Kuibuka na kufa kwa Merilyn Monroe

Kuibuka na kufa kwa Merilyn Monroe

Chilojnr

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
308
Reaction score
1,354
Unapomzungumzia muigizaji na mwanamuziki, Marilyn Monroe, unamzungumzia msichana mrembo, mwenye uzuri wa kipekee sana kiasi cha kumtetemesha kila mtu aliyekuwa akimwangalia kipindi hicho cha miaka ya 1960.

Uzuri wake ulikuwa gumzo sana kiasi kwamba matajiri na watu wengi maarufu walitamani kuwa naye, kuwa na Monroe miaka hiyo ilikuwa ni ‘title’ kubwa kwa kuwa kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakimmendea, akiwemo Rais J Kennedy na mdogo wake, Robert.

Msichana huyu mrembo alikutwa akiwa amefariki dunia mwezi wa nane nyumbani kwake kwa kujizidishia madawa ya kulevya. Hapa kuna swali, je, ni kweli alijiua ama aliuawa? Na kama aliuawa, nani alimuua? Kwa nini? Kama aliamua kujiua mwenyewe, kwa nini alijiua? Humu nitaelezea kwa undani A mpaka Z kwa kilichotokea, mwisho wa siku utakuwa na majibu yako mwenyewe kama aliuawa ama kujiua.
Hapa kuna theories tofauti kuhusu mauaji yake.

Ya kwanza tuiite...

Agent wa CIA alimuua Monroe.

Mapenzi na siasa.

Ndugu wawili, Kennedy (Brothers)

Mapinduzi ya Cuba.

Unapomzungumzia Marilyn Monroe unamzungumzia msichana maarufu duniani, inawezekana umaarufu wake ulikuwa mkubwa zaidi ya Beyonce wa sasa hivi. Amekufa mwaka 1962 lakini mpaka leo hii watu wanasema alikuwa maarufu sana, na alimsisimua kila mtu.


Tuianze baadaye wiki hiihii. Kama ulikuwa humfahamu huyu msichana mrembo, sasa utamjua kwa undani.

Inaandikwa na Nyemo Chilongani kwa msaada wa makala mbalimbali za kimataifa.
 
Nikakaa mkao wa kula kumbe ni pending na awaiting story. Haya mkuu wacha tusubirie
 
Haku"tetemesha kila mtu" bana, wazungu wanajua ku-hype vitu sana.. wanajua kuuza habari, wanajua kutengeneza mada. they can make business out of nothing,
apo vitaandikwa vitabu, zitachezwa movie, zitatengenezwa conspiracy theory nyingi ili watu wapige hela.

ni kweli alikua mzuri, na kipaji kidogo,
kama tu hawa akina wema na akina hamisa.

dont believe everything they told you.
 
Wale wa picha,mrembo huyo hapo.

Mtoto mzuri sana alikuwa,me mwenyewe ningempiga mingo
JamiiForums1232439152.jpg


Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Sijaona maajabu ya uzuri wake au ile rangi wazungu wanapenda sana kufanya vyao viwe bora hata ukigoogle wasichana wazuri duniani kumkuta mweusi humo ndoto wakati wapo kibao,,,
 
KUIBUKA NA KUFA KWA MONROE.

SEHEMU YA 02.

Ni wakati wa mwaka 1946 Hollywood ilikuwa ikiitwa Hollywoodyland, yaani hata pale mlimani kulipokuwa na majina hayo makubwa palikuwa panasomeka hivyo.

Ni miaka mingi baadaye Monroe alikuwa akizungumzia maisha ya miaka hiyo, jinsi alivyokuwa akipenda sana kuangalia filamu. Alipenda sana kuziangalia na alitamani siku moja angekuwa muigizaji mkubwa tu lakini hakujua ni kwa namna gani angeweza kuigiza.

Kipindi hicho Hollywood ilikuwa ikiendelea kukua kwa kasi. Unajua kwa nini muvi zilianzishwa nchini Marekani? Ama hujui? Acha nikwambie kidogo tu.

Watu walikuwa wakiigiza sana tu, hawakuwa serious kivile ila baada ya uchumi wa dunia kuyumba mwaka 1929, wengi kupoteza ajira, watu walikaa chini na kufikiria ni kitu gani kifanyike, sasa wakaona bora wazingatie muvi kuliko kitu chochote.

Kwa nini?

Ni kwa sababu kupitia filamu, watu waliokuwa na msongo wa mawazo, wagerudi kwenye hali ya kawaida, waliokuwa na hasira za kupoteza ajira, kidogo wangekuwa na furaha baada ya kuburudishwa kwenye televisheni.

Hiyo ilikuwa moja ya sababu iliyoifanya Hollywood kukua kwa kasi sana. Mkazo ukawekwa na mpaka leo hii watu wanapiga pesa sana kupitia filamu.

Monroe anasema muigizaji aliyekuwa akimpenda na kuvutiwa naye alikuwa Jean Harlow. Huyu muigizaji alikuwa na nywele nyeupe kichwani mwake, alikuwa mrembo sana na Monroe alisema endapo angebahatika siku moja kuwa muigizaji, basi angejipa muonekano wa Jean. Na ndivyo alivyofanya.

Ukiachana na Harlow, pia alimpenda sana Clark Gable. Kwa miaka hiyo ukiwazungumzia watu hao, ilikuwa ni sawa na kuwazungumzia mastaa kama Leonardo DiCaprio ama Angeline Jolie kwa miaka hii hapa.

Monroe hakuwahi kufikiria kama kuna siku angekuwa muigizaji mkubwa, alikuwa na kipaji ambacho hakukiona, ni sawa leo mtu anaposema sijui kipaji changu, ila kuna siku unakuja kugundua una uwezo wa kufanya jambo fulani kwa ufasaha sana, ndivyo ilivyokuwa kwa mrembo huyu.

