Kuhusu hili la mimba kwa wanafunzi

DENLSON

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
381
500
Baada ya kumsikiliza Mh Rais kwa umakini na kwa tafakari kubwa nimeona kuna kasoro kubwa ambayo ipo katika sera na sheria zetu kama nchi hasa kuhusu masuala haya ya haki za jinsia

Napenda niende moja kwa moja alichosema Rais leo ni sawa kabisa hata mimi siwezi kusomesha mtu aliyezaa akiwa shule tatizo linakuja sio wote walio pata mimba shuleni walipenda, wengine walibakwa na wengine ni kutokana na changamoto za kiuchumi na kijamii ikiwepo ukosefu wa mabweni shuleni, umbali kutoka nyumbani, ugumu wa maisha na hata ushawishi wa aliyempa mimba.

Sasa basi katika hili sera na sheria zetu ikatoa adhabu sio tu kwa aliyebeba mimba na aliyempa mwenzie mimba bali kwa wote hata na wasio husika

Ntaelezea wasio husika ni kina nani

Mzazi, huyu anaweza kuhusika au asihusike lakini sheria inamudhibu

Mtoto atakaye zaliwa katika hali ya kawaida huyu ahusiki hata kidogo juu ya makosa ya baba au mama yake lakini sheria inamudhibu vikali tena pengine kuliko wote. Kwanini nitaeleza

Hebu fikiria wanafunzi wawili wa kike na wakiume wana mahusiano ya kimapenzi Mwanafunzi wa kike akipata mimba atafukuzwa shule na yule wakiume atafungwa miaka 30. Maana yake mtoto atakaye zaliwa atakuwa na mama kilaza maana akumaliza shule lakini hana baba wa kumlea kwa kuwa baba yuko jela. Hivyo basi mtoto atakua kwa shida na wengi huishia mtaani kama adhabu ya kosa la wazazi wake.

Nini kifanyike

1. Nashauri sheria na sera zetu ziwe na exceptional option yaani kwa mfano Endapo itatokea mazingira kama hayo yametokea mama yaani aliyepata mimba ndio awe final say katika decision ya nini kifanyike kwa baba yaani aliyempa mimba kama atachagua kumfunga basi afungwe la ataki basi aachwe walee mtoto wao.

2. Mtoto wa kike aliyebakwa au kupata mimba kwa makosa ambayo ni ya sisi Jamii mfano ukosefu wa mabweni kama atutaki arudi shule basi tumpeleke vyuo vya ufundi stadi kama VETA ili apate ujuzi wa kumuwezesha kumlea mtoto angalau tuepuke laana ya kumuadhibu mtoto asiye na hatia

Mengine mnaweza kuongezea kushauri tujenge nchi kama taifa
 

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,246
2,000
ukizaa lazima uende kulea mwanao, why umunyime mwanao riziki eti unaenda shule..!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom