Kuibiwa Nyota Kupoje?

Ujue hizi thread mnaanzisha ndio maana mnatapeliwa humu achaga kuamini vitu kama hivyo uchawi ni psychological sense acha kujishuku kuwa unarogwa ! Na hali ilivyo huko akina Mtu mzito watawapata Wateja wengi Sana.
 
Soma ufunuo wa yohana 5:12 utaona nyota 7 ambazo kila mwanadamu anapozaliwa huja na nyota hizo ambazo hupewa na MUNGU BABA . nahivyo wachawi,waganga na washirikina hukuibia utotoni hata ukubwani na kuzitumia wao na kukuacha wewe ukitaabika hat kama umesoma vipi na wanafanya hivyo kwa kutumia ulimwengu
 
Kuibiwa nyota ipi sasa nyota ya kijani ama hizi tuzionazo angani? Unaibiwa tuu kama kuibiwa mke/mme au simu.
 
Yaani ni kama vile YANGA alivyotaka kuchukuliwa Ngoma na Simba, kule ndo kuibiwa
nyota au Hassan Kessy alivyochukuliwa na yanga kabla ya mkataba hapo ina maanayanga
waliiba nyota kutoka simba.
 
Kuibiwa nyota ni sawa na kuibiwa pesa nk na ndio mtindo wa kila siku wa watu wakishirikiana na ulimwengu wa giza. Ukijua nini kinachoendelea kuhusu wizi wa nyota, destiny, pesa, uzuri, nk utashangaa mpaka chini! Lakini ndio uchumi wa "watu fulani" huo. Lakini pia ukijua ukweli huu utajinda kama mboni ya jicho lako, na hapo ndio mwanzo wa mafanikio yako, KUJILINDA NA WEZI katika ulimwengu wa roho. Unamwitaji MUUMBA WA ULIMWENGU kuweza kufanya hivyo! Yupo tayari kukusaidia.
 
Kweli
 
Back
Top Bottom