Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,052
- 24,442
Jamani hili janga la corona siyo la kitoto!
Kama imefikia watu kulazimishwa kukaa ndani kwa viboko na wengine kufungulia simba mtaani, kwa kuhakikisha usalama wa wananchi basi ni dhahiri kuwa hili gonjwa ni tata sana!
Sasa kwa hapa kwetu tz hayo hayajafanyika ya kuwafungia watu ndani!
Licha ya jitihada za serikali zinazofanyika kwa kutoa elimu lakini bado wananchi wanaona ni kitu cha kawaida tu au pengine ni kitu ambacho hakipo!
hali ya mitaani kwa kweli sidhani kama wenye mamlaka wameona hili! Ipo hivi humo mtaani kuna watu wanaumwa aisee, wapo wanaoonekana wanakohoa, wakiwa na mafua pamoja na kusema wanajisikia vibaya lakini wanaendelea kutembea mitaani huko na kuendelea na shughuli zao za kawaida za kila siku kwa kujichanganya na umma!
Wengine wapo pia wenye dalili zinazofanana na zilizoainishwa za corona ila wanaficha, pengine kwa kuogopa kuwa wakisema watatengwa au watazua taharuki maeneo wanayoishi hivyo huamua kujitibu wenyewe kwa kununua panadol huko pharmacy na kuzitumia...
Licha ya wizara na wadau kutoa maelekezo namna ya kujikinga na kutoa taarifa pale unapopata dalili za ugonjwa huu, bado watu ni wachache wanaofuata hayo maelekezo!
Mathalani daladala bado zinakaza abiria, mwendokasi vile vile abiria wanalundikana!
Kwenye bajaji huko ndio wanakaa hakuna hewa, distance ni zero so tutegemee nini hapa!
ni wazi hili gonjwa lipo mtaani na watu wengi yawezekana kabisa wameukwaa ila kwa ubishi au kutokujua watu wanaendelea kuusambaza!
Naamini hata wanajf wapo ambao wameshaugua au wanaugua kwa sasa na wanadalili zinazofanana kabisa na za corona ila wapo mtaani na hata sasa wapo sehemu za umma wakiendelea na shughuli zao kama kawaida!
Jitihada zaidi zinahitajika, mambo yakiiva tutaanza kutupiana mpira! Tuambe kwamba kama wapo walioupata huu ugonjwa na wapo mtaani wanakula mitishamba basi madhara yasiwe makubwa au yasitokee kabisa!
Nawasilisha...
Sent from my iPhone using JamiiForums