? Ujue kwa kuweka lami safi kwenye maeneo ambayo nimeyataja, Mtu aliyepo Chunya na Aliyepo Itumba watafika pengine wakati huohuo Mbeya Mjini na mtu ambaye anatakoka Kyela.

Wakati huo huo uboreshaji wa miundombinu--hasa hasa barabara utakuwa na faidi nyingi za ziada ukiachana na hili la kufikika kwa urahisi makao makuu ya mkoa. Wagonjwa watafika Rufaa haraka, wahalifu wa jinai kubwa watafika haraka mahakama kuu Mbeya mjini. Huduma chake zinazolazimika kufanyika mkoani kwa kuwa haziwezekani wilayani zitafuatwa na kufikika kwa urahisi Mbeya mjini.

Mimi kwa kweli nadhani kitu sahihi ni kuboresha miundo mbinu badala yakuongeza gharama za kuendesha serikali kule Mbeya. Kama kuna mtu ana pesa zinamuwasha kujenga majengo na kuajiri rundo la watu Mkwajuni nashauri ajenge lami kwenda Chunya na Ileje na hizo hela.

Mkuu ninakubaliana nawe 100% nikiwa kama mwana mbeya mwenzako wa pande za Isiyonje-Irambo. Mgogoro mzima umesababishwa na wanyakyusa wa Rungwe. Ni wabinafsi sana, nakiri hili nikiwa kama mwenyeji wa huko.
 
wadau wa hapa great thinkers
ninalo ombi maalumu kwenu kuhusu tatizo la kuugawa mkoa wa mbeya. Kuna kambi tatu zimezuka kule mbeya kuhusu suala hili, kwa mujibu wa taarifa ambazo ninazo leo, na ni kambi zenye sura ya ukabila. Ninaamini jamvi hili linao uwezo kuisaidia serikali yetu kufanya uamuzi ambao ni sahihi kufuta hii sura ya ukabila badala ya kustawisha taswira hiyo. Kambi moja inataka rungwe kuwa ndo mkoa mpya, kambi ya pili inataka chunya, na sasa mbozi wanataka kwao ndiyo kuwe mkoa mpya na makao makuu yawe mlowo! Na kwamba wazo hili 'eti' linaungwa mkono ya wanaileje.

background:
miaka ya 1980 mkoa wa mbeya ulikuwa na chama kikuu cha ushirika kikiitwa mbecu: Mbeya co-operative union. Wanambeya wanaotoka kyela na rungwe waliomba wapewe uhuru kuunda chama chao. Walipewa idhini hiyo wakajitenga na kuunda chama chao kilichoitwa kyerucu: Kyela-rungwe co-operative union. Lakini baadaye wakazi wa wilaya za kyela na rungwe walishindwa kukaa pamoja katika chama hiki kyerucu ikavunjika na kuunda vyama viwili tofauti zikazaliwa kyecu ya kyela na rucu ya rungwe.

Angalizo ni kwamba kusambaratika kwa mshikamano wa wanambeya kupitia mbecu ulianzia kwenye ukanda wa unyakyusa kutafuta kujitenga. Mbecu bila wanyakyusa ilichechemea kwa muda fulani ikajifia taratibu baada ya watu wa mbozi, ambako makabila makubwa ni wanyiha na wanyamwanga walipoamua nao kujitenga na kuunda vyama vyao vya ushirika, kikiwepo chama kilichoitwa isayula: Isansa-iyula co-operative union.

hoja ya kuigawa mbeya iliyopo leo
taarifa nilizo nazo ni kwamba wilaya ya rungwe ndio waasisi wa wazo la kuigawa mbeya. Rungwe waliomba wapewe idhini kuwa mkoa. Katika mtizamo huo, ilieleweka wazi kwamba mazingira ya ki-jiografia ya mkoa huo yangelazimisha wilaya za rungwe na kyela kuingia katika mkoa huo wa rungwe. Lakini pia ileje ingeweza kuingia bila shida, na pengine sehemu fulani-fulani za iringa ya zamani kwenye maeneo ambayo pengine sasa ni njombe. Wazo la rungwe ndilo hasa msingi wa mgororo uliopo leo, ambao umeanzia kwenye msimamo wa serikali kukataa rungwe kuwa mkoa: Ambapo mimi pia nikiwa mwanambeya mwenye kutetea umoja na mshikamano wa mkoa wetu nasita kukubali ombi hilo la rungwe haraka-haraka kwa sababu ya historia niliyoiweka hapo juu.

mbozi, momba, ileje na chunya
leo nimepewa taarifa ifuatayo: Kwamba katika siku mbili tatu zilizopita, full council ya wilaya ya mbozi imepitisha azimio kukataa chunya kuwa makao makuu ya mkoa mpya dada wa mbeya ambao unatakiwa kuitwa mkoa wa songwe. Wanambozi wamepitisha azimio mkoa mpya uwe mbozi na makao makuu yawe mlowo. Kwa mujibu wa taarifa hizo, wanaccm wa wilaya za ileje na momba wanaafiki wazo hili kuweka makao makuu ya mkoa mpya kuwa mlowo, mbozi. Tatizo linalozuka ni hili: Chunya watapata shida sana kuja mlowo.

