kuhusu ugonjwa wa moyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kuhusu ugonjwa wa moyo

Discussion in 'JF Doctor' started by Hardman, Jun 18, 2012.

 1. H

  Hardman JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 597
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 60
  Wakuu,
  kutokana na uchunguzi mdogo niloufanya nimegundua kuwa siku za hivi karibuni kumekuwa na idadi kubwa ya watu(hapa Tanzania) kufa kwa ugonjwa wa moyo......so nilikuwa naomba kujuzwa vyanzo vya ugonjwa huu na namna ambavyo tunaweza kujizuia nao...:help:
   
 2. k

  kamili JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Zipo sababu nyingi lakini mbili za muhimu zaidi, 1st uwezo wa ugunduzi wa ugonjwa huo umeongezeka sana, kwa sababu madaktari, vituo vya huduma na vifaa vimeongezeka sana mpaka vijijini.

  Zamani mtu aliweza kuuguma labda mpaka kifo bila ya kujulikana shida yake,labda wale wachache ambao walikuwa na uwezo na ufahamu wa kwenda kwenye vituo vikubwa.

  2nd mfumo wa maisha umebadilika na hivyo magonjwa nayo yamebadilika (mfumo wa maisha ni maana ya shughuli na vyakula) kwa hiyo tumeanza kuachana na kuugua magonjwa ya kimaskini kama minyoo, upele, kwashakor, malaria nk. na tumeanza kuugua magonjwa kama uzito uliozidi (obesity) hypertension, diabetic, renal diseases nk. hayo yote yanaleta magonjwa ya moyo.

  Ukiangalia riport za zamani za nchi tajiri utashangaa kuona hata wao kabla ya kuendelea waliugua magonjwa kama malaria, minyoo nk. lakini baada ya kuendelea kwa sasa wanaougua magonjwa ya aina ingine ikiwemo ugonjwa wa moyo.

  Jinsi ya kujikinga ni pamoja kufanya mazoezi ya kutosha,kula vyakula kwa kipimo na kwa wakati maalum (achana na mara chips, mara soda, mara biskuti mara chokolate nk), kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi, kuchunguzwa mara kwa mara na wataalamu na kutibiwa kwa haraka kasoro zote zitakazoonekana
   
Loading...