Kuhutubia Wakimbizi: Mahakama wilayani Mpanda yamkuta Masha na Viongozi wa CHADEMA hawana hatia

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,399

CoXwkWEXgAA96Ro.jpg:large


Mahakama ya Wilaya, Mpanda imemkuta Mh. Lawrence Kego Masha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana Mwanza pamoja na washtakiwa wengi ambao ni Viongozi wa Chadema Jimbo la Nsimbo, Katavi kutokuwa na hatia katika makosa mawili ya Kula Njama Ili Kutenda Kosa na Kuhutubia Wakimbizi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kosa lingine la kuingia makazi ya Wakimbizi bila Kibali.


Mahakama imesema kwamba upande wa mwendesha mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wowote unaonyesha kwamba washtakiwa hao walikutana na kupanga njama kutenda kosa. Pia hakuna ushahidi wowote kuonyesha kwamba washtakiwa walikamatwa wakihutubia wakimbizi.

Ila Mahakama iliona kwamba washtakiwa hao wana kosa la kujibu kwa shtaka la kuingia kwenye kambi/makazi ya wakimbizi bila kibali. Mara baada ya uamuzi huo washtakiwa walitakiwa kutoa utetezi wao ambapo washtakiwa Lawrence Masha na Stansalaus Kaswele walitoa utetezi wakiongozwa na Wakili Albert Msando.

Leo Mahakama imetoa hukumu na kusema kwamba washtakiwa wote saba hawana hatia kwa kukubaliana na hoja zote za Wakili wa Utetezi. Hivyo washtakiwa wako huru.

Chanzo: Wakili Msomi Albert Msando
 
Baada ya siku chache watarudi CCM.?? Walisahau hiyo sente....
 
Back
Top Bottom