My take: Mkoa ubakie ulivyo!

Naomba mawazo yenu wadau tuisaidie serikali yetu kufanya maamuzi sahihi.

===================
maangalizo:
===================
Dhana ya kugawa gawa mikoa ni ya kuwagawa watu kwa mabila yao. muasisi mkuu ni CCM.

Tukiendelea hivi haitakuja kushangaza huko mbeleni kila kabila likiwa na ka mkoa kake.

Geographically, Mbeya mjini ipo almost katikati ya makao makuu ya wilaya zote za mkoa wa Mbeya. Kwa bahati nzuri pia ni kwamba asilimia 80 zimeunganishwa na barabara za lami. ni ujinga sana kuzalisha mkoa mwingine kutoka mkoa huu labda ikiwa ni kwa sababu za kisiasa. Nitakuwa mmoja wa wale wanaopinga ubaguzi huu mpya kupitia dhana ya mikoa mipya.

hili suala ni la msingi kujadiliwa, hata hivyo utata lazima utakuwa sawa na ilivyokuwa wakati wa kuigawa mikoa mingine iliyo tangulia. Naomba watu wa kutoka hiyo mikoa wajitoe pia kuchangia uzi huu na watoe maoni yao kuleta picha kamili ya mchakato wa kuigawa mbeya.

Hata hivyo ingefaa wale wanaopigania kuugawa mkoa wangekuja na hoja, waseme wenyewe nia yao ya kuugawa mkoa imetokana na nini, na ni nini wananchi wenyewe wanasema kuhusu hili......na zaidi kama sababu ni za kukosekana kwa utolewaji sawia wa huduma za msingi pia wasema kwa nini imekuwepo hivyo na wakubali kuwajibishwa.....
 
Mkuu ninakubaliana nawe 100% nikiwa kama mwana mbeya mwenzako wa pande za Isiyonje-Irambo. Mgogoro mzima umesababishwa na wanyakyusa wa Rungwe. Ni wabinafsi sana, nakiri hili nikiwa kama mwenyeji wa huko.

MKUU fYddel, nikushukuru sana kwa neno lako hapa kuunga mkono angalizo la chanzo cha mgogoro uliopo wa kugawa mkoa wetu. labda tu nikusihi kuzimua kidogo msimamo wako katika lile tamshi la ubinafsi wa wanaRungwe. Mimi ni mzoefu wa kutosha wa mambo ya rungwe. hawa watu pamoja na viashiria vya ubinafsi kuwa vingi ni wachaMungu, ni wasikivu na ni waoga sana wa ugomvi. Ninayo hakika haya wanayasoma, wanatafakari na pengine atatokea mmoja wao atakuja hapa atoe maelezo kwa nini wanaona ulazima saaaaana wa kujitenga na sisi ndugu zao.
 
Mkuu ninakubaliana nawe 100% nikiwa kama mwana mbeya mwenzako wa pande za Isiyonje-Irambo. Mgogoro mzima umesababishwa na wanyakyusa wa Rungwe. Ni wabinafsi sana, nakiri hili nikiwa kama mwenyeji wa huko.
Wagona ndama. Wauache kabisa mkoa wetu kama ulivyo. Na tanzania waache upuuzi huu wa kugawagawa mikoa kwa sababu za kijinga kila kukicha.
 
Ile dhana ya umoja ni nguvu imekwisha kabisa nchi hii! Nawalaani kabisa JK na Pinda kuendekeza ubaguzi!

Mkuu Ileje, jana nimeunga mkono Serikali kukwepesha utekelezaji wa ombi la Rungwe kuwa mkoa nikitumia kigezo cha historia. Lakini hili wazo lako pia lina mashiko. Mgogoro huu kwa upande mwingine umeletwa na udhaifu wa kimanejmenti uliopo serikalini.

Nasema mgogoro imekuja kwa sababu serikali inagoma kuwapa Rungwe walichoomba, lakini pia umekuja kwa sababu kuna udhaifu wa kimanejiment pale TAMISEMI. Hata sijaelewa ni waziri gani mwenye dhamana ya TAMISEMI na kama kichwani mwake kuna uelewa kiasi gani wa mkoa wa Mbeya, kama ana uelewa gani wa mambo ya umoja wa kitaifa kupitia mshikamano wa makabila mengi badala ya moja; au hata prudence katika matumizi ya pesa za umma. Hili tatizo linaweza likawa 'manifestation' ya kujaza wanasiasa katika nafasi ambao elimu zao zina utata TAMISEMI; hii ndo sababu peke yake kwa nini wameendelea kufanya maamuzi ambayo hatima yake ni kustawisha ubaguzi wa kikabila.

Nakubaliana kabisa nawe Ileje: dhana ya umoja ni nguvu imekwisha Tanzania, na uwezekano mkubwa ni huu, kwamba nchi imebaki na wanasiasa wenye uelewa finyu sana wa mambo muhimu kwa umoja wa taifa letu.
 
Kulipa kodi sio issue kwa serikali yetu
ki-comment kimesheheni sana hiki, ingawa unakuwa kama ujatenda haki vizuri kutokana na kuwa too brief. kodi siyo ishu kivipi Mkuu.
 
Hujanielewa mkuu nlicho maanisha ni kua kyela na tukuyu kwenda mbeya ni mbali kuliko moshi to arusha au dar to kibaha, si kwamba nataka kyela iwe mkoa hapana mkuu, kyela huiwezi kuipa mkoa make ni ndogo sn ni kati ya wilaya ndogo apa nchini na kyela haifai hata kugawanywa iwe na majimbo mawili hapana,. Kyela inaki kua wilaya na jimbo moja,. Rungwe iwe mkoa mbapo ichukue wilaya ya ileje na mbeya vijijini itakua sio mbaya,. Kama utakua umenielewa ntashukuru,. Ila wazo la kuugawa mkoa wa mbeya halina maana yoyote zaidi ya siasa

Ahsante sana kiongozi kwa ufafanuzi mzuri. Ni kweli kabisa kwamb kuongeza maeneo ya kiutawala ni kuongeza matumizi ya serikali bila sababu. Hata hivyo pia inadhihirisha udhaifu wa serikali na kukosa nia ya dhati na ama mikakati thabiti yenye malengo muru a ya kuboresha maisha ya wananchi. Ni dhahiri kabisa kwamba hakuna sehemu yoyote Tanzania ambayo imeonekana kuendelea kwa sababu eneo lile lilimegwa kutoka sehemu.

Kwa hiyo kugawa maeneo yetu na kuongeza watawala hakuna uhusiano na maendeleo ya Watanzania.
 
Kulikuwa na sababu nzuri sana ya Kuugawa Mkoa wa Arusha....sioni mantiki yoyote ya kuendelea kuigawa mikoa Mingine.
Sikubaliani na sababu yoyote ile ya kuugawa Mkoa wa Mbeya na tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha hilo halitokei. Jiografia ya mkoa yenyewe inakataa mkoa huo kugawanywa, lakini bado mijitu na akili zao inalazimisha, kama si akili za kibakaji hizo ni kitu gani?
Tutahakikisha mkoa huo haugawanywi.
 
Kulikuwa na sababu nzuri sana ya Kuugawa Mkoa wa Arusha....sioni mantiki yoyote ya kuendelea kuigawa mikoa Mingine.
Sikubaliani na sababu yoyote ile ya kuugawa Mkoa wa Mbeya na tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha hilo halitokei. Jiografia ya mkoa yenyewe inakataa mkoa huo kugawanywa, lakini bado mijitu na akili zao inalazimisha, kama si akili za kibakaji hizo ni kitu gani? Tutahakikisha mkoa huo haugawanywi.

tuko pamoja mkuu....
 
Asante mkuu haya magamba yameishiwa mbinu za kiutawala, yamebaki kutugawagawa tu inatia kinyaa sana,. Iazhen mbeya iendelee kama ilivyo ila tunahitaji huduma za kijamii ziboreshwe hospitali ya makandana iboreshwe ili ihudumie jyela na rungwe vizuri, barabara ziboreshwe na umeme vijijini usambwambazwe hatuhitaji upumbavu wa kutugawa hovyo
Ahsante sana kiongozi kwa ufafanuzi mzuri. Ni kweli kabisa kwamb kuongeza maeneo ya kiutawala ni kuongeza matumizi ya serikali bila sababu. Hata hivyo pia inadhihirisha udhaifu wa serikali na kukosa nia ya dhati na ama mikakati thabiti yenye malengo muru a ya kuboresha maisha ya wananchi. Ni dhahiri kabisa kwamba hakuna sehemu yoyote Tanzania ambayo imeonekana kuendelea kwa sababu eneo lile lilimegwa kutoka sehemu.

