"Ujinga ni kuendelea na Uchaguzi kwa Tume ileile na namna ileile huku ukitegemea matokeo tofauti"
- Albeit Einstein
Nimekupata Mkuu wangu, uko sahihi sana 100%.Shark;
Msimamo wangu hapa jukwaani ni kuwaunga mkono CUF na msimamo wao wa kuwaachia CCM waendelee na marudio ya uchaguzi wao chini ya Jecha wao;
Au, kama ni uchaguzi mwingine basi kwa hii ZEC chin Jecha kupigwa chini kisha awepo msimamizi huru wa uchaguzi wa mwingine mpya!
Hapa tunajadili kauli ya Rais wa JMT bwana JPM ya "nitaendelea kukaa kimya kuhusu kile kinachoendelea Zanzibar".
Ndo nikasema si afadhali hata angesema serikali za JMT na SMZ zinaendelea kulifanyia kazi ikiwemo kushauriana na CUF kukubali kushiriki wa uchaguzi wa marudio japo tunatambua na tunajua hawezi kuwashawishi kushiriki hiki kiitwacho na Jecha "uchaguzi wa marudio" kwa sbb ambazo ziko wazi!!
sasa huo usuluhisho unakujaje ikiwa maalim seif 'ameweka mpira kwapani, na kutoka uwanjani'? hataki mazungumzo ameshajitoa, wakisema uchaguz urudiwe hataki pia, hv unafikir kwa situation kama hyo, unataka maguful afanyaje?Kama sisi tunavyojitolea kuwasuluhisha wengine e.g. S Sudan, Burundi, Kenya, DRC , Cote de Voire etc. INATAKIWA NA SISI TUSULUHISHWE TUSIONE AIBU. Wenzetu huko walipopata shida viongozi wetu walikwenda mbio kuomba kuwasuluhisha, lakini hapa nyumbani hao hao hawataki suluhu AJABU
Watawala wameshasema hawataki kutawaliwa na vyama vya hovyo hovyo unategemea Magufuli aseme nini zaidi.
Hana uwezo wa kuingilia mgogoro ila ana uwezo wa kuleta majeshi kutuliza mgogoro huo?ok fine sasa tunamwambia magu na ccm wenzake tanganyika wauweni wazanzibar wote ila kwa hili wala hawatorudi nyuma.Magufuli yupo sahihi kwa sababu hizi
1. Katiba ya Zanzibar haimpi uhuru na nguvu ya kuingilia mambo ya ndani. Maalim Seif na timu yake ndio waliopeleka pendekezo hilo ili kuikomoa Bara.
2. Tume ya uchaguzi imepewa uwezo wa kutohojiwa hata na Rais katika maamuzi yake. Hili ni pendekezo la Jussa ili kuidhibiti Bara isitie mkono.
3. Katiba ya Muungano inampa Rais mamlaka ya kuangalia usalama wa Jamhuri ya Muungano, kwa kutumia eneo hilo, Rais anaweza kuingia Zanzibar na kuhakikisha hakuna amani inayovunjwa.
Mlitaka Rais aseme nitashughulikia mambo ya ndani ya Zanzibar yanayohusu uchaguzi ndani ya tume wakati hana huo uwezo? Rais yupo straight ndo maana wanaopenda kusikia kauli za kupambwa hawazipendi.
Mwacheni Rais afanye yale ambayo yako ndani ya mamlaka yake. Vile vile tujifunze kusikia na kuyachambua yale anayesema hata kama
hamyapendi.
Nimekupata Mkuu wangu, uko sahihi sana 100%.
Uchaguzi uliharibika kwa makosa yaliyoko chini ya Tume, kuurudia kwa Tume ilele huku kukiwepo hakuna aliewajibishwa ndani ya Tume ni Usanii.
Ila kwa upande mwengine naona kama Bwana Magu uwezo wake ni mdogo sana compare to level ya huu Mgogoro wa Zanzibar. Ikitokea Uchaguzi ukarudiwa basi ni faida kubwa kwa CCM ambayo yeye Magu hana hata cheo cha ukatibu tarafa pale Chamani. Wenye chama chao ambao yeye yuko chini yao ndio wanaotaka uchaguzi urudiwe, yeye pale hawezi kwenda kinyume na matakwa ya Chama.
