KUHUSU KUZAA KWA MKATABA

Je umewaza jinsi mwanao huyo akikuwa atakavyojisikia vibaya kuwa ulizaa na mwanamke kwa malipo ili apatikane as if kama ni bidhaa fulani umeenda kununua dukani.
 
Mkuu umeongea vizuri sana,nina uwezo wa kutosha wa kuhakikisha mama wa mtoto wangu anaishi vizuri kwa kipindi chote miaka miwili pamoja na mtoto wangu
nilijaribu kuwapa mwongozo kdg,,,,, nna hakika PM umepata za kutosha....usiwe mchoyo kimya kimya
 
Sheria inasema baba waweza kabiziwa Mtoto Mara afikishapo umri was miaka 7 na kuendelea
Unaweza fanikiwa na kutimiza lengo lako lakini vipi je umefikiri kuhusu mtoto, maisha ya kukaa bila mama yake na kupata malezi na upendo wake baada ya hio miaka miwili
 
nimepata mkuu,ntakuagizia!
Hii kitu si rahisi kama tudhaniavyo. Kwanza lazima huyo mama awe ashazaa. Pili kuna hatari iwapo yai ni lakwake, huwezi kumpata kirahisi. Kama unataka mtoto na usipate usumbufu, fanya IVF na utimize masharti ya IVF ambayo ni kuwa wewe hupaswi kuona sura yake au kufahamu jina. Ni daktari pekee anayetakiwa kukujua wewe na huyo surrogate mother wa mtoto wako. Unashauriwa yai litoke kwa donor si kwake la sivyo pesa yako itaishia mahakamani kwa maloya
 
Mkuu wanawake wa kiafrica hawaelewi mambo ya mikataba wala hawajui nini maana yake!cha msingi usipoteze muda wewe piga mimba kimya kimya hudumia mtoto akizaliwa na kufikisha umri unaona utaweza kumtunza mwenyewe pita nae kama watu walivyopita na mo
 
Sheria tz haziruhusu
 
Wanawake wa kibongo ukiongelea mkataba wanajifanya wakali balaa na kutoa experience za maumivu ya labor.
Wakati wengi wamepewa mimba wameachiwa watoto hata mia hawapati kutoka kwa baba wa hao watoto.
Sasa si Bora mnayeelewana tangu mwanzo!!
 
Wanawake wa kibongo ukiongelea mkataba wanajifanya wakali balaa na kutoa experience za maumivu ya labor.
Wakati wengi wamepewa mimba wameachiwa watoto hata mia hawapati kutoka kwa baba wa hao watoto.
Sasa si Bora mnayeelewana tangu mwanzo!!
Inatokea tu hatufanyi kwa kupanga, na wengi tunatamani mambo yangekuwa tofauti na yalivyo
 
Tangu muambiwe mfyatue tu watoto watasomeshwa bure, naona kuna mlioamua kufungua viwanda kabisaa vya kufyatulia hao watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…