Kwa hiyo kugawa maeneo yetu na kuongeza watawala hakuna uhusiano na maendeleo ya Watanzania.
 
Asante mkuu haya magamba yameishiwa mbinu za kiutawala, yamebaki kutugawagawa tu inatia kinyaa sana,. Iazhen mbeya iendelee kama ilivyo ila tunahitaji huduma za kijamii ziboreshwe hospitali ya makandana iboreshwe ili ihudumie jyela na rungwe vizuri, barabara ziboreshwe na umeme vijijini usambwambazwe hatuhitaji upumbavu wa kutugawa hovyo

Wewe ni kidume cha mbegu kwelikweli! Big up.... MADE IN MBEYA!
 
mkuu nimekupata kutokana historia fupi ya vyama vya ushirika mbeya! labda ningeomba kujuzwa kwanini serikali inataka kuigawa mbeya? je ni kwasababu za kijiografia au kisiasa?

kwa kifupi wazo la kuugawa mkoa wa mbeya ni la kisiasa zaidi, kwani ktk karne hii ya leo tunazungumzia zaidi juu ya kupeleka huduma na mamlaka ya maamuzi juu ya rasmali kwa wananchi kwa kuboresha serikali za mitaa/vitongoji kama ambavyo leo tunaona shule za msingi sekondari za kata zikiwa chini ya umiliki wa wananchi wenyewe. hili limeleta mtazamo mpya zaidi kwa wananchi kuona wanasehemu yao ktk uendeshaji. kwa mtazamo huu ninashawishika sana kama wilaya ya chunya ingegawanywa na kuwa wilaya mbili na hivyo kuiongezea uwezo zaidi wa kupeleka huduma kwa wananchi. kwa kusema haya hayaniingii akilini kama mkoa una nafasi yoyote ya kuleta maendeleo zaidi ya kuongeza gaharama ya utawala (administrative cost) kwa mwananchi wa chini/kawaida. kimsingi najaribu kuona ni sawa na kuwaongezea kituo cha polisi.
 
Mi sijaona sababu ya kutugawa hovyo ka vipande vya matikiti, uroho wao wa madaraka uishie huko pwani na rukwa ssio huku kwetu mbeya
Wewe ni kidume cha mbegu kwelikweli! Big up.... MADE IN MBEYA!
 
Mi sijaona sababu ya kutugawa hovyo ka vipande vya matikiti, uroho wao wa madaraka uishie huko pwani na rukwa ssio huku kwetu mbeya

Next week tunatakiwa kuhamia Phase Two ya operation hii: ACTION. We need to knock sense into these people. Wenzetu waliopo on the ground kule Mbozi na Ileje wameanza kuchukua hatua kwa mujibu wa taarifa ambazo ninazo. Intelligentsia ya Mkoa wa Mbeya tulioko katika Diaspora ya Mkoa, tunatakiwa kuwaunga mkono wenzetu walioko on the ground kwa kuchukua hatua kuzuwia upuuzi huu. Tusiishie kupost-post tu maneno humu JF. Jaza Vocha kwenye laini yako, hamasisha madiwani, hamasisha wajumbe wa nyumba kumi, hamasisha Walimu wa shule za Msingi na Sekondari, mabibi shamba na mabwana shamba, manesi na Medical assistant wataopata shida sana kusafiri kutoka Itumba, Msia na Idunda kwenda Mkwajuni wapinge ujinga huu --ukiwapa maelezo yanayojitosheleza: Waelekeze kwenye petittion ambayo inaandaliwa kama hawa mbumbumbu watajaribu kutekeleza upuuzi huu.
 
kwa kifupi wazo la kuugawa mkoa wa mbeya ni la kisiasa zaidi, kwani ktk karne hii ya leo tunazungumzia zaidi juu ya kupeleka huduma na mamlaka ya maamuzi juu ya rasmali kwa wananchi kwa kuboresha serikali za mitaa/vitongoji kama ambavyo leo tunaona shule za msingi sekondari za kata zikiwa chini ya umiliki wa wananchi wenyewe. hili limeleta mtazamo mpya zaidi kwa wananchi kuona wanasehemu yao ktk uendeshaji. kwa mtazamo huu ninashawishika sana kama wilaya ya chunya ingegawanywa na kuwa wilaya mbili na hivyo kuiongezea uwezo zaidi wa kupeleka huduma kwa wananchi. kwa kusema haya hayaniingii akilini kama mkoa una nafasi yoyote ya kuleta maendeleo zaidi ya kuongeza gaharama ya utawala (administrative cost) kwa mwananchi wa chini/kawaida. kimsingi najaribu kuona ni sawa na kuwaongezea kituo cha polisi.

Hili nalo neno....
 
Back
Top Bottom