Kuhusu tatizo la nidhamu

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Ili taifa lolote liendelee haina budi watu wake wawe na nidhamu. Kukosekana kwa nidhamu katika taifa ni hatua moja kubwa kwa taifa lolote kujinyima maendeleo yake. Na sisi kama taifa ni lazima tukubali tuna tatizo hilo sio kwa viongozi na sio kwa raia. Na kwa hakika hatutaweza kuwa na dira kama taifa pasipo uwepo wa nidhamu. Nidhamu ni ufunguo kwa taifa, kwa familia na kwa mtu binafsi kuendelea.

Nidhamu huleta mpangilio na kinyume chake ni vurugu na fujo. Kunapokosekana nidhamu katika nyumba Baba hamheshimu mama, mtoto hana utii na haijulikani nani mkubwa na nani mtoto katika nyumba; sidhani kama familia hiyo itakuwa na utulivu na maendeleo ya kweli. Na kama baba pia hajiheshimu na kuheshimu wengine vile vile ni tatizo. Hili ni sawa pia katika nchi. A president must watch himself carefuly not to act without discipline. Heshima hailetwi na cheo bali how you conduct yourself.

Nguvu ya familia inategemea umoja wa watu wake ni sawa na kwa taifa. Kwahiyo kunapokuwepo na nidhamu ya watu kuweza kujiongoza na kutenda mambo sahihi wenyewe, ni hatua moja kubwa mno.

Hakuna serikali itakayoheshimiwa na raia wake kama hakuna nidhamu. Na kusema kweli raia wanapaswa kuipenda serikali yao ikiwa tu serikali hiyo itakuwa na uwezo wa kuonyesha nidhamu na uadilifu.

Kama watu wanaoongoza serikali wakishindwa kujitawala wenyewe na kujizuia kutenda mambo yasiyo sahihi watawezaje kutawala raia ? Utawala unahitaji nidhamu ya hali ya juu. You can not control others if you dont have ability to control yourself. Kama unashindwa ku control unachozungumza to the public, kama unashindwa ku control tabia yako, hisia na matamanio yako na kuyaongoza katika mkondo unaofaa you are unfit to be a leader.

Sehemu yeyyote ya watu wenye nidhamu huheshimiana na kuwa tayari kushirikiana kama hakuna kuheshimiana watu hawawezi kushirikiana. Tukiheshimu utu wa mtu mwingine watu watakuwa tayari kujitoa na kushirikiana. Ubinafsi ni ujinga there is more we can gain kama taifa kama tukishirikiana kuliko kuwa wabinafsi.

Kwahiyo nataka kusema tabia ni muhimu sana katika uendeshaji wa taifa. Maendeleo yetu yanategemea haswa tuna raia wa tabia gani. Na lengo moja la elimu ni kujenga tabia ya kufikiri na kuwa na nidhamu ku regulate hulka zetu za choyo, ulafi , ubinafsi , wizi , ulaghai nk, na kumfanya binadamu kuwa bora na mwenye faida kwa taifa lake.

The aim of education is to eliminate evil in society na kumpatia mwanadamu uwezo wa kisayansi wa kutawala mazingira yake (skills za kazi ) kama elimu yetu haijengi character na kumpatia maarifa ya kutosha binadamu kutawala mazingira yake haitufai. They must know all wrongs and avoid it. then our country will be the best in everything. Lazima wajue umalaya ni kosa, wizi ni kosa and any other bad behaviour. Hakuna taifa litakaloendelea pasipo values. People who are truthful and honest only can build a great country.

Kwahiyo miongoni mwa nidhamu ni uwezo wa kuzuia au ku control midomo yetu kwa kuongea yale tu sahihi na yenye kujenga kwa wengine kwa kuwapa maarifa na kuwaendeleza na kuwakuza kuwa watu bora.

Hatuwezi kuendelea kama asilimia 80% tunayosikia kwenye radio na kwenye vijiwe sio yenye kumjenga mtu na kumkuza. Na tunadhani tunajenga taifa la namna gani na national character ya namna gani? We need reformation. We must renew our minds. Our thought is what build this country. inategemea tuna fikra za namna gani na tunalishana pia fikra za namna gani. If we change direction of our thoughts things will be better. And if you ask me, I see great potential for this country to be amongs the great.

Lazima tujenge taswira nzuri ya taifa letu na taswira nzuri ya taifa letu itajengwa na tabia zetu. Na heshima yetu pia kama taifa inategemea hilo. Na hili hatutafanikiwa pasipokufanya jitihada za kuwa hivyo. Vijana wa taifa hili huu ni ujumbe wenu tunaweza kubadili taifa hili kama tutabadilika tunavyofikiri na tunavyoishi.

Kwa wanasiasa lazima watambue kwamba malengo yoyote ambayo wanataka wayafikie kwa manufaa ya nchi yanategemea watu. Ni watu ndio wanaofanya kazi kuletea taifa maendeleo kama hawana uzalendo na kama hawana umoja hakuna malengo tutakayofikia. Tunatumiaje nguvu kazi ambayo tunayo?

Swali ni kwamba watu hao unawatayarishaje kuyafikia malengo hayo ya taifa? Au unawatumia kwa manufaa yako binafsi na kuwafanya na wao kuwa wabinafsi zaidi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom