Yani hujiulizi kuna nini Leo hii Hadi Diamond na dharau zake anahofia kuwa Kiba ananunua views? Naomba nikujibu Diamond anaijua nguvu ya Alikiba vizuri Sana Ila pia yeye anajua kuyatumia madhaifu ya Alikiba Kwa miaka nenda Rudi Ila kama nilivotoka kusema juu kuwa hawa jamaa Wana mtaji wa watu Ila lifestyle zao ndio zinafanya Kiba aendelee kuwa Kiba na Diamond ataendelea kuwa diamond Platnumz
kuna wakati inatokea Mambo yanabuma hiyo ipo kwenye kila kitu ndo kilichomtokea Diamond Kwa hivi sasa, kuna wimbo mwingine ambao kauweka kwenye Chanel yake ya YouTube ambao ni audio kashirikishwa na masterclaft Leo ni siku ya 3 Ila Una viewers laki 3 napo hujiulizi imekuaje account yenye subscribers 5ml wimbo unakaa siku 3 Una laki 3? So shit happens bro
ila anataka kuwaaminisha mashabiki wake kuwa Kiba ananunua views Jambo ambalo halina mashiko, na kitu kingine we kama kweli mfatiliaji wa issue za kununua views basi ulijionea kwenye nyimbo ya kondeboy, wimbo ulikosa flow ya kutuaminisha kuwa hanunui viewers ilikuwa ndani ya dkk 30 unaona viewers laki 7 wameongezeka Ila Kwa kiba flow yake mbona inaeleweka unless kama utafata mihemko ya kishabiki
Trust me katika wasanii ambao waga hawajali issue za views basi Alikiba namba 1, jamaa pamoja na kujua ana nguvu ya watu ila ashagaridhika na Aina ya maisha aliyonayo so hafanyi kushindana ata siku moja, but Kwa Diamond everything kwake ni ushindani, atashindana ata na akina Marioo ilmradi Tu ajiridhishe he's on top of everyone
Na kuweka records Sawa Sawa kabla haya Mambo ya record za views wengi ndani ya muda mfupi hayajatanda Moto Sana, msanii wa Kwanza kupata views 1ml ndani ya masaa 24 Alikuwa Alikiba na wimbo wake wa seduce, ambapo akafanya Diamond akatoa Ile collabo ya WCB yote siikumbuki jina wakiwa wameact km wazee wa zamani ili kuuzima ule Moto Ila ikashindikana na baada ya hapo ndio Diamond swala la viewers kwake likawa ushindani rasmi na anaweka record na kuzivunja mwenyewe