Ni ajabu kama Rais hajui kuwa maamuzi ya Tume hayajadiliwi mahakamaniLakin si amesema hasiyeridhika aende mahakaman
Binafsi namuunga mkono JPM kwa mambo mengi anayofanya. Kama ni kumpa ranking kati ya 1 na 10 amnapo 10 ni alama ya juu kabisa na 1 ya chini ningempa 9. Ila kwa jinsi anavyoshughulikia suala la Znz ningempa 1!Jana katika Hotuba yake kwa wazee wa Dar Rais magufuli alitusisimua wengi (kama kawaida yake) kwa jinsi alivyodhamiria yeye na serikali yake kuondoa ufisadpi na kuleta maendeleo kwa watanzania wanyonge. Hata hivyo kuhusu Zanzibar amekosea. Amesema hataingilia. Anakosea kwa sababu nne:
1. Si kila mzozo, na hasa zaidi mizozo ya kisia inasuluhishwa kwa sheria. Pale sheria inaposhindwa kuleta haki au kuwafanya watu wajisikie wanatendewa haki basi mazungumzo hufanyika ili pande zote zilidhike kwa ajili ya usitawi wa nchi na amani. Binafsi naunga mkono sana kurudiwa kwa uchaguzi. Sioni njia nyingine practical ya kumaliza mzozo huu. Hata hivyo CUF wanapaswa waridhie. Uchaguzi hauwezi kuwa wa chama kimoja.
2. Sheria zinawekwa na watu na zinabadilishwa mara kwa mara. Tuna tatizo la katiba na baadhi ya sheria zetu. Kwa sababu hiyo (inawezekana) watu hawajaenda mahakamani kwa vile wanajua uamzi wa mahakama hautatoa suluhisho sahihi.
3. Tume ya Uchaguzi iko huru na haipaswi kuingiliwa - huo ni mtazamo chanya sana na wakupongezwa. Lakini kwa upande mwingine tume inaongozwa na watu na sio malaika. Kwa mfano kama Salum Jecha alifuta matokeo kwa shinikizo au mapenzi yake kwa CCM, je hapo heshima ya uhuru wa tume itasaidia?
4. Kuna hatari (Rais asipoingilia kwa ushawishi) CUF wakasusia uchaguzi. Naiita hatari kwa vile yalitokea siku za nyuma tunayajua. Kuweka majeshi aisaidii sana. Amani ya kweli hailetwi na majeshi. Watu watakaa kimya kwa woga lakini hawatapendana, hawatashirikiana, hawatashiriki kutekeleza mipango ya maendeleo. Siku wakikosa uvumilivu damu inaweza kumwagwa na majeshi yaliyowazunguka!!! Mungu apishe mbali lakini jambo hili limetokea wakati wa Rais Mkapa. Sio hypothesis.
Utafiti wa Citizen (Magufuli impresses many after 100 days ) umeonyesha karibu 50% ya watanzania hawaungi mkono rais anavyoshughulikia suala la Zanzibar. Bado ana muda. Anaweza kufanya kitu.
Hayo unasema weww, yeye hakjsema hivyo.Tatizo lililopo upinzani mnataka atoe tamko msikie mtazamo wake, HATOFANYA HIVYO. Behind the scene, sio kwamba amekaa tu, anashughulikia hilo suala, Mama Samia yuko bize na hiyo issue, kama mnataka rais aite waandishi alafu aseme, hiyo haitatokea kamwe. Atakaa kimya!
Keep it up!Magufuli yupo sahihi kwa sababu hizi
1. Katiba ya Zanzibar haimpi uhuru na nguvu ya kuingilia mambo ya ndani. Maalim Seif na timu yake ndio waliopeleka pendekezo hilo ili kuikomoa Bara.
2. Tume ya uchaguzi imepewa uwezo wa kutohojiwa hata na Rais katika maamuzi yake. Hili ni pendekezo la Jussa ili kuidhibiti Bara isitie mkono.
3. Katiba ya Muungano inampa Rais mamlaka ya kuangalia usalama wa Jamhuri ya Muungano, kwa kutumia eneo hilo, Rais anaweza kuingia Zanzibar na kuhakikisha hakuna amani inayovunjwa.
Mlitaka Rais aseme nitashughulikia mambo ya ndani ya Zanzibar yanayohusu uchaguzi ndani ya tume wakati hana huo uwezo? Rais yupo straight ndo maana wanaopenda kusikia kauli za kupambwa hawazipendi.
Mwacheni Rais afanye yale ambayo yako ndani ya mamlaka yake. Vile vile tujifunze kusikia na kuyachambua yale anayesema hata kama hamyapendi.