Kabla hatujaendelea zaidi, kuna vitu nitakuwa nakuletea, watu watakuwa wakibuka na kupotea, kote huko ni kutafuta ukweli wa kilichotokea kwa binti huyu. Hebu tuanze na Al Rosen.

Miaka hiyo, kimzungumzia Al Rosen, ulikuwa ukimzungumzia wakala mkubwa sana wa waigizaji wengi. Kila sekta kubwa ilikuwa ni lazima uwe na watu wa kukuunganisha, sasa Rosen alikuwa mmoja wa watu hao, na kulikuwa na waigizaji wengi waliokuwa chini yake kama Cary Grat, Fredrick March, si hao tu bali hata madairekta wakubwa.

So Al Rosen anasema alimfahamu sana Monroe, alikuwa miongoni mwa wasichana warembo mno kipindi hicho. Anasema siri kubwa ya biashara hiyo ilikuwa kila studio walikuwa na utaratibu wao mpaka mtu kupata nafasi, ilikuwa unaandikwa mahali fulani kwanza, wanakufuatilia mpaka pale utakapoanza kufanikiwa.

Kupata nafasi Hollywood haikuwa kazi nyepesi, ilikuwa ni lazima uwe na kipaji. Anasema tofauti na siku hizi, wanawake wanaliwa sana (wanatoa rushwa ya ngono) mpaka kupata nafasi ya kuigiza, haikuwa hivyo enzi hizo.

Kwa miaka hiyo, yaani 1940 soko la Hollywood lilitawaliwa sana na wanawake, na hata baadaye Monroe alipoibuka, alipata nguvu na umaarufu mkubwa sana.

SUGAR DAD ANAMPIGANIA SAS

Sasa sikia! Baada ya kuingia kwenye tasnia ya filamu, mwanaume wa kwanza kabisa kuwa na Monroe alikuwa Johnny Hyde. Huyu jamaa alikuwa wakala mkubwa sana wa majumba na biashara nyingine nchini Marekani.

Mwanaume huyu alikuwa na miaka 53, yaani alimzidi Monroe miaka 30 ila hilo wala hakujali sana, kwenye mapenzi, umri huwa namba tu kama Magazijuto. Mbali na umri mkubwa, ila jamaa alikuwa tajiri mno. Yaani alinuka pesa.

Hyde alikuwa na connection kubwa na watu wa Holywood, mbali na hizo connection pia alikuwa na nguvu kubwa. Mbali na hayo yote, jamaa alikuwa mgonjwa, na daktari alimwambia alikuwa na miezi 18 tu ya kuishi. Alichokifanya, akasema ataimalizia miezi hiyo akiwa na Monroe.

Hata kabla ya Monroe kuwa staa, siku moja akamchukua na kumpeleka kwenye sherehe fulani hivi huko akaanza kumsifia kwa watu kuwa Monroe ana kipaji sana cha kuigiza watu hawakumuelewa waliuelewa uzuri wake tu.

Hyde hakutaka kukubali. Alichohitaji ni kumfanya Monroe kuwa staa mkubwa wa filamu. Akiwa nyumbani kwake akampigia simu dairekta mkubwa tu aitwaye John Huston ambaye aliongoza muvi kali miaka hiyo. Hyde akamwambia kuhusu demu wake yaani Monroe ampe nafasi aigize ili aonyeshe alichokuwanacho.

Huston akakubali.

Hyde akamchukua Monroe na kumpeleka katika Studio ya Metro akamkutanisha naye. Jamaa alivutiwa na Monroe, alichokifanya akampa script ya kwenda kuifanyia kazi, Monroe akaichukua na kuondoka, baada ya siku mbili, akarudi na kuonyesha kile alichokifanyia kazi kwa siku hizo. Kila mtu akavutiwa na uwezo wake kwenye hiyo script.

Akakubalika na hivyo Huston kumwambia angekuwa miongoni mwa waigizaji kwenye filamu ya In The Asphalt Jungle. Huston anasema siku ya kwanza kuwa locaton, uwezo alioonyesha Monroe ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kumvutia kila mtu. Hiyo ilikuwa mwaka 1952.

Sasa hapo ndipo alipoanza kupata jina lake, kutengeneza ulimwengu wake wa kipekee. Hata zilipokuwa zikiandaliwa tuzo mbalimbali, alikuwa akipigiwa kama Muigizaji Bora wa Filamu Marekani.

Kutokana na uzuri wake, majarida mbalimbali yakaanza kufanya naye kazi, picha zake zikaonekana ukurasa wa mbele kabisa. Kwa miaka hiyo, Monroe akaanza kuwa gumzo kila kona, umaarufu ukaongezeka, umaarufu ambao uliopelekea kifo chake.

Unajua nini kiliendelea katika maisha ya Monroe? Kumbuka hii ni simulizi ya maisha ya kweli ya msichana maarufu sana duniani aliyetembea na rais wa Marekani na kuuawa.

Itaendelea.
 
Nina
Haku"tetemesha kila mtu" bana, wazungu wanajua ku-hype vitu sana.. wanajua kuuza habari, wanajua kutengeneza mada. they can make business out of nothing,
apo vitaandikwa vitabu, zitachezwa movie, zitatengenezwa conspiracy theory nyingi ili watu wapige hela.

ni kweli alikua mzuri, na kipaji kidogo,
kama tu hawa akina wema na akina hamisa.

dont believe everything they told you.
Ninazo Novel mbili za Marilyn Monroe, search Hilo Jina huko Facebook na Google utamwona,ni maarufu kuliko unavyofikiria
 
Back
Top Bottom