Kuhusu utaifa

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Tuna maswali kadhaa ya kujiuliza je demokrasia ni kubadilisha utawala mmoja na kwenda mwingine kwa njia ya kura? mantiki nzima ya demokrasia iko katika hili tu au ni zaidi ya hapo? je demokrasia ni utamaduni fulani wa watu wanavyofikiri na kutenda na kuendesha maisha yao ya kila siku mbali ya kuchagua na kuchaguliwa? Demokrasia ni nini haswa? Ni kuwa na uhuru wa kuongea bila mipaka na watu kuwa na vyama vingi vya kisiasa bila mipaka? Vipi kuhusu tabia na mienendo ya watu ? kuna tabia ya kidemokrasia na isiyo ya kidemokrasia kwa watu? Je tunawapa muda watu kuongea na kuwasikiliza kwa umakini au tunawakandamiza bila hata kuwasikiliza? Tunaitumia demokrasia for evil purpose or for good purpose? Je ni kweli ndoto yetu ni kujenga good society and people who are capable of doing good deeds?

Kwa maoni Yangu ni kweli demokrasia huwezi kuitenganisha na uhuru wa watu, na inawajibika kuwafanya watu kuwa hivyo. Lakini uhuru huu ni mgumu kupatikana pasipo kujenga jamii ya watu wenye nidhamu. Ama sivyo demokrasia haiwezi kuwa na maana kwetu, zaidi ya kuwa chanzo cha mgawanyiko katika taifa na ku create confusion.

kwahiyo demokrasia inahitaji discipline ambayo haiwezi kupatikana nje ya watu wenyewe wanaounda taifa bali ndani yao. Kuwawezesha watu kuwa na uwezo wa kujenga hoja na kusikilizana na kujua aina ya jamii na taifa tunalotaka kulijenga. Kujitawala kunaanza na mtu mmoja mmoja kwanza alafu taifa.

Kama watu wetu wanashindwa kujitawala wenyewe binafsi hatutaweza kujitawala kama taifa kwa ufanisi. Bila ya hivyo watu wetu hawatoweza kufanya maamuzi sahihi na yenye tija kwa taifa. Wataendekeza ubinafsi na sio utaifa na demokrasia itatumika kama tool ya kuendeleza ubinafsi huo. Katika mfumo wowote wa kisiasa ulio bora lazima uwe na malengo ya ku create order, Kwakuwa pasipo order hakuna maendeleo yeyote ya kweli yatakayofikiwa. Order and harmony ni nguzo ya maendeleo ya taifa lolote. Kama watu hawawezi kusikilizana watawezaje kupata maendeleo? Kwahiyo hii self regulation ya watu namaanisha raia ni muhimu sana kwa stability ya nchi. Hatuwezi kufanya watu wetu kujitambua kwa taifa lao kama akili zao bado zimejawa ubinafsi na kama hazina malengo ya kitaifa. Corruption and self oriented people ni pacha.

Demokrasia inahitaji watu waliopevuka wenye nidhamu ya kujiongoza na kiendesha, Watu wenye uwezo wa kufikiri kwa kujenga hoja na wanaoweka maslahi ya umma mbele kuliko yale ya ubinafsi. Nje ya hapo for unthinking community ni ujinga na fujo. It need self regulation. Bila ya watu kuwa na uwezo wa kutawala tabia zao demokrasia haiwezi kufanya kazi. Bila watu kujua Right and wrong demokrasia ni fujo. Watu hawatoweza kuelewana. Kwenye siasa kutajaa wenye fitna, walaghai, wachonganishi, watafanya chochote ili kupata vyeo na mali kama mioyo yao haijajengwa kwenye principals na taifa litavurugwa haswa kwasababu their principal is Mali, vyeo na umaarufu na anasa. Tunapozungumza uongozi sio kuwapa watu mkate tu (uchumi) bali kuongoza watu kwenye njia sahihi ( we must give them MANNA) Binadamu sio mwili peke yake . Muendelezo wa taifa letu unategemea sana Decisions zetu ni sahihi kwa kiwango gani. Na umoja wetu pia unategemea hilo. Haki za watu zinategemea hilo. Uongozi unategemea ubora wa maamuzi ambao huamua fate ya mataifa. Hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya kwa taifa au kwa mtu. Ni matokeo ya maamuzi. Kwahiyo majaliwa yetu yanategemea aina za viongozi tunaochagua. Je watalinda haki zetu? watadumisha umoja na mshikamano?

Kama hatuna ramani hatuwezi kufika tunapotaka kwenda kwasababu kujenga taifa sio kuwa na madaraja mengi, majengo ya maghorofa kuwa na ndege nyingi nk Taifa linaundwa na watu na linatakiwa kujengwa huko kwanza kwa kujenga mahusiano yetu. Any wise leader anajua hili.

Kama taifa mahusiano yake yako broke kuanzia huko kwenye familia kuja juu katika ngazi ya utaifa tusifikirie amani itakuwepo. If we are not look each other as brothers, how can we cooperate? Nadhani inabidi tujifikirie upya kwanini tuko taifa na malengo yetu ni yapi? and if we are truly liberated. Tuna kikundi cha watu kinachotutawala na hawataki ku create aina hii ya taifa. Most of them are very selfish. Na kamwe hatutaweza kujenga taifa la kidemokrasia pasipo uhuru na uhuru huletwa na self regulation. We must regulate our appetites and act with justice. Kamwe hatuwezi kupata ahueni tukiwa na aina hii ya fikra na kamwe kama taifa hatutaweza kuwa na furaha badala yake anasa tutaiita furaha huku roho zetu zikinyong'onyea kwa huzuni.

Tunaweza kujiita sisi ni taifa pengine tukawa sio. Tukawa kundi la watu tu wanaoishi pamoja kila mtu na interest zake na hatuna common bond inayotuunganisha. Kila mtu anaishi kivyake na ubinafsi wake. Na tuna serikali inayoahidi ulinzi tu wa mali za watu lakini haina common bond na watawaliwa. watawaliwa ni just subjects and they don't have real freedom. Na kila mtu akawa anaangalia interest ya group lake. but we need to meet at the centre. wote tuna majukumu yetu lakini linapokuja suala la utaifa we must meet at the centre. Pengine tunapaswa ku reflect kwanini tuko pamoja kama taifa? Values gani zinatuweka pamoja na ni nini spirations zetu kama taifa. Au ni kupata mkate wetu wa kila siku tu?

We can have anything in our country kama hatutajenga mahusiano yetu vyema ni kama hakuna kitu. Kama hatutoheshimiana na kupendana is nothing.
 
Back
Top Bottom