Rulleger
Member
- Aug 29, 2015
- 84
- 60
Jana katika Hotuba yake kwa wazee wa Dar Rais magufuli alitusisimua wengi (kama kawaida yake) kwa jinsi alivyodhamiria yeye na serikali yake kuondoa ufisadpi na kuleta maendeleo kwa watanzania wanyonge. Hata hivyo kuhusu Zanzibar amekosea. Amesema hataingilia. Anakosea kwa sababu nne:
1. Si kila mzozo, na hasa zaidi mizozo ya kisia inasuluhishwa kwa sheria. Pale sheria inaposhindwa kuleta haki au kuwafanya watu wajisikie wanatendewa haki basi mazungumzo hufanyika ili pande zote zilidhike kwa ajili ya usitawi wa nchi na amani. Binafsi naunga mkono sana kurudiwa kwa uchaguzi. Sioni njia nyingine practical ya kumaliza mzozo huu. Hata hivyo CUF wanapaswa waridhie. Uchaguzi hauwezi kuwa wa chama kimoja.
2. Sheria zinawekwa na watu na zinabadilishwa mara kwa mara. Tuna tatizo la katiba na baadhi ya sheria zetu. Kwa sababu hiyo (inawezekana) watu hawajaenda mahakamani kwa vile wanajua uamzi wa mahakama hautatoa suluhisho sahihi.
3. Tume ya Uchaguzi iko huru na haipaswi kuingiliwa - huo ni mtazamo chanya sana na wakupongezwa. Lakini kwa upande mwingine tume inaongozwa na watu na sio malaika. Kwa mfano kama Salum Jecha alifuta matokeo kwa shinikizo au mapenzi yake kwa CCM, je hapo heshima ya uhuru wa tume itasaidia?
4. Kuna hatari (Rais asipoingilia kwa ushawishi) CUF wakasusia uchaguzi. Naiita hatari kwa vile yalitokea siku za nyuma tunayajua. Kuweka majeshi aisaidii sana. Amani ya kweli hailetwi na majeshi. Watu watakaa kimya kwa woga lakini hawatapendana, hawatashirikiana, hawatashiriki kutekeleza mipango ya maendeleo. Siku wakikosa uvumilivu damu inaweza kumwagwa na majeshi yaliyowazunguka!!! Mungu apishe mbali lakini jambo hili limetokea wakati wa Rais Mkapa. Sio hypothesis.
Utafiti wa Citizen (Magufuli impresses many after 100 days ) umeonyesha karibu 50% ya watanzania hawaungi mkono rais anavyoshughulikia suala la Zanzibar. Bado ana muda. Anaweza kufanya